Facebook Comments Box

Monday, February 18, 2013

MH PINDA ALIPOKUTANA NA VIONGOZI WA KIISLAM NA KIKRISTO KUJADILI MGOGORO WA UCHINJAJI NYAMA

 
 Sheikh Hasani Kabeke wa Mwanza  akichangia katika kikao cha klutatafuta muafaka kati ya Waislamu na Wakristo kuhusu uchanjaji wanyama kilichoitishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Banki  Kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013
 
 Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba.
 Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijadili jambo na Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Ahmed  Ali (kushoto) na Sheikh wa msikiti wa Buswelu, Athumani Ali  katika kikao cha kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kati ya Waziri Mkuu na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013.
Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba akichangia katika kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Viongozi wa dini za Kikristo na Dini ya Kiislamu cha kujadili mgogoro wa uchinjaji  wanyama kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu  jijini Mwanza Februari 16,2013.


Sunday, February 17, 2013

HII NDIO IDADI YA WATU WALIO KAMATWA MPAKA SASA KWA TUKIO LA KUPIGWA RISASI PADRI ZANZIBAR




MBELA ASKARI ALIEKATWA MIKONO ANATUMIA MIGUU KULIMA

 
 
PAMOJA na kuwa na ulemavu wa kutokuwa na mikono yote miwili, Salim Mbela mkazi wa eneo la Delux, nje kidogo ya mji wa Songea, amefanikiwa kulima shamba la mahindi kubwa na zuri kwa kutumia miguu yake.
Ukiliona shamba hilo la Mbela licha ya kuwa na mahindi, pia lina maharage, magimbi na ndizi yaliyostawi na kupendeza.
Huwezi kuamini kuwa shamba hilo linalimwa na Mbela, ambaye ni mlemavu kwa kutumia miguu yake.
Ulemavu huo umemkuta na kulazimika kulima kwa miguu, baada ya kukatwa mikono yake alipokuwa akidai kurejeshewa mahari kutoka kwa wakwe zake.
Mbela anasema kuwa pamoja na ulemavu alioupata ukubwani, hawezi kutembea mitaani kuomba omba, wakati bado mwili wake una viungo vingine anavyoweza kuvitumia kujipatia mahitaji yake ya kila siku.
Kilichosabisha kukatwa mikono
Mbela alizaliwa miaka 53 iliyopita akiwa na mikono miwili na mwenye afya tele, lakini misukosuko ya maisha imemfanya leo abaki hana mikono yake miwili, huku akiishi peke yake.
Anaeleza kuwa kabla ya kuwa mlemavu, aliwahi kuajiriwa na Jeshi la Polisi, akifanyia kazi Kituo cha Polisi Makuyuni mkoani Arusha miaka ya nyuma, lakini alicha kazi hiyo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Baada ya hali hiyo, aliona bora arudi nyumbani kwao Kijiji cha Malumba wilayani Tunduru ili kuendelea kupata matibabu.
Mbela anasema kuwa alipofika kijijini kwao, aliendelea kupata matibabu na baadaye akapona.
Akizungumza kwa kusaidiwa na rafiki yake wa karibu ambaye amejitambulisha kwa jina la Zacharia Dikala, maarufu kama Babu Masai, Mbela anasema kuwa alikutana na matatizo ya kukatwa mikono miaka minne iliyopita.
Mbela ambaye pia ni baba wa watoto Mwanabibi Salim (28), Siku Salim (19) na Said Salim (24) anaeleza kuwa akiwa na mkewe na familia yake, siku moja ali kwenda nyumbani kwa wakwe zake waliokuwa wakiishi katika kijiji hicho cha Malumba na kuchukua mbuzi wake aliotoa mahari miaka ya nyuma wakati akimchumbia mkewe ambaye ndiye aliyemzalia watoto hao.
Anasema kuwa wakati huo alikuwa na nguvu na alitumia mabavu kufanya fujo, hadi akafanikiwa kufika zizini na kupora mbuzi, bila kujua kama maisha yake yange badilika na kuishia pabaya.
Hata hivyo, anajutia kitendo hicho akisema kwamba iwapo angefahamu mapema yataka yomkuta, asingethubutu kwenda kufanya fujo hizo.
“Nilikuwa najiamini sana, nilikuwa na nguvu sana, nikaamua kwenda ukweni kwangu kufuata baadhi ya mifugo yangu, niliyotoa mahari wakati namposa mke wangu,” anasimulia na kuongeza:


CHUO CHA ST JOHN'S DODOMA CHAFUNGWA BAADA YA WANAFUNZI KUGOMA

Chuo Kikuu cha St John’s cha mkoani Dodoma kimefungwa baada ya wanafunzi kususia mitihani wakituhumu na kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa na wahadhiri kwa kuwangusha kwenye mitihani na baadhi kuwabaka wanafunzi wa kike.

Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Gabriel Mwaluko, wanafunzi zaidi ya 290 wamesimamishwa masomo baada ya kukiuka sheria na kugomea mitihani, hivyo chuo kimefungwa kikisubiri taratibu za kinidhamu kuchukuliwa.

Awali uongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo ulieleza kuwa wanafunzi 290 wa St John’s na vyuo vikuu vishiriki vya Dar es Salaam walisimamishwa masomo huku uongozi wa chuo ukiwapa barua za kuwaondoa chuoni kuanzia wiki hii.

Habari hizo zilisema wanafunzi 196 wanaosoma Dodoma na wengine 94 wanaosoma katika vyuo vishiriki vya St. Mark's na Town Centre vya jijini walipewa barua za kuondolewa chuoni.

Rais wa serikali ya wanafunzi, Andrew Chiduo, akizungumza na NIPASHE Jumapili, alisema hatua ya kuwasimamisha inalenga kuwatisha ili kuendelea kuwalinda walimu wanaodaiwa kuwanyanyasa na kuwadhalilisha na kwamba wanasusia kufanya mitihani inayofanyika mwezi huu. Alisema wahadhiri wanalazimisha kufanya ngono na wanafunzi wa kike, kuwabaka na wale wanaokataa wanaangushwa kwenye mitihani.

Alisema katika tukio la hivi karibuni muhadhiri (jina tunalo) alituhumiwa kumbaka mwanafunzi baada ya kumhadaa kumpa mitihani mingine baada ya kushindwa ile aliyofanya mhula uliopita. Alisema wamelazimika kugomea mitihani baada ya mhadhiri mmoja (jina linahifadhiwa) kuwafelisha kwa makusudi wale wanaochukua kozi ya biashara wa mwaka wa kwanza huku akiwapa vitisho.

Akijibu tuhuma hizo Profesa Mwaluko alisema madai ya mwalimu kumbaka mwanafunzi yanachunguzwa kwa kuwahusisha polisi, kadhalika alisema mhadhiri anayetuhumiwa kuwafelisha wanafunzi madai yake yanafuatiliwa pia.


KATUNI YA KIPANYA KUHUSU VIKAO VYA BUNGE KUTOKUWA LIVE

Picture

HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOPIGWA MOJA NA LIBOLO


Mshambuliaji wa timu ya FC Libolo ya nchini Angola, Joao Martins, akiruka juu kupiga mpira wa kichwa na kuifungia timu yake bao la kuongoza mnamo dakika ya 24 ya mchezo katika kipindi cha kwanza,wakati wa mchezo wao wa Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya Timu ya Simba kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.hadi mwisho wa mchezo Simba ilechezia kichapo cha Bao 1-0 toka kwa FC Libolo

Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa akimtoka mchezaji wa Recreativo de Libolo ya Angola,Dario Cardoso katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Libolo ilishinda 1-0.

Ngassa akimtoka beki wa Libolo, Antonio Cassule

Haruna Chanongo wa SImba akipasua katikati ya wachezaji wa Libolo

Ngassa akimtoka Cassule

Ngassa na Cassule

Kiungo wa Simba SC, Amri Kiemba (kushoto) akiwania mpira dhidi ya beki wa Libolo, Pedro Ribeiro kulia

Simba na Libolo wakiingia uwanjani

Kikosi cha Libolo leo

Simba wakiomba dua na nyuma yao ni Libolo pia wakiomba dua 

Kikosi cha Simba SC leo

Wachezaji wa Simba SC wakiwapungia mikono mashabiki wao kabla ya mechi

Mrisho Ngassa akipiga krosi baada ya kufanikiwa kumtoka beki wa Libolo

Kipa wa Simba, Juma Kaseja akienda kuokota mpira nyavuni baada ya Libolo kufunga bao

Libolo wakiwapungia mikono mashabiki wao baada ya mechi kuwashukuru kwa kuwashangilia

Haruna Moshi 'Boban' (kushoto) akipiga shuti mbele ya beki wa Libolo

Beki wa Simba, Juma Nyosso akimiliki mpira  mbele ya beki wa Libolo

Haruna Chanongo akipasua katikati ya mabeki wa Libolo

Kiungo wa Libolo, Manuel Lopez akiondoka na mpira baada ya kumzidi maarifa Mwinyi Kazimoto wa Simba SC

Manuel Lopez kulia akigombea mpira na Mwinyi Kazimoto wa Simba SC kushoto

Mwinyi Kazimoto akigombea mpira wa juu na kiungo wa Libolo

Beki wa Simba SC, Shomary Kapombe akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Libolo

Haruna Moshi 'Boban' akimtoka beki wa Libolo

Amri Kiemba akimtoka beki wa Libolo

Mwinyi Kazimoto wa Simba akigombea mpira wqa juu na kiungo wa Libolo


HAKI YA KUCHINJA WANYAMA: DESTURI ILIYOPO IENDELEE - WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ameagiza kuundwa kwa kamati maalumu itakayohusisha pande mbili za waumini wa dini ya Kiislam na Kikristo, ili ishughulikie mgogoro mbichi unaohusu haki ya kuchinja wanyama. Waziri Mkuu aliyasema hayo jana alipofika mkoani Mwanza na kufanya kikao -kilichodumu kwa saa tano- na wawakilishi wa madhehebu ya dini hizo mbili ikiwa ni hatua ya kutafuta njia ya kutatua mgogoro wa nani mwenye haki ya kuchinja wanyaka kati ya waumini wa dini hizo mbili. Kwa wakati huu, Waziri Mkuu amesema shughuli hiyo iendelee kufanywa kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa desturi zilizokuwepo hadi hapo yatakapofikiwa na kutolewa maagizo mapya. Waziri Mkuu ameagiza kamati hiyo ifanye shughuli zake na kuwasilisha ripoti yake Serikalini haraka iwezekanavyo kwa ajili ya hatua zaidi za kimaamuzi. Hata hivyo, hadi Waziri Mkuu anaondoka katika kikao hicho, Waislam waliridhia kuundwa kwa Kamati hiyo wakati Wachungaji na Mapadre walikataa. Waziri Mkuu alikumbushia kuwa suala hili ni la kiimani na ijapokuwa Serikali haina dini, wananchi wake wanazo imani kwa mujibu wa dini zao hivyo ni vyema Wachungaji, Mapadre na Masheikh wakawasihi waumini wao kuwa na subira hadi hapo utakapopatikana ufumbuzi mwingine. Waziri Mkuu pia ameonya kuhusu redio mbili ambazo zimenyooshewa vidole na waumini wa pande zote mbili kuwa zinachochea uhasama wa kidini. Akazitaja kuwa ni redio Imani iliyopo Morogoro na redio Neema iliyopo mkoani Mwanza na kuzionya kuhusu mafundisho yake ambayo ikilazimu, Serikali itachukua hatua dhidi yake.


PADRE MUSHI APIGWA RISASI NA KUFA LEO ASUBUHI

Taarifa kutoka Zanzibar zikiripotiwa na mwanahabari Donisia Thomas wakati kipindi cha Patapata cha WAPO radio FM kinaendelea, zinasema kuwa Padre Evaristus Mushi wa Kanisa la Parokia ya Minara Mirefu huko Zanzibar amepigwa risasi majira ya saa moja asubuhi -na watu wasiofahamika- na kufariki dunia.

Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na madaktari kutoka hospitalini alikopelekewa katika harakati za kuuokoa uhai wake.

Padre Mushi aliuawa akiwa anashuka kwenye gari lake tayari kuingia Kanisani kwa ajili ya kuendesha misa ya kawaida ya Jumapili katika kanida la Mtoni, mjini St. Joseph. Inaelezwa kuwa gari lisilofahamika lilifika na kufyatua risasi zilizomlenga Padre Mushi sehemu ya kichwani na hivyo kumsababisha majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.

Mwanahabari anasema tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa waumini ambao wamekataa kuahirisha ibada iliyokuwa iendeshwe na Padre huyo na kusema ikiwa kusudio ni kuwaangamiza Wakristo wote, basi na waangamizi wafike Kanisani wawaangamize wakiwa pamoja.

Jeshi la Polisi limeshafika katika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.



Saturday, February 16, 2013

JE, PICHA HII INATOSHA KUTHIBITISHA KUWA HUYU NDIO MPENZI MPYA WA DIAMOND?

katika kusheherekea siku ya wapendanoa mwanamuziki kipenzi cha warembo Diamond "rais wa wasafi" aliamua kuweka picha yake na anayesadikiwa kuwa mpenzi wake mpya Penny Mungilwa kwenye mtandao wa Instagram. Kitendo hicho hakikuwapendeza watu wengi ambao watu wengine walimshambulia na kumwambia awe na heshima na wanawake. Picha hiyo ambayo ilifanyiwa mabwebwe ili ionekane kama ya zamani kidogo na isionekane vizuri iliwashitua washabiki wengi. Mmoja wa washabiki wake waliokerwa ni anaejulikama kwa jina la someaglymofo.




FULL TIME: AZAM 3 - 1 Al NASIR JUBA

FULL TIME AZAM 3 - 1 AL NASIR JUBA

Dk 94 Gooool Kipre Cheche anaiandikia Azam bao la tatu

Dk 90 zimeongozwa dakika 4

Dk 89 wachezaji wa Al nasir wamekuwa wakijidondosha dondosha ili kupoteza muda

Dk 80 Azam 2 - 1 Al Nasir

Dk 81 Goooool Kipre cheche anaipatia Azam goli la pili

Dk 80 Azam 1 - 1 Al Nasir 

DK 72 kipre cheche anapiga shuti kali kipa wa Al Nasir anatoa nje

Dk 71 John Boco anapiga kichwa kipa wa Al Nasir anaokoa na kuwa kona

Dk 70 Azam 1 - 1 Al Nasir 

Dk 65 Azam 1 - 1 Al Nasir azam wanapata faulo karibia na 18

Dk 59 anatoka Abdi Kassim anaingi John Boco

Dk 52 Azam wanakosa bao. Mpira unagonga mwamba

Dk 48 Abdi Kasim anakosa tena goli la wazi hapa

HT Azam 1 - 1 Al Nasir

Kipindi cha pili kimeanza

Dk 46 Kipa natokea goli linabaki wazi ila Mcha Hamis anapiga mpira nje

Dk 45 Refa anaongeza dakika 3 za ziada

Dk 44 Abdi Kassim "Babi" anakosa goli la wasi kwa kupiga mpira fyongo ndani ya 6

Dk 43 Abraham Malik Sadik wa Al Nasir anaonywa na refa kwa kuoneshwa kadi ya njano

Dk 38 Goooool Al Nasir wanasawazisha hapa. Jacob Osuru anawainua wasudani

DK 37 Azam wanapata kona baada ya piga nikupige kwenye lango la Al Nasir

Dk 30 Azam 1 - 0 Al Nasir

Dk 27 Beki wa Azam anateleza na kuipa nafasi Al Nasir ila Mwadini Ally Mwadini  okoa hatari ile

Dk 21 Abdi Kassim Babi anakosa bao la wazi kipa anautoa mpira

Dk 19 Simon Amanya anaonywa kwa kuoneshwa kadi ya njano. Mcha Hamis anaenda kupiga faulo na inatoka nje

Dk 18 kipre cheche anaingia ndani ya 18 na kutoa pasi ambayo inatolewa nje na beki. Azam wamekuwa wakilisakama lango la wasudani sana

Dk 16 Azam inafanya mabadiliko, ametoka Brian Umony ameingia Khamis Mcha.

Dk 14 Gooo...! Abdi Kasim anaipatia Azam bao la kwanza kwa kichwa akiunga krosi ya Kipre Tcheche. Azam 1-0 Al Nasir.


Dk 13 Azam 0 - 0 Al Nassir Juba

Kikosi cha Azam FC kitakachoshuka Uwanja wa Taifa leo jioni kuikabili Al Nasri Juba ya Sudan Kusini kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kinaundwa na

Mwadini Ally (GK), Himid Mao, Malika Ndeule, David Mwantika, Jockins Atudo, Michael Bolou, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Humphrey Mieno, Brian Umony, Abdi Kassim ‘Babi’ na Tchetche Kipre.

Sub: Aishi Salum, Luckson Kakolaki, Khamis Mcha ‘Vialli’, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aziz, Abdulhalim Humud, Seif Abdalah ‘Karihe’, Gaudence Mwaikimba, Seleman Uhuru na Omari Mtaki

Benchi la ufundi: Kocha Stewart Hall, msaidizi Ibrahim Shikanda, kocha wa makipa Idd Abubakar, Daktari Mwanandi Mwankemwa na Paul Gomez

All the Best Guys!
God Bless Azam FC, God Bless Tanzania!


TENGA AMCHINJIA BAHARINI MALINZI, AMWAMBIA; "KAKA NENDA FIFA TU, HAPA UMEKWAMA"


Rais wa TFF, Tenga akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo Uwanja wa Taifa

Na Mahmoud Zubeiry
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba wagombea walioenguliwa na Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wana namna mbili tu za kufanya ili kutafuta haki yao, moja kuomba pingamizi dhidi yao kusikilizwa tena au kwenda Mahakama ya Usuluhishi ya Soka (CAS), iliyo chini ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). 
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF, Tenga amesema kwamba TFF ilijiwekea utaratibu ambao lazima uheshimiwe.
Alisema mchakato wa uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Februari 24, mwaka huu ulianza vizuri na umeendelea vizuri hadi kufika hapa ulipo, ingawa amekiri kuna matatizo.
Tenga alisema kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa TFF, Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ndiyo chombo cha mwisho na mtu anapokwama hapo hana pa kwenda zaidi ya CAS.
Kauli hiyo ya Tenga imefuatia Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake Iddi Mtiginjola kumuengua mgombea wa nafasi ya Urais, Jamal Malinzi kwa madai mawili, kukosa uzoefu na kupinga waraka wa mabadiliko ya uchaguzi. 
Taarifa ya Mtiginjola Jumatatu, ilisema kwamba mgombea pekee aliyepitishwa katika nafasi ya Urais, inayoachwa wazi na Tenga anayeng’atuka ni Athumani Jumanne Nyamlani.
Malinzi aliwekewa pingamizi awali, lakini akashinda mbele ya Kamati ya Uchaguzi na baadaye akakatiwa Rufaa, ambayo imemuengua. 
Nyamlani pia aliwekewa pingamizi, akashinda na akakatiwa Rufaa lakini pia ameshinda, baada ya pingamizi alilowekewa kutupiliwa mbali.
Wengine walioenguliwa ni Michael Wambura aliyekuwa akiwania nafasi ya Makamu wa Rais na Ahmed Yahya aliyekuwa akiwania nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Ligi.
Hata hivyo, Tenga amesema kwamba tayari Malinzi na Mohamed Yahya wameomba kusikilizwa upya  kwa pingamizi dhidi yao.
Kufuatia matatizo haya, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Jumanne wiki hii iliamua kusimamisha kampeni za uchaguzi wa shirikisho hilo zilizopangwa kuanza Jumatano, kuelekea uchaguzi huo Februari 24, mwaka huu.
Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Lyatto ilisema kwamba, Kamati yake imechukua hatua hiyo kutokana na Mamlaka iliyonayo Kikatiba.
“1. Kamati ya Uchaguzi, kwa mamlaka iliyonayo,  kupitia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 3(1), 6(1) (g) na (l), 10(5), 11(6) inayosomeka pamoja na Ibara ya 14(1) na (2) na pia Ibara ya 26(5) na (6), imesitisha zoezi la kampeni za uchaguzi wa TFF na TPL Board lililokuwa lianze kesho tarehe 13/02/2013 hadi hapo itakapowatangazia, ili kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF,”imesema taarifa hiyo.
Aidha, Taarifa ya Lyatto imesema; “2. Tarehe za Uchaguzi Mkuu wa TFF na TPL Board zinabaki kama zilivyopangwa. 3. Taarifa hii inazingatia pia Ibara ya 2(4) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF inayoagiza uongozi uliopo madarakani kuendelea na kutekeleza majukumu ya Shirikisho hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika,”.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU