Facebook Comments Box

Sunday, December 15, 2013

OKWI ATUA YANGA

Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.

Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.

Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania linafungwa leo usiku  Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa kihistoria  klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.

Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji  watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.

Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.

Baraka Kizuguto

Afisa Habari – Young Africans SC

Disemba 15, 2013.


VIDEO: HOTUBA ALIOTOA RAIS KIKWETE KWENYE MSIBA WA MANDELA LEO




NIKIWA RAIS NITARUHUSU POMBE HARAMU YA GONGO NA SILAHA HARAMU-DR SLAA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.

CHANZO: NIPASHE



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU