Facebook Comments Box

Wednesday, September 17, 2014

SAMAKI ALIEFANYIWA OPERATION YA UBONGO ANAENDELEA VIZURI



Samaki aina ya Goldfish, anaendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji kutolewa uvimbe kwenye ubongo wake. Upasuaji huo umesemekana kufanywa kwa uangalifu mkubwa kutokana na hofu yatisho kwa maisha ya Samaki huyo. Samaki huyo kwa jina George, ambaye mmiliki wake anaishi Melbourne, alidunguwa sindano ya kuondoa fahamu iliyogharimu dola 200.

Daktari Tristan Rich, aliyefanya upasuaji huo, aliambia kituo cha redio cha 3AW mjini Melbourne kuwa Samaki huyo kwa sasa amepata fahamu na tayari ameanza kucheza na kuogelea majini.
Wataalamu wa matibabu ya wanyama, wanasema kuwa Samaki huyo mwenye umri wa miaka 10, anatarajiwa kuiishi kwa miaka mingine 20.

"George alikuwa na uvimbe mkubwa sana kwenye ubongo wake na alikuwa anakuwa polepole sana, na hali hiyo ilikuwa inaanza kuathiri maisha yake,'' alisema daktari Rich kutoka hospitali ya matibabu kwa wanyama ya Lort Smith. Mmiliki wa George, alikuwa ameambiwa achague kati ya Samaki huyo kufanyiwa upasuaji au adungwe sindano ya kulala. 

Lakini aliona bora kujaribu kuokoa maisha ya Samakai wake na ndipo akakubali Samaki huyo afanyiwe upasuaji. Aliongeza kuwa Samaki huyo alisalia kuwa hai kutokana na madaktari kuweka hewa ya Oxygen kwenye maji wakati wa upasuaji


TRAFIKI ALIEGONGWA MBAGALA AFARIKI DUNIA

ASKARI wa usalama barabarani, aliyejulikana kwa jina moja la Riziki, WP 2806 CPL Riziki, aliyegongwa na daladala aina ya DCM wakati akiwa katika harakati za kutimiza majukumu ya kazi eneo la Mbagala Rangi Tatu Jijini Dar es Salaam jana asubuhi amefariki dunia leo.
Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
WP 2806 CPL Riziki, akiwa chini baada ya kugongwa na daladala eneo la Mbagala Rangi 3 jana kabla ya kukimbizwa hospitali.
WP 2806 CPL Riziki, akiwa chini baada ya kugongwa na daladala eneo la Mbagala Rangi 3 jana kabla ya kukimbizwa hospitali.


KASEJA,DIDA,PONDAMALI NA BECHI LA UFUNDI LA YANGA WANA SIRI NZITO.



Hali  katika  klabu  ya  Yanga  kwa upande  wa  walinda  milango  inaonekana  si shwari, hali  hiyo  ilijionyesha  dhahiri  wakati  wa  mchezo  wa  ngao  ya  jamii  ambao  pia  ni  maalumu  kama  mchezo  wa  ufunguzi  wa  pazia ya ligi  kuu  ya  Tanzania  al  maarufu  Vodacom  Premier  Leagu (VPL).  wakati  timu  hiyo  ya wana  Jangwani  walikuwa  wakimbana  na timu ya waoka mikate  Azam  Fc   (wana  lamba lamba.)

Kilichowashtua  wengi  ni kule  kutokuwepo  kwa  ushirikiano  hata  kidogo kwa walinda  milango  hao  kabla  ya  mchezo huo  kuanza, kwa  kawaida  wakati  timu inayoanza  huwa  inachukuliwa  na  mwalimu  msaidizi  kwa ajili  ya  kuwapa  mazoezi  ya  kupasha  misuli  joto  makipa  huwa  wanakuwa  na  mwalimu  wao huku  akiwafanyisha  mazoezi  kabla  ya  mchezo, hivyo  ndivyo  hali  ndiyo  ilivyokuwa  kwa  upande  wa  Azam  wakati  wachezaji  waliokuwa  wanatarajiwa  kuanza  walikuwa  na  Trainer (mkufunzi) wao  Ibrahim  Shikanda  mchezaji  wao wa  zamani  wale  wa  akiba  wao  walikuwa  na  mwl  Kally  Ongara  akiwapasha joto  kwa  kufanya  nao  mazoezi  mepesi  mepesi, kwa  upande  wa  makipa  wao  walikuwa  na  mwalimu  wao  Idd  Abubakar  ‘Phantom’  aliyekuwa akiwafanyisha mazoezi  ya  kwa pamoja  huku  wakishirikiana  na  hata  walipomaliza  walikusanyika  wao  watatu  mwalimu  Idd  Abubakar, Mwadini  Ally  na  Ayishi  Manula  kwa  pamoja  wakaomba  dua  bila  kujali  nani  anaanza  katika  mchezo  huo  ndiyo  wakaenda  ndani  kwenye  vyumba  vyao  vya  kubadilishia  nguo.

Kwa  upande  wa  yanga  wao  wale  wanaonza  walikuwa  na  mwalimu  Salvatory  Edward  na Mwalimu  wao  Mbrazil  Leiva,wale  wasioaanza  kwenye mchezo  ule  wao  walikuwa  wakisimamiwa  na  mwalimu  Shedrack  Nsajigwa "FUSO" huku  wakifanya  mazoezi  mepesi. 

Kazi  ilikuwa  kwa  walinda mlango  wao sasa ndiyo  walioonekana  hawakuwa  na  ushirikiano  hata  kidogo  kuanzia  walipoingia,  Dida  alikuwa  mbele  ya  wachezaji  wakati  Kaseja  yeye  alikuwa  yuko  nyuma  ya  wachezaji  wengine  na  hakuna  sehemu  yoyote  ambayo  walishirikiana  hata  mmoja  kumpa  mwenzake  mpira  kitu  ambacho  si cha  kawaida  kwa  walinda  milango  na  aina  ya  mazoezi  wanayoyafanya  kabla  ya  kuanza kwa  mchezo hicho  ni  kitu  cha  kwanza.

Kitu cha pili, hata mwalimu wao Pondamali yeye  hakujishughulisha  na  kumuandaa  Kaseja  pia  kwa  ajili  ya  mchezo  huku  akijua  kwamba  hata  dakika  ya  10  tu  ya  mchezo  Dida  akiumia  atayeiingia  ni  Kaseja  ambaye  yeye  alikuwa  hajishughulishi  kabisa  na  kumuandaa  kimchezo  hali  ambayo  ilizusha  maswali  kwa wale  baadhi  tu  tuliogundua  kitu  hicho  na baadhi  yetu  tukawa  tunakwama  yupi  yuko  sahihi  kwa  kuwaandaa  makipa  kwa  kile  kilichokuwa  kinaendelea  pale  uwanjani  kati  ya  mwalimu  Pondamali   wa  Yanga  na  mwalimu  Idd  Abubakar  wa  Azam  bila  kupata  majibu.

 kitu  cha  tatu  na  cha  mwisho  ambacho  ni pale  Kaseja  alipojitenga  kabisa  na  Pondamali  na  Dida.
wakati  wao  wakiendelea  na  mazoezi  yeye  alikuwa  pembeni  kabisa  akicheza  ule  mchezo  maarufu  sana  dana  dana  huku  akifanya  manjonjo  ya  kuuchezea  mpira  peke  yake  mpaka  alipopata  msaidizi  na  yeye  kwa  kuwa  anapigiwa  mpira  na  mtu  wa  vifaa  wa  Yanga.

Hii  si  kawaida  kitimu  na  haijawahi  kutokea  kwenye  timu  yeyote  walipokuwa  pamoja  kuanzia  Simba  na  hata  Timu  ya  Taifa   Stars  na  hata  pale  Kaseja  alipokuwa  na  Ivo  Mpaunda  Timu  ya  taifa  haijawahi  kujitokeza  hali  ya  namna  hii  kiasi  cha  wadau  pia  kuona  kuwa  Pondamali  pia  ni  chanzo  cha  kuwagawa  makipa  hao  kwa  kuwa  yeye  kama  mwalimu  wao  haonyeshi  jitihada  za  kutaka  kuonyesha  kuwe  na  ushirikiano pale  wanapokuwa  kwenye  mechi  kama  ilivyokuwa  katika  mchezo  huo  wa  ngao. 

Ndiyo  maana  kitongoni  inahisi  kuwa  kuna  siri  nzito  ndani  ya  Yanga  inayowahusisha  Juma  Kaseja, Deo  Munishi  Dida, mwalimu  wao  Juma  Pondamali  Mensah  na  huenda  hata  Benchi  zima  la ufundi  chini  ya  Mbrazil  Maxio  Maximo  wanajua  nini  kinaendelea  katika  wawili  hao  na  jitihada  zetu  za  kuzitafuta  pande  zote  3 zinaendelea. 


PROF JAY ft DIAMOND - KIPI SIJASIKIA (Official Video)



WASHIRIKA WA MAENDELEO WARIDHISHWA NA UJENZI WA KITUO CHA UMEME CHA KINYEREZI

Baadhi ya Washirika wa Maendeleo wakipita jirani na unapojengwa mmoja wa mitambo wa kupokea gesi katika eneo la Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam, walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupokea gesi.

Pichani ni mmoja wa Mtambo wa kuzalisha umeme ambao ni miongoni mwa mitambo itakayotumiwa katika kuzalisha kiasi cha megawati 150 za umeme katika Mradi wa Kinyerezi I.
 
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi, Saimoni akiuleza jambo ujumbe wa Washirika wa Maendeleo wakati walipotembelea kuona maendeleo wa ujenzi wa mradi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, akiwaongoza Washirika wa Maendelo kuangalia namna utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme na kituo cha kupokea Gesi unavyoendelea katika eneo la Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni mojawapo ya mapipa yatakayotumika kuhifadhi mafuta ambayo yatatumika wakati wa dharura.

Washirika wa Maendeleo kutoka taasisi mbalimbali nchini waliotembelea Mradi wa kuzalisha Umeme  wa Kinyerezi I na kituo cha kupokea Gesi  wameeleza kufurahishwa na kuridhika na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.

Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier, akiongea kwa niaba ya washirika hao ameeleza kuwa, wameridhishwa na hatua ambazo miradi hiyo imefikia na kupongeza jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba inafanyia kazi changamoto ya upatikanaji umeme wa uhakika Tanzania. Pia Dongier ameitaka Serikali kushirikiana na wadau katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya umeme ili iweze kufikia lengo lake la kuhakikisha Tanzania inazalisha umeme wa kiasi cha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza wakati ujumbe huo ulipotembelea kituo cha kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150 na  kituo cha kupokea gesi katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim  ameeleza kuwa, Wizara imeona ni jambo la msingi kwa wadau hao kutembelea miradi hiyo ili kujionea hatua mbalimbali ambayo miradi hiyo imefikia.

Aidha, Maswi ameongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, imedhamiria kuleta mabadiliko ya kiuchumi kupitia sekta ya nishati hususani kupitia gesi asilia na kuongeza kuwa, hakuna kinachoshindikana hivyo, miradi hiyo inatarajiwa kukamilishwa kwa wakati kama ilivyopangwa.

Kwa mujibu wa Meneja Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba, ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo cha kupokea gesi cha Dar es Salaam umekamilika kwa asilimia 60. Naye Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

 Mhandisi, Saimoni Jilima ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo hicho umekamilika kwa asilimia 70.Washirika wa Maendeleo  waliotembelea miradi hiyo ni pamoja na  Benki ya Dunia, GIZ, USAID, MCC, Korea Exim Bank, Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB),DFID, Umoja wa Ulaya,Ubalozi wa Sweden, Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Ujerumani na Ubalozi wa Ufaransa


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU