Wakati straika Emmanuel Okwi akiwa Dar es Salaam, timu yake ya
Etoile du Sahel imeendelea kufulia na kuitaka Simba imchukue mchezaji
huyo ili mambo yaishe juu kwa juu.
Simba iliipa Etoile du Sahel mpaka Septemba 30
mwaka huu iwe imelipa Sh 480 milioni za kumnunua mchezaji huyo, lakini
hilo halijafanyika mpaka sasa.
Wiki iliyopita, Simba iliandika barua kwenda kwa uongozi wa Etoile du Sahel, lakini timu hiyo ya Tunisia haijajibu lolote.“Jamaa wana hali mbaya kiuchumi, wanatulazimisha
tumchukue Okwi, halafu watulipe fedha kidogo kama fidia, lakini bado
sisi hatuafiki tunasubiri mpaka hiyo Septemba 30.
Wakishindwa tunakwenda moja kwa moja Fifa,” alisema mmoja ya viongozi wa Simba jana Jumatatu.“Okwi mwenyewe yupo tayari kurudi Simba wakati wowote, lakini ngoja kwanza tusubiri hiyo Septemba 30 ambayo ndio siku ya mwisho tuliyokubaliana na Etoile du Sahel,” alisema.

Okwi mwenyewe ambaye yupo Dar es Salaam aliliambia
Mwanaspoti jana Jumatatu kuwa amekuja nchini kwa mapumziko mafupi na
kutuliza akili yake.
Katika mechi ya Jumamosi iliyopita, mashabiki
walitaka kumvalisha Okwi jezi na skafu zenye nembo ya Simba, lakini
alikataa kwani angekuwa anakwenda kinyume na mkataba wa Etoile du Sahel.
Okwi yupo nchini baada ya kualikwa na rafiki yake
Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Simba, Abdulfatah Saleh, ambaye ndiye
mmiliki wa hoteli ya Sapphire.
CHANZO:Mwanaspot
CHANZO:Mwanaspot