Facebook Comments Box

Thursday, January 24, 2013

SIMBA 'B' YAFUNGWA NA CHUI

Baada ya kipigo cha mara mbili mfululizo kutoka kwa timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, timu ya Black Leopards ya nchini Afrika ya Kusini, leo imepunguza machungu yake kwa kuichapa Simba ya jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Hata hivyo imeelezwa kuwa kutokana na hofu Klabu ya Simba iliwachezesha wachezaji wa timu B, jambo ambalo limewakera hadi mashabiki wa Simba waliokuwapo uwanjani hapo leo, ambapo baadhi ya mashabiki waliohudhuria mtanange huo uwanjani hapo walisikika wakilalama kwa kitendo hicho, ambacho kimeelezwa kuwa ni sehemu ya hofu na dharau.

Katika Kikosi cha simba wameonekana wachezaji wanne tu walio katika kikosi cha kwanza cha ligi kuu. huku wachezaji wote waliobaki wakiwa ni wa kikosi cha pili, ambao wengi wao wakiwa ni wchezaji wa kikosi cha timu B ya klabu hiyo.
Simba kupitia makamu mwenyekiti wake Godfrey Nyange Kaburu jana ilithibitisha kwamba watachezesha kikosi cha kwanza baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba walikuwa na mpango wa kutaka kuchezesha kikosi cha pili cha timu hiyo, lakini Kaburu alizungumza kwenye Sports Xtra ya Clouds FM na kuthibitisha kwamba kikosi kilichotoka Oman ndio kitakachoshuka dimbani kupambana na Black Leopards.
Kitendo ilichokifanya Simba sio cha kiungwana kwa sababu imehairibia jina kampuni iliyoratibu mchezo huo ya Prime time promotions, ambao walitimiza kila kitu katika makubaliana yao na Simba ili wailete timu ya kwanza kucheza na Black Leopards lakini matokeo yake wakafanya kinyume na makubaliano. 


LULU KUACHIWA KWA DHAMANA KESHO IJUMAA 25/01/2013

. 
 Taarifa za uhakika zilizopo kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kwa jina la uigizaji 'Lulu' akatoka kwa dhamana kesho January 25, 2013. Kutokana na dhamana ambayo inatarajia kusikilizwa kesho Ijumaa.

Uhakika wa Lulu kupata dhamana ulikua jana jumatano january 23 lakini ikashindikana kutokana na kuahirishwa kwa sababu Jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za dhamana kilikua hakijatimia.
Chanzo cha kuaminika kilichoongea kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.

Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba, na baadae mashitaka yake yalibadilishwa na kuwa Ameua bila kukusudia, kitu ambacho kinampa nafasi ya kuweza kupata dhamana.




ARSENAL YAIBAMIZA WESTHAM EPL

Arsenal jana waliendeleza wimbi la ushindi katika Ligi ya Premia pale walipo wasambaratisha West Ham kwa ushindi wa bao 5-1 katika uwanja wao wa Emirates.
 Wafungaji wa mabao ya washindi walikuwa ni OLIVIER GIROUD(2), SAINT CAZORLA(1), THEO WALCOTT(1) na LUCASS PODOSKY(1).
Brace yourself: Olivier Giroud scored two goals in ten minutes as Arsenal ran riot at the Emirates on Wednesday
Olivier Giroud alifunga mabao mawili ndani ya dakika 10.


Unconscious: There were 12 minutes of injury time at the Emirates after a collision involving Danny Potts

Danny Potts

On target: Santi Cazorla popped up with the third goal for Arsenal after 53 minutes
Santi Cazorla akifunga bao la 3 dakika ya 53 


TIMU YA SIMBA YAWASILI SALAMA KUTOKA OMAN

Nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, baada ya kuwasili wakitokea Oman walipoweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.


Nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere,
Nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja akizungumza na shabiki wa timu hiyo, Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam 
Wachezaji wakmiwa kwenye basi lililowapakia kuwapeleka kambini

Mwanachama wa Simba, Makoye akimlaki Kocha Mfaransa Patrick Liewig

Kipa wa Simba SC, Abbel Dhaira akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
Kiungo wa Simba SC, Mussa Mudde akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere,.
Mshambuliaji wa Simba SC, Felix Sunzu akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere,
Mudde ..

Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo akitoka kwa furaha, 

Kaburu akimlaki Komabil Keita


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU