Monday, August 12, 2013
KIONGOZI WA SHIA TANZANIA AKEMEA VIKALI KITENDO ALICHO FANYIWA SHEIKH PONDA
Sheikh Hemedi Jalala |
Kiongozi wa Shia Tanzania Sheikh Hemedi Jalala ameungana na Masheikh na wanazuoni wengine wa kiislam kupitia ukurasa wake wa facebook kukemea kitendo alichofanyiwa Sheikh kipenzi cha waislam wengi na mpigania haki Sheikh Ponda Issa Ponda na kusema kuwa busara haikutumika na jeshi la polisi katika tukio hilo. Pamoja na kuto kukubaliana na mbinu anazotumia Sheikh Ponda bado Sheikh Hemedi Jalala amekubali kuwa Sheikh Ponda anapigania haki za Waislam wa Tanzania. Hapo chini ni maelezo aliyoyaweka Sheikh Jalala katika ukurasa wake huo
POLISI WAMUWEKEA ULINZI SHEIKH PONDA MUHIMBILI
Dar es Salaam/Moro. Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda yupo chini ya ulinzi huku akitibiwa
majeraha katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Sheikh Ponda alisafirishwa usiku wa manane kutoka
Morogoro baada ya juzi kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni mtutu wa
bomu saa 12:25 jioni alipokuwa akisindikizwa na wafuasi wake kwenda
katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja mara baada ya kumaliza kutoa
mhadhara katika kongamano mjini hapo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Sheikh Idd Mussa Msema, alidai kuwa Sheikh Ponda alipigwa risasi tatu begani.
Taarifa kutoka ndani ya familia ya Ponda zilisema
kwamba baada ya kupata taarifa za kupigwa risasi, baadhi ya masheikh
walifunga safari kwenda Morogoro na kumrejesha Dar es Salaam usiku
huohuo. Kabla ya kurudishwa Dar es Salaam, imeelezwa kuwa Sheikh Ponda
alipelekwa katika Zahanati ya Islamic Foundation.
Mmoja wa wanafamilia alidokeza kwamba Sheikh Ponda
alifichwa na alikuwa chini ya ulinzi mkali wa wafuasi wake na hakuna
aliyeruhusiwa kumsogelea.
Muhimbili
Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye jana
zilisema kuwa alifikishwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
Sheikh Ponda alifikishwa Muhimbili jana saa 7:18
mchana na alipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa wa dharura na baadaye
alitolewa na kupelekwa kwenye chumba cha x-ray kwa ajili ya vipimo.
Baadaye alipelekwa chumba cha upasuaji.
Eneo kubwa la hospitali hiyo lilikuwa na idadi
kubwa ya askari na mmoja wa askari waliokuwa doria hospitalini hapo
alisema walitawanywa kwenye hospitali mbalimbali za Dar es Salaam baada
ya kupata taarifa kuwa angeletwa kwa matibabu.
“Nakuambia tuko hapa tangu saa kumi na moja
asubuhi, tumetawanywa hospitali mbalimbali baada ya kupata taarifa kuwa
analetwa Dar. Bahati nzuri kaletwa hapa Muhimbili... tunasubiri apate
matibabu na tutamtia mbaroni,” alisema askari huyo.
Taarifa ya polisi
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema jana
katika taarifa yake kuwa Sheikh Ponda yuko Hospitali ya Muhimbili
akitibiwa baada ya kupata majeraha yaliyotokana na purukushani na polisi
wakati wafuasi wake walipokuwa wanataka kumtorosha
SOURSE:MWANANCHI
SAKATA LA ZAM TV: TENGA AOMBA KAMATI IMPE MAELEZO AZAM ILISHINDA VIPI ZABUNI YAKE
Sakata
la klabu ya Yanga kugomea kukubaliana na mkataba wa kati ya kamati ya
Ligi na Azam Media wa kuipa haki za matangazo ya televisheni ya mechi za
ligi kuu kituo cha Azam TV limechukua sura mpya baada ya Raisi wa
shirikisho la soka la nchini TFF Leogdar Tenga kuingilia kati.
Kwa
mujibu wa taarifa rasmi mtandao huu ulizozipata ni kwamba Tenga
amewaandikia barua Yanga akiwaambia kwamba amepata malalamiko yao dhidi
ya mkataba wa urushwaji wa matangazo ya mechi za ligi kupitia Azam TV.
Pia
Tenga amewaambia Yanga kwamba ameiomba kamati ya ligi kumpatia maelezo
namna mchakato mzima wa ugawaji wa tenda hiyo ulivyofanywa mpaka kufikia
maamuzi ya kuingia makubaliano na Azam TV.
Tenga
amewaomba Yanga kuwa wavumilivu ili kushughulikia malalamiko yao
kuhakikisha muafaka unafikiwa kwa ajili ya manufaa ya soka la Tanzania.
SOURSE: SHAFFIH DAUDA
Subscribe to:
Posts (Atom)