|
Mh Mbatia |
WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka hadharani majina ya wajumbe wa Tume ya Taifa ya Kuchunguza Matokeo ya mwaka 2012 ya Kidato cha Nne jana, baadhi ya wajumbe waliopewa heshima hiyo ya kusaidia kutafuta sababu za matatizo ya elimu na jinsi ya kuyatatua, Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel Oluoch, wamekataa uteuzi huo.
Mbatia katika hoja yake kwa waandishi wa habari jana, alisema kwa kuwa hadi jana hakuwa amepata taarifa ya maandishi kuhusu uteuzi wake, asingeweza kutamka kama amekubali au la, hadi atakapokuwa amepata maandishi hayo akisema atakapoyapata ndipo, “nitafanya uamuzi kwa maslahi ya pamoja ya Watanzania.”
Hata hivyo, habari za uhakika kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, zilisema Mbatia alifahamishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo kwa njia ya simu afike Ofisi ya Waziri Mkuu achukue barua yake ya uteuzi kama walivyofanya wajumbe wengine.
Oluoch alipotafutwa azungumzie uamuzi wake wa kujitoa kwa mujibu wa barua aliyoiwasilisha Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema yuko mkutanoni akaomba apigiwe baada ya nusu saa na ilivyofanyika hivyo, alikata simu kila alipopigiwa.
Ikiwa nia yetu ni thabiti ya na kweli ya kutaka kubadili mwenendo wa mambo yasiyo sahihi katika nchi ya Tanzania, hatuna budi kutii na kufuata sheria tulizojiwekea sisi wenyewe. Kama siyo kasuku, kila leo tunaimbiana misemo maarufu tunayonukuu kutoka kwa watu mahiri, mfano, “insanity: doing the same thing over and over again and expecting different results. ~Albert Einsten” na “walk the walk, talk the talk” (ingawaje hii tumeibadili tunavyojua kwa akili yetu ati, ‘walk the talk’ -- hakuna msemo kama huo! How do you walk the talk? Kupinda tu misemo ya wenyewe).
Sasa ikiwa Waziri Mkuu aliripotiwa na Ofisi yake kuwa alikutana na Wajumbe wa Tume aliyoiteua, bila ya kupata hakika ya kila mteuliwa --iwe ni kwa njia ya kumpigia simu kuthibitisha, kutuma ujumbe mfupi wa simu, kutuma barua, nukushi, barua pepe n.k-- kuwa (1) Amepata taarifa rasmi ya uteuzi huo na (2) Ameridhia uteuzi huo; Waziri Mkuu akaitisha kikao ijapokuwa baadhi ya wajumbe hawakuwemo kikaoni bila ya kuwa na hakika kama wanaopelea wametoa taarifa rasmi ya udhuru wa kutokuhudhuria kikao hicho, sioni ni kwa namna gani Mbatia analaumiwa kususia Tume il hali anaifuata sheria. Kuongoza ni mfano na Kiongozi ni mfano.
Kwa wasiojali sheria au wanaojiona wapo juu ya sheria ama wenye adabu za woga, hili litakuwa jambo la kipuuzi kwao. Kwao wao amri ya mkubwa inatiiwa bila kuhojiwa hata kama imekiuka sheria, hata kama nchi ni ya utawala wa kiraia na haiendeshwi kijeshi. Kwao kuvunja sheria mama si jambo la ajabu. Ndiyo wale kila leo wanaimba misemo kama kasuku bila kutafsiri wala kujua maana yake. Na hao hawakawii kusema kwa kuwa huyu ni mmoja wa wanachama wa upinzani, basi lolote lile hata liwe jema atapata pa kupinga tu. Na utawasikia majuha hao wakijitapa kwa bezo la kejeli, “sheria Bongo?”
Utakuwa na kasoro ukithubutu kusema Mbatia hana nia ya kusaidia nchi kuondokana na tatizo kwa kuhoji utaratibu uliotumika kumfikishia taarifa. Angekuwa hana nia angetumia miaka inayokaribia kumi kutafiti kuhusu elimu na kisha kukusanya vielelezo na kuwasilisha hoja Bungeni kuhusu uozo wa elimu? Kama anaweza kuunda hoja yenye nguvu hivyo kwa maslahi binafsi, je atakapounda hoja inayolihusu Taifa?
SOURCE:
WAVUTI