Facebook Comments Box

Tuesday, April 9, 2013

UKUTA WA TBC WABOMOLEWA

Picture
Mkurugenzi wa TBC, Clement Mshana akikagua eneo la ukuta wa Shirika hilo la utangazaji uliobomolewa (picha: Lukwangule)
Ukuta ambao unatenganisha studio za Shirika la Taifa la Utangazaji, TBC, Makao Makuu na barabara ya Nyerere umebomolewa kwenye upande wa barabara ya Mandela inayoelekea Bandarini.

Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana na wafanyakazi wa ofisi hizo wamedai kuwa hawakuwa na taarifa yoyote, wala alama maafufu ya “X” ambayo huwa inaashiria kuwa eneo hilo litabomolewa wakati wowote.

Ukuta huo ulivunjwa mchana wa leo kwa mfululizo kuanzia maeneo ya mataa ya TAZARA.

Mshana alisema kuwa kwa unyeti wa kituo hicho na mali zake za thamani, ambacho pia ni mali ya Wananchi na Serikali, haikupaswa ukuta wake kuvunjwa kiholela na kuacha eneo hilo likiwa wazi.

Watu waliokuwa eneo la jirani walijizolea na kuondoka na nondo zilizotokana na kuvunjwa kwa ukuta huo.


RAIS KIKWETE AISHUKURU MCC YA MAREKANI KWA KUGHARAMIA MIRADI YA GHARAMA KUBWA NCHINI

Picture
Rais Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Millenium Challenge Corporation MCC, Daniel Yohannes, Ikulu jijini Dar es Salaam, Aprili 8, 2013. Kushoto ni Balozi wa Marekani Alfonso E. Lenhardt.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru Marekani na Shirika lake la Misaada la Millenium Challenge Corporation – MCC- kwa msaada wa mabilioni ya fedha ambao umechangia kuboresha miundombinu nchini na kuwaletea wananchi maendeleo.
 
Aidha, Rais Kikwete amelishukuru taifa hilo kubwa na MCC kwa uamuzi wake wa kutoa awamu ya pili ya msaada kama huo kwa Tanzania ambao maandalizi yake yameanza. Rais Kikwete ametoa pongezi hizo leo, Aprili 8, 2013 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa MCC, BwanaDaniel Yoannes Ikulu, mjini Dar es Salaam.
Yoannes yuko nchini kuzindua baadhi ya miradi iliyogharimiwa na msaada wa dola za Marekani milioni 689 ambao Serikali ya Tanzania imeutumia katika kujenga ama kuboresha miundombinu ya barabara, umeme, viwanja vya ndege na maji.

Miongoni mwa miradi ambayo itazinduliwa kwa pamoja na Rais Kikwete na Bwana Yoannes wakati wa ziara yake katika Tanzania ni ujenzi wa barabara ya Tanga-Horohoro kwa kiwango cha lami, njia ya kulaza nyaya za kusafirishia umeme chini ya Bahari ya Hindi kutoka Bara hadi Zanzibar, na njia ya kusafirisha umeme na kuusambaza katika wilaya mbali mbali nchini kutokea Mkoani Dodoma.

Hiyo ni baadhi ya miradi michache kati ya mingi inayogharimiwa na msaada huo ambayo tayari imekamilika tayari kuzinduliwa. Mingine mingi inaendelea kujengwa.
“Msaada wenu umetuwezesha kufanya mambo makubwa kama vile kujenga barabara katika maeneo ambako hakuna mshirika mwingine yoyote wa maendeleo alikuwa tayari kutusaidia, na sisi wenyewe tulikuwa hatujapata uwezo wa kiraslimali wa kujenga barabara hizo,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Baadhi ya barabara hizo ni ule ya Tunduma-Sumbawanga na Namtumbo-Songea. Kuna kiongozi wa nchi moja ambaye nilimpata kumwomba msaada wa kuijenga barabara hii na akasema kuwa ilikuwa vigumu kwa nchi yake kujenga barabara inatoka kusikojulikana kwenda kusikojulikana. Nawashukuru nyie kwa msaada wenu mkubwa.”
MCC ilitangaza kuipa Tanzania msaada huo wa mabilioni ya fedha Desemba 2005.
Picture
On April 8, 2013 President Jakaya Kikwete (third from right) met with the Millennium Challenge Corporation (MCC) CEO Daniel W. Yohannes (third from left) at the State House in Dar es Salaam. President Kikwete and Mr. Yohannes discussed the ongoing partnership between MCC and Tanzania, which was deemed eligible to develop a second compact in December of 2012. Mr Yohannes is currently visiting the country to mark the upcoming completion of MCC’s $698 million compact, which invested in roads, water and energy sectors in both Tanzania mainland and Zanzibar. Others in the picture are Ambassador Alfonso E. Lenhardt (second from right), MCC Managing Director for Public Affairs Nasserie Carew (right), MCC's Resident Country Director Karl Fickenscher (second from left) and U.S Embassy's Political and Economic Affairs Counselor, Elizabeth Pelletreau (left).



YANGA WAKATAA MECHI ZAO KUONESHWA BURE NA SUPER SPORT

Siku moja baada ya shirikisho la soka nchini TFF kubadilisha ratiba ya baadhi ya mechi za ligi kuu ya Tanzania bara ili kuweza kufanikisha mpango wa kuonyesha mechi hizo kupitia kituo cha Supersport, klabu ya Yanga kupitia makamu wake mwenyekiti Clement Sanga imesema haikubaliani na mpango huo kwasababu haujafuata utaratibu na pia utaziingizia hasara kubwa klabu zinazohusika na mpango huo.

Akizungumza na mtandao huu Sanga alisema kwamba mpango huo wa kuonyesha mechi za ligi kuu bure kwenye Supersport haupo katika kuzinufaisha vilabu bali wahusika wengine wa mpango huo.

"Kwanza jambo muhimu kuhusu suala hili kumekuwepo na mfumo m'bovu wa mawasiliano baina ya TFF, Supersport na vilabu vyenyewe kama Yanga. Sisi kwa upande wetu tunaona kabisa huu mpango unatuingizia hasara sana, kwa mfano baada ya kubadilisha ratiba ya mechi zetu tutacheza mechi 3 ndani ya siku 8 wakati ilitakiwa ndani ya wiki tucheze mechi mbili na bado ukumbuke bado tunapaswa kusafiri kwenda Tanga hivyo kuna mambo ya gaharama na vitu vingine vingi tu. Lakini pia mechi ambazo wanataka kuzionyesha bure ni zile ambazo sie vilabu tunazitegemea sana kwenye suala zima la mapato na wao ndio wanataka kuzionyesha bure - na watanzania wengi wanaposikia hivyo mahudhurio uwanjani yanakuwa hafifu hivyo tunakosa mapato. Bora waonyeshaji wa mechi hizo wangekuwa wanatoa fidia kiasi fulani kutokana na matangazo ya kibiashara wanayopata ili kuweza kuzinufaisha klabu zetu, lakini si hivyo wanavyotaka wao. Nadhani kwenye hili TFF wangeliangalia vizuri liweze kutunufaisha sote na sio watu wachache kama ilivyo sasa," Aliongeza Sanga.

Alipoulizwa kama wameshawasilisha msimamo wao kwa uongozi wa TFF na kamati ya ligi Clement Sanga alisema, "Kwanza walipotuletea taarifa kuhusu jambo hilo kwa njia ya barua pepe tuliwajibu na baadae ikaja barua ambayo katibu wetu alijibu kutoa msimamo wetu juu ya suala hili, kinachojitokeza hapa TFF wanatumia mabavu yao kutupeleka peleka, sie tumeshika makali wao mpini. Sie tusipokubali kucheza jumatano kama wanavyotaka wao basi watachukua maamuzi ya kuigawia timu pinzani ushindi, la msingi sie tutakalolifanya hatutokubali mechi zetu zionyeshwe kwenye TV bila kupata fidia ya fedha. Sisi kama Yanga hatupo tayari kuona tunafanyishwa kazi bure. Supersport imeshafanya majaribio sana, sasa haya ya sasa nini? Viongozi wa soka tubadilike tuweke mbele maslahi ya soka letu kabla ya kujiridhisha nafasi zetu, haiwezekani watu wawili watatu waamue tu kwamba mechi kesho hakuna bila kujali hasara zitakazowagharimu wengine. Sie tulishajipanga kwamba Jumatano tunacheza na Oljoro, then tunasafiri kwenda Tanga kucheza na Mgambo then turudi Dar kwa ajili ya mchezo mwingine. Matayarisho ya mechi hizi tulishafanya wiki mbili kabla, tukalipia hotel na gharama nyingine, sasa haiwezekani ghafla kikundi cha watu fulani wenye nguvu za kimaamuzi kutubadilishia ratiba - je zile fedha tulizolipa mahoteli watatulipa akina nani, kwa sababu ni dhahiri unapolipia hotel unapewa na muda wa kuivitumia vyumba vile hivyo muda ule unapoisha fedha yako inakuwa imeenda. Nadhani hili suala linahitaji kuangaliwa vizuri, na viongozi wa vilabu tuwe na umoja kuweza kulipigania hili suala dhidi yetu. Tusiwe viongozi wa kuburuzwa ovyo ovyo."

Akizungumzia mahitaji wanayotaka ili wakubali mechi zao ziweze kuonyeshwa kwenye TV, Sanga alisema kwamba hicho kituo cha TV kinachotaka kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mechi zao inabidi walete ofa ya kueleweka ambayo itaweza kufidia hasara ya kwenye mapato na gharama nyingine ambazo timu wataziingia ili kuweza kwenda sawa na ratiba zao. Pia akataka uwepo uwazi wa makubaliano yote ya kimsingi ili kuepusha migogoro ya namna hii.


MH ZITTO KABWE AONESHA JINSI MAKAMPUNI YA SIMU YANAVYO IIBIA TANZANIA




HILI NDIO GAZETI LILILO RIPOTI SKENDO YA PENGO YA KUUZA UNGA




ANGALIA LIVE JINSI UHURU KENYATA ANAVYO APISHWA LEO




TAKUKURU YAWAACHIA HURU WACHEZAJI WANNE WA AZAM BAADA YA KUSHINDWA KUTHIBITISHA TUHUMA YA RUSHWA DHIDI YAO



TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliyokuwa ikifanya uchunguzi wake dhidi ya wachezaji wanne wa Azam FC
waliotuhumiwa kupokea rushwa kupanga matokeo, imeshindwa kuthibitisha tuhuma hiyo.
Wachezaji ambao walikumbwa na kashfa hiyo ni kipa Deogratius Mushi 'Dida' na mabeki Erasto Nyoni, Said Morad na Aggrey Morris ambao wapo huru baada ya uchunguzi kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo. 

Kosa la kupokea rushwa ni kinyume na Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.
Kwa mujibu wa kifungu hicho ni kosa kwa mtu yoyote kuomba, kupokea, kushawishi au kulazamisha kupewa rushwa au kuahidi kutoa rushwa. 

Afisa Uhusiano wa TAKUKURU, Doreen Kapwani alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa Wachezaji hao walituhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kupanga matokeo ya mechi kati ya Azam FC na Simba SC iliyochezwa Oktoba 27, mwaka jana Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Simba ilishinda mabao 3-1.

"Tuhuma hizo ziliwasilishwa TAKUKURU Mkoa wa Temeke Novemba 9, mwaka jana na Azam ikiwatuhumu wachezaji hao kupokea kiasi cha Sh7 milion kutoka kwa uongozi wa Simba wagawane na kupanga matokeo ya mechi hiyo."


BAADA YA KUIPA STARZ USHINDI WA BAO 3 KWA 1 DHIDI YA MOROCO SAMATA ATEGEMEWA KUIUA BOTSWANA JUMAPILI



TP Mazembe watawakaribisha Mochudi Centre Chiefs jijini Lubumbashi Jumapili huku macho yote yakiwa kwa mshambuliaji Mbwana Samata kuwavusha kuingia raundi ya pili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
Samata amereja Mazembe akiwa na ari kubwa baada ya kufunga mabao mawili kwa Taifa Stars iliyoshinda 3-1 nyumbani dhidi ya Morocco jijini Dar-es-Salaam katika mchezo wa kusaka kufuzu kushiriki Fainali za  Kombe la Dunia 2014.
 
Kiwango chake kimekuwa ni habari njema kwa kocha wa Mazembe, Lamine Ndiaye mwenye matumaini ya kuiongoza timu hiyo ya DR Congo kuibwaga Mochudi katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
Mazembe kwa sasa inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Mochudi ushindi iliyopata katika mchezo wa kwanza uliofanyika Machi 16 jijini Gaborone, ambapo goli hilo pekee lilifungwa na Samata.
 
Pamoja na ukweli kwamba ubora wa Mazembe unamtegemea Samata, kocha wa Mochudi, Madinda Ndlovu bado anaamini kuwa kikosi chake kitafanya maajabu Lubumbashi hapo Jumapili.
 
"Bado hatujakata tamaa pamoja na kuwa tumefunga bao moja nyumbani kwetu,” alisema Ndlovu.
Wakati huo huo; hakuna timu iliyowahi kuifunga Mazembe jijini Lubumbashi kwa zaidi ya miaka kumi sasa katika mashindano haya ya Afrika.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU