Facebook Comments Box

Saturday, August 9, 2014

WABUNGE WA YANGA WALIVYO WANYANYASA WABUNGE WA SIMBA

Kikosi cha Yanga kilichokwaana na Simba na kuibuka na ushindi wa 3-2.

Kikosi cha Simba kilichopigwa 3-2 na Yanga.
Mechi ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 imemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2. 

Wafungaji Simba: Maji Marefu na Yusuf Gogo. 

Yanga: Idrissa Kitwana, Ahmed Ngwali na Mark Tanda.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akishangilia na shabiki wake baada ya ushindi wa Yanga.
Mwigulu Nchemba akiwarushia skafu yake mashabiki wa Yanga.
Ridhiwan Kikwete akishangilia ushindi wa Yanga dhidi ya Simba.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye ni shabiki wa Yanga, Ridhiwan Kikwete akivua jezi yake kwa ajili ya mashabiki mara baada ya ushindi wa timu yake wa mabao 3-2 dhidi ya Simba leo.
Hekaheka wakati wa mtanange huo.
Mashabiki wakifuatilia mtanange huo.
Timu zikiingia uwanjani.
Ridhiwan akiwapa hi mashabiki.
Waamuzi wakiingia uwanjani.

Mwamuzi Othman Kazi akiongea na manahodha wa Yanga na Simba (Wabunge).


RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA WATEMBELEA MAKTABA YA KIRAIS YA RAIS BUSH

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) sehemu ambayo imejengwa kwa mfano wa Ikulu ya Marekani, White House, hususan katika bustani y a Waziri (Rose Garden) pamoja na ofisi ya Rais wa Marekani, Oval office
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush 

 (Bush Presidential Library) sehemu ambayo imejengwa kwa mfano wa Ikulu ya Marekani, White House, hususan katika bustani y a Waziri (Rose Garden) pamoja na ofisi ya Rais wa Marekani, Oval office

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) na kujionea nafasi kubwa iliyotolewa kwa Tanzania na zawadi ambazo Rais Bush alizipata katika ziara yake rasmi ya Tanzania wakati akiwa Rais wa Marekani. Maktaba hiyo ya kuvutia inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa kabisa ya habari na mawasiliano.

Rais Kikwete alikuwa amesimama mjini Dallas kwa muda akiwa njiani kutoka Washington D.C., kwenda Houston, jimbo hilo la Texas kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara wa mafuta na gesi ambao wanataka kuwekeza katika sekta hiyo hapa Tanzania.

Rais Kikwete amekuwa Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tisa, ambako miongoni mwa mambo mengine, amehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani na Afrika uliofikia kilele chake jana kwa kikao kilichoendeshwa na Rais Barack Obama wa Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington D.C.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library)

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea sehemu ya mfano wa ofisi ya kupangia mikakati ya Ikulu ya Marekani iliyotumika na Rais MStaafu George W. Bush kwenye Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library)





BONGO FLEVA WAWANYAYASA BONGO MOVIES

Mchezaji wa Bongo Fleva, Ali Kiba akimtoka msanii wa Bongo Movies, Issa Mussa ‘Cloud 112′.

Mwanamuziki H-Baba akijaribu kuwatoka wachezaji wa Bongo Movies.
Nyomi ndani ya Uwanja wa Taifa ikifuatilia mechi hiyo.
 Kikosi cha Bongo Movies.
Kikosi cha Bongo Fleva.
 Bongo Fleva wakisalimiana na Bongo Movies kabla ya mechi.

 Bongo Movies kabla ya kuanza mtanange dhidi ya Bongo Fleva.

Kikosi cha timu ya Bongo Fleva kimeibuka kidedea katika mtanange wao dhidi ya Bongo Movies kwenye Tamasha la Usiku wa Matumanini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mfungaji wa bao pekee la Bongo Fleva ni mwanamuziki Ali Kiba.


LORI LAPINDUKA KIBAHA





KIBONDE MBARONI

Kibonde akiwa chini ya ulinzi
Na mwandishi wetu mtaani;

Kibonde wa Clouds anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, amemgonga dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walipofika kupima ajali, Kibonde karudi nyuma kaendesha gari lake kasepa! Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia. 

Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge. Trafiki aliingia ktk gari lake nakumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. 

Kibonde kagoma na kumtaka trafiki ashuke ktk gari lake, trafiki naye kagoma kushuka. Mchezo ulioendelea Kibonde aliondoa gari na kuanza kupiga misele, akizunguka mitaa akiwa na trafiki huyo! Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kila kiunga cha jiji hususani eneo la Mwenge na Ubungo.

kunifuatafuata sio dili achana na mimi
Hayawi, hayawi yakawa, Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo nikashuhudia senema ya Kibonde na trafiki! Trafiki wa kike aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde iliyokuwa kasi, gari hiyo haikuonesha dalili za kupunguza mwendo.

 Trafiki alikomaa kusimama mkono wake ukiwa juu kuashiria kumtaka Kibonde asimame huku akipaza sauti ktk radio call akisema ananigonga, afande, ananigonga! Akiwa ktk hali hiyo, kuna gari ilikotokea sikujua ikakatisha kati ya trafiki na gari ya Kibonde ndiyo ikawa kigingi cha gari ya Kibonde na kutiwa mbaroni! 

Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki ambapo kwa sasa amepelekwa Oystabay! Kwa utafiti wangu kidogo nilioufanya nikifukuzana na muda kuwahi kanisani, ni kwamba Kibonde na watu wengine aliokuwanao ndani ya gari lake walikuwa 'TINGASI'!


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU