Facebook Comments Box

Tuesday, August 12, 2014

MBUNGE WA CHADEMA AELEZA KWANINI KARUDI BUNGENI


Mh Said Arfi
Na Magreth Kinabo Dodoma; 
Mjumbe wa Bunge  Maalum la Katiba Said Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)amezitaja sababu za kurejea katika bunge hilo, kuwa ni hofu ya  Mwenyezi Mungu.

Aidha Arfi ameitaja sababu nyingine ni kwamba amerudi katikaBunge hilo, ili kuhakikisha kwamba anaisadia nchi kupita katika mchakato wa Katiba mpya kwa amani na utulivu kwa kutumia kipaji chake na kuwatumikia Watanzania. Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma na mjumbe huyo, wakati akihojiwa na kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Tanzania(TBC).

Akizungumza katika kipindi hicho, huku akinukuu kitabu cha Nabii Musa, Arfi alisema Mwenyezi Mungu hapendezwi na mtu mwenye jeuri na anayejivuna. “Nimejitathimini na kuona mimi mwenyewe nina nafasi gani… maaskofu, mapadre, wachungaji na masheikh. Viongozi wetu wametusii turudi napata kiburi wapi cha kutokurudi,” alihoji Arfi.

Akirejea katika kitabu cha Qruan anasema Mwenyezi Mungu hapendezwi na mtu mwenye kiburi na anayejivuna. Aliongeza kuwa viongozi hao “ wana nafasi kubwa pia wanaheshima ndio maana nimeweza kurudi,””alisema. Mjumbe huyo alisema sasa ni wakati wa kila mtu kueleza ukweli, kwani amerejea katika Bunge hilo, amepata bahati ya kuchangia katika sura ya nne katika kifungu cha 43na 44 kinachohusu haki za msingi. “Nimepata fursa ya kutoa mapendekezo ya haki za wazee nisingewezakuwasilisha kama ningekuwa nje. Pia haki za wafanyakazi,” alisema.

Akizungumzia kuhusu wajumbe wenzake waliosusia Bunge hilo, aliwataka kutanguliza maslahi ya taifa huku akisisitiza kwamba atajitahidi kuwashawishi wajumbe walioko nje ya Bunge hilo ili waweze kurejea. Arfi aliwahakikishia wananchi kuwa  wanawatengenezea Katiba itakayowasaidia kubadilisha maisha ya watu wote.


MAGAZETI YA LEO: JUMANNE 12/08/2014

   
 



DEREVA WA BASI LA YANGA AFARIKI DUNIA


 MAULID KIULA

Uongozi wa klabu ya Young Africans unasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Dereva wa Bus Kubwa la Wachezaji (Yutong) Bw Maulid Kiula kilichotokea alfajiri ya leo Ilala jijini Dar es salaam.Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu mtaa wa Chunya karibu na Bungoni Ilala jijini Dar es salaam.

Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi Ameen.


KIBONZO: KABATI LA VIKOMBE LA ARSENAL


Wilshere hana habari anavuta mambo yake tu.

MTOTO WA MWAKA MMOJA ABAKWA ARUSHA


Mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja tunayemtaja kwa jina moja la Devota wa Sokoni One jijini hapa, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kufuatia kubakwa na njemba moja iitwayo Rajabu Mkoba (30), mkazi wa eneo hilo.

Tukio hilo lilitokea Jumapili ya Agosti 3, mwaka huu ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumbaka mtoto huyo kwa saa 9 na alimrejesha nyumbani kwa mama yake usiku wa manane. Akizungumza na paparazi wetu, mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la  Mwitango alisema siku ya tukio, asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga na yeye kwenda kwenye kikundi cha akina mama.

Usiku saa mbili alikwenda kwa jirani yake huyo kumchukua mtoto wake lakini akaambiwa alichukuliwa na Rajabu. “Nilikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, yeye anaishi na wazazi wake. Hata hivyo, sikumkuta mwanangu wala mtuhumiwa, nikarejea nyumbani.

“Lakini kabla sijarudi, nilimwambia mama wa mtuhumiwa kuwa mwanaye kaondoka na mtoto wangu akaniambia  nirudi nyumbani nikaendelee kumtafuta nikimkosa niende kwake ili akajue cha kufanya, aliamua kwenda polisi’’ alisema mwanamke huyo“Ilikuwa saa 9 usiku nikiwa narejea nyumbani kutoka polisi, nilimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa akiwa na mtoto wangu akimrejesha kwangu lakini mtuhumiwa hakuwepo.

“Niliamua kumchunguza vizuri mwanangu ndipo nilipogundua kuwa sehemu zake za siri zimevimba kupita kiasi huku damu zikimtoka.

“Nilikwenda kumweleza mama yake jinsi mwanaye alivyomtenda mtoto wangu na kumwachia mtoto ampeleke hospitali, alinisihi nisitoe taarifa za tukio hilo popote na akaniahidi kunipa shilingi laki moja,” alisema mama huyo.nImeelezwa kuwa mama wa mtuhumiwa baada ya kukabidhiwa mtoto huyo hakumpeleka hospitali badala yake alikuwa akimtibu kwa kutumia miti shamba.Baadhi ya majirani walikerwa na kitendo cha mwanamke huyo ambapo walimvamia na kumtolea maneno makali ya kumtaka alifikishe suala hilo kwenye vyombo vya sheria.

Kufuatia kelele za majirani ndipo alipokubali kurudi Kituo cha Polisi cha Unga Ltd ambapo polisi walifika nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na kumchukua mtoto huyo kisha kumwandikia hati ya matibabu (PF3) na kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Mount Meru ambako anatibiwa.

Polisi hao walifungua jalada la mashtaka la kubaka na kunajisi lenye namba Ung/RB/2473/2014, bado mtuhumiwa hajakamatwa kwani alikimbia baada ya tukio hilo lakini mama yake ameshikiliwa
kwa mahojiano Devota wa Sokoni One jijini Arusha akiwa na mama yake.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU