Facebook Comments Box

Sunday, October 26, 2014

SIMBA YAWASIMAMISHA KIEMBA,KISIGA NA CHANONGO

AMRI KIEMBA
Klabu ya Simba SC imewasimamisha wachezaji wake watatu kutokana na kile ninachodhaniwa wachezaji hao kuwa sehemu ya klabu hiyo kufanya vibaya, wachezaji waliosimamishwa ni viungo Amri Kiemba,Shabani Kisiga na Haruna Chanongo,hapo jana jijini Mbeya Simba ililazimishwa sare ya tano msimu huu na Prisons.
Shabaan Kisiga

Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya klabu hiyo kinasema pia benchi la ufundi limepewa changamoto ya kuakikisha timu hiyo inakusanya pointi tisa  kutoka kwenye michezo mitatu inafuata kama ikishindikana basi benchi Zima la ufundi nalo litapigwa chini.

Habari zaidi zikisema kuwa mshambuliaji wa kigeni Hamis Tambwe akipewa onyo kwa kuhusishwa na Simba ukawa huku Ramadhan Singano nae akipewa onyo kali pia.

 Kocha msaidizi Matola na mtoa tiba kwa vitendo Bwana Gembe wamesimamishwa kwa muda usio julikana.


PICHA: MAADHIMISHO YA GROUP LA KANDADA: TEAM ISMAIL YAFUNGWA NA TEAM DIZO MOJA

Katika maadhimisho ya Group la kandanda la Facebook kutimiza miaka minne. Ilifanyika mechi kati ya Team Ismail na Timu Dizo moja. Team Dizo iliibuka na ushindi wa magoli manne kwa moja. Team zote zilionesha soka safi na la kupendeza.

chini ni picha za bonanza hilo.

mtanange ukiendelea

Kipindi cha Pili Nassoro Binslum akiwa tayari kuanza kazi


wakati wa zawadi







wakishangilia ushindi wa taem Dizzo one





keki na kombe

mameneja wa timu mbili wakipongezana


mfungaji wa mabao matatu "hat trick" akipewa zawadi ya mpira

keki ikikatwa


Patrick Dumulinyi muanzilishi wa group la kandanda akilishwa keki



STAND UNITED WAKIINGIA UWANJANI NA TINGATINGA WAKIWA NA MBUNGE WAO

Hii ndio njia ambayo stand united waliitumia kuingia uwanjani. Mwenye shati la kitenge ni mbunge wa shinyanga mjini ambae pia ni Naibu waziri mh Masele. 

Hii inatakiwa kukemewa ni hatari.





 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU