Facebook Comments Box

Saturday, August 23, 2014

KIBONZO: ISRAEL NA UMOJA WA MATAIFA DHIDI YA PALESTINA




SAMAHANI KWA PICHA: WEZI WACHOMWA TABATA LIWITI

Chini ni picha ya mmoja ya wezi ambao hufanya wizi kwa kutumia pikipiki. Inasemekana vijana hao wawili walikuwa kwenye pikipiki maarufu kama bodaboda walimnyang'anya mkoba binti mmoja leo alfajiri.
Watu walijitokeza na kuwakamata baada ya hapo waliwakata mikono na kuwachoma moto.
 Polisi walifika eneo la tukio na kuchukua miili ya watu hao.
 Tumeweka picha chache  kwa tahadhari nyingine zipo katika hali mbaya kiasi ambacho hatuwezi kuziweka hapa.

Miili ya wezi hao ikiteketea kwa moto
Polisi wakiwa wamefika kuchukua miili



VIFAA MAALUM VYA KUGUNDUA EBOLA VYAINGIA NCHINI: KUTUMIKA VIWANJA VYA NDEGE

Picha inayoonyesha moja ya kifaa (kamera) nne
zilizoagizwa na Serikali kupimia dalili za ugonjwa wa Ebola maeneo ya viwanja vya ndege. Kifaa hicho kina uwezo wa kutunza picha na kumbukumbu za msafiri, muda , joto la
msafiri, tarehe aliyoingia nchini pia uwezo wa kupata takwimu kutoka kwenye hali ya majimaji au jasho la Binadamu pindi kinapoelekezwa kwake.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Steven Kebwe akiongea na waandishi wa habari eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kupokea na kukabidhi vifaa vya kupima dalili za ugonjwa wa Ebola. Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Dharula
na Maafa (kulia) na Kaimu Mkurugezi wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifani.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Steven Kebwe
akiangalia kwa karibu taarifa zilizorekodiwa na moja ya kifaa (kamera) nne zilizoagizwa na Serikali kupimia dalili za ugonjwa wa Ebola maeneo ya viwanja vya ndege.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
========= ======= ========
Sehemu ya vifaa vya kubaini hatua za awali za ugonjwa wa Ebola kwa kupima hali ya joto la mwili kwa wasafiri kutoka nje nchi wanaotumia viwanja vya ndege vilivyokuwa vimeagizwa na Serikali vimewasili jijini Dar es salaam.
Vifaa hivyo vinavyohusisha kamera 4 zenye uwezo wa kubaini joto la mwili wa msafiri kwa umbali wa mita 100 bila kumgusa muhusika vimewasili leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar
es salaam kutoka nchini Afrika ya Kusini vilikonunuliwa.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe amesema kuwa kuwasili kwa vifaa hivyo ni moja ya juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa kuuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.

Amesema vifaa hivyo vitapelekwa katika maeneo ya viwanja vya ndege na maeneo yanayotumiwa na raia wa kigeni kuingia nchini vikiwemo vya Dar es salaam, Zanzibar, Kilimanjaro,Mbeya na Mwanza. Ameongeza kuwa Serikali inaendelea na mpango wa kuagiza vifaa zaidi vya kuwezesha shughuli ya upimaji wa afya kwa wasafiri wanaotembea (scanners) zitakazowezesha kubaini afya za wasafiri wengi zaidi kwa wakati mmoja bila kulazimu kuwasimamisha.
Aidha, amewataka wataalam hao wa afya kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa kwa kuhakikisha wanawapima abiria wote wanaotoka nje ya nchi bila kujali hadhi walizonazo ili kuweza kubaini kama wana maabukizi au dalili za ugonjwa wa Ebola.

“Nataka mfanye kazi yenu kwa kuzingatia weledi wa taaluma yenu na kwa kuzingatia yale mliyojifunza,mvitumie vifaa hivyo kupima kila abiria ili kubaini joto lake bila kujali cheo wala hadhi yake maana janga hili ni kubwa” Amesema Dkt. Kebwe.
Kuhusu utunzaji wa vifaa hivyo amewataka wataalam hao kuhakikisha wanavitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu na kutimiza malengo yaliyokusudiwa ya kuwasaidia wananchi kutokana na vifaa hivyo kugharimu fedha nyingi kila kimoja.

Katika hatua nyingine Mh. Kebwe amefafanua kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaendelea na shughuli ya utoaji wa Elimu ya Afya kuhusu ugonjwa wa Ebaola ili kuwawezesha wananchi kuchukua tahadhari na kuzielewa
dalili za ugonjwa huo na namna ya kujingika endapo utagundulika nchini.
Amesema tayari kamati mbalimbali za wataalam
zimeshaundwa ili kuwezesha zoezi la utoaji wa elimu na mafunzo kwa wataalam wa ndani ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na janga hilo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), Cosmas Mwaifwani ambaye ofisi yake imehusika katika uagizaji wa vifaa hivyo nchini Afrika ya Kusini amesema kuwa mahitaji ya vifaa hivyo kwa sasa yameongezeka kutokana na umuhimu wake na jinsi vinavyofanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Amesema upimaji kwa kutumia vifaa hivyo unatumia teknolojia ya kubaini mionzi ya joto kutoka katika mwili wa binadamu pindi vinapoelekezwa katika maeneo ya macho na masikio ya mwili wa binadamu.

Amefafanua kuwa vifaa hivyo vinauwezo wa kutunza picha na kumbukumbu za msafiri, muda , joto la msafiri na tarehe aliyoingia nchini na kuongeza kuwa vifaa hivyo vina uwezo wa kupata takwimu kutoka kwenye hali ya majimaji
au jasho la Binadamu pindi kinapoelekezwa kwake.

Mwaifwani ameeleza kuwa MSD inaendelea kuimarisha uwezo wake kwa kuongeza vifaa zaidi kutoka Ubelgiji na China na kufafanua kuwa Bohari hiyo imejiandaa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kwa kujenga uwezo wa kuwa na dawa za kutibu hali ya magonjwa yanayoambatana na homa hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Viwanja vya ndege nchini, Moses Malaki akizungumza kwa niaba ya Viwanja vya ndege nchini ameielezea hali hiyo ya upatikanaji wa vifaa katika maeneo hayo kuwa itaongeza ufanisi wa uchunguzi wa afya kwa wasafiri na kuondoa usumbufu kutokana na uwezo wa vifaa hivyo kumpima msafiri akiwa mbali.


MJUMBE: TUPO DODOMA KWA AJILI YA POSHO TU

Rasimu ya Katiba Mpya
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Alli Omari Juma amefuta matumaini ya Watanzania kuhusu kupatikana kwa Katiba mpya, badala yake akabainisha kuwa wajumbe wako Dodoma kwa ajili ya kula posho tu.
“Nawakumbusha watu kufuta matumaini ya kupata Katiba Mpya, kinachojadiliwa hapa ni mambo ya kulazimishana kila upande, sisi wengine tunaona bora ya Ukawa waliotoka nje kuliko mambo ya humu ndani,” alisema Juma na
kuongeza:

“..Hata wale Wapemba waliokwenda Umoja wa Mataifa kudai haki ya kujitenga , naona walikuwa halali kwani hapa bungeni hakuna mwakilishi hata mmoja kutoka huko wakati tunaambiwa kuwa itakuwa Katiba ya wote, ni kudanganyana.”
Mjumbe huyo alisema kuwa Rasimu ya Warioba imetupwa na wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi kiasi cha kuwafanya wengine waone kuwa kinachotengenezwa ni marekebisho ya Katiba ya 1977.

Alisema kuwa suala la akidi pia litakuwa ni moja ya vikwazo vitakavyosababisha kutopatikana kwa Katiba, akitolea mfano kutoka kwenye kamati yake Namba 4.
 
Alisema ndani ya kamati hiyo mambo mengi yanachakachuliwa kwani wajumbe wanaotakiwa kutoka Zanzibar ni 14 lakini waliopo ni 12 tu, ambao baadhi hawakubaliani na mawazo ya CCM lakini wanaambiwa mambo ni mazuri. “Ukawa walitoka kwa uhalali kabisa nami nawaunga mkono, sisi tuliobaki humu ndani tulikuja kwa makusudi ya kuangalia kinachoendelea na sasa tunaona mambo ni ovyo,” alisema.

Kwa upande mwingine alimlaumu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu Samuel Sitta kwamba amekuwa ni kinara wa kuvuruga kanuni kila wakati na kutaka mambo yake mwenyewe. Jumba ambaye ni mtaalamu wa sheria, aliwatupia lawama pia
viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwamba nao wanapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kuwaweka Wazanzibar pamoja ili wajue wanataka nini.

Kwa mujibu wa Juma, kila maeneo wanayojadili wanafanya kazi hiyo kwa kuboresha maslahi ya CCM kwani wanawasaidia kuwaandikia Ilani yao.
Alimtaka rais Jakaya Kikwete kukubaliana na maoni ya watu mbalimbali kwamba bunge la Katiba lisitishwe mara moja kuliko kuendelea kujadili misimamo mikali ya CCM.

Chanzo;Mwananchi


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU