Facebook Comments Box

Wednesday, November 20, 2013

HAYA NDIYO MANENO ALIYOANDIKA KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK MUUWAJI WA JANA DAR


IMG-20131119-00045 
Anaitwa Gabriel Munissi mkazi wa Mwanza ambae Polisi Ilala Dar es salaam ilithibitisha kwamba ndio amehusika kufanya mauaji ya watu wengine wawili kabla ya yeye kujiua huku ikiaminika ni kutokana na wivu wa kimapenzi.

Kama hukuipata hii taarifa ni kwamba: 
Gabriel alikwenda Ilala na kusimama nje ya nyumba moja iliyokuwa na uzio na geti jeusi kusubiria atoke Mwanamke anaetajwa kuwahi kuwa mpenzi wake na kisha baada ya Mwanamke huyo kutoka huku akiendeshwa na mwanaume mmoja kwenye Toyota Surf na kukiwa na abiria wengine wawili kwenye gari. 
 
Gabriel ndio alianza kufyatua risasi hovyo, Shahidi alieshuhudia tukio hili mwanzo mwisho anasema waliamini kabisa kwamba Gabriel hakuwa jambazi kwa jinsi alivyoshambulia na kuendelea kubaki eneo la tukio bila kuwadhuru watu wengine waliokuwemo karibu, vilevile kama angekua jambazi isingekuwa rahisi kwa yeye kujiua.
Shuhuda anasema Gabriel alipiga risasi mpaka zilizokuwa ndani zikaisha ikabidi aongeze nyingine na kuendelea kushambulia huku akiwa hana nia ya kuwaua wale abiria wengine kwenye gari baada ya kuwajeruhi isipokua Mwanaume aliekua anaendesha pamoja na Mwanamke anaetajwa kuwa mpenzi wake ambae alikua amekaa pembeni ya dereva.

Hiki hapa chini ndio kitu cha mwisho alichokiandika Gabriel kwenye ukurasa wake wa facebook kabla ya kutenda unyama alioufanya.

Waliouwawa kwenye tukio hilo wanatajwa na polisi kuwa ni mwanaume aliekuwa anaendesha gari pamoja na mdogo wa Mwanamke anaetajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Gabriel.

Baadhi ya marafiki wa Gabriel Mwanza wanasema Gabriel ni miongoni mwa vijana wa mjini waliokuwa wanaishi vizuri kwa kuendesha magari ya kifahari na kuwa na pesa za kutosha hivyo pesa haikuwa tatizo kwake.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU