Facebook Comments Box

Wednesday, July 31, 2013

BAADA YA KUTEMWA NA KLABU YAKE KASEJA AFANYA MAZUNGUMZO NA FC LUPOPO YA DRC

 

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, (Taifa Stars), Juma Kaseja Juma maarufu kama (Juma K. Juma) amesema kwamba amefanya mazungumzo na wakala wa klabu ya St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini bado hajaingia Mkataba na klabu hiyo ya Lubumbashi.
 
  Kaseja amesema kwamba mtu aliyejitambulisha kwake kama wakala wa Lupopo alimfuata wakafanya mazungumzo na kufikia makubalino juu ya dau la usajili, mshahara na mambo mengine ya msingi.

Hata hivyo, kipa huyo namba moja Tanzania amesema kwamba baada ya mazungumzo hayo na maafikiano, wakala huyo amepeleka majibu Lupopo ambao wakiafiki ndipo masuala ya Mkataba yatafuatia.

“Nimezisikia hizo habari, kwamba mimi tayari ni mchezaji wa Lupopo, hapana, si kweli. Ni kwamba tumefanya mazungumzo tu na wakala wao na tumefikia makubaliano, nasubiri hadi nisaini Mkataba ndipo nitajihesabu tayari ni mchezaji wa Lupopo,”alisema Kaseja.

Pamoja na Simba SC kutomuongezea Mkataba Kaseja, ameendelea kuwa kipa chaguo la kwanza timu ya taifa mbele ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen.
 
Iwapo Kaseja atafanikiwa kuingia Mkataba na Lupopo atakwenda kuwa mpinzani mkuu wa wachezaji wenzake wa Taifa Stars, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea Tout Puissant Mazembe ya Lubumbashi.
 
Kaseja alicheza pamoja na Samatta na kiungo Mganda wa Mazembe, Patrick Ochan katika klabu ya Simba mwaka 2010 kabla ya 2011 wachezaji hao kuuzwa DRC.     
Source:Bin Zubeiry


MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) IMEZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA MATUMIZI MAZURI YA MAWASILIANO

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John S. Nkomo akizungumza mbele ya Wamiliki wa Blogs mbalimbali Tanzania na Waandishi wa habari katika Warsha ya kampeni ya kuzindua matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo.

ProfesaNkomo amesema kuwa kwa sasa kumekuwepo na ongezeko kubwa la matumizi ya intanet kwa Watanzania walio wengi toka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni.

Amesema kuwa wengi wa watumiaji wa intanet matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, BBM na Blogs zinazotoa habari mbalimbali kama vile habari za maendeleo, burudani na michezo.

Meneja uhusiano wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Bw Innocent Mungi akiwakaribisha wadau mbalimbali wa habari na mitandao kuhusiana na uzinduzi wa kampeni hiyo.
Wadau wa mawasiliano ya kijamii, Blogs wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Mamlaka ya Mawasiliano katika uzinduzi wa matumizi mazuri ya mitandao kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo ya Taifa kwa ujumla ambapo Mstari wa pili kulia mtu wa pili nyuma ni Muwakilishi wa kitongoni Blog Bw. Juma Kabange.
Wawakilishi wa TBC Bw. Elisha Elia na Bi. Daula Abdul
John Bukuku kutoka Full Shangwe Blog
Prof. John Nkomo akiwa na Mrisho Mpoto ambae ameimba wimbo maalum wa kampeni hiyo unaoitwa 'Delete Futa Kabisa' ukiashiria kufuta kabisa ujumbe mbaya utakaoupata katika simu yako au kwenye mtandao wako kabla hauja usambaza kwa wengine wengi.











JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhfKhIZuVa-nyuNh8KCKIUzrysQRxIceLLTs1qM7cj2O5-yWGphgpY2g1BzmFgFW1Cq4Y5O-J1D3xIk0ckg7VcUXIyEUb3S-qKf4YALtgq4O4gFXns4pRd5bLxckQtXczoDRxpotjUu9e8/s1600/TCRA_logo4.jpg

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
Taarifa kwa VYOMBO VYA HABARI

KAMPENI YA KUHAMASISHA MATUMIZI MAZURI YA MAWASILIANO

Siku za hivi karibuni, ongezeko la huduma za mawasiliano nchini limekuwa kwa kasi sana. Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi kifupi zimekuwa sana na kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Kutoka laini za simu za mkononi  milioni tatu tu mwaka 2000 hadi kufikia laini 28,000,000.  

Watanzania walio wengi hivi sasa wanafaidika kwa huduma za mawasiliano, yakiwemo mawasiliano ya simu za mikononi, utangazaji. Vile vile huduma za ziada kama kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao na simu za mkononi zimeongezeka maradufu. Wananchi wengi wanapata huduma za kibenki kwa kutumia simu zao, wanawasiliana kwa kutumia simu zao kupitia sauti, SMS na kadhalika.

Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la matumizi ya intaneti kwa watanzania walio wengi kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni. Wengi wa watumiaji wa intaneti matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, BBM, LinkedIn na blog mbalimbali zinazotoa habari mbalimbali zikiwemo za kimaendeleo, burudani pamoja na michezo.

Matumizi haya ya intaneti yamewanufaisha watanzaia walio wengi kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani miongoni mwa watanzania.

Hata hivyo pamoja na maendeleo haya, kumekuwepo na baadhi ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo vurugu, kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla.

Leo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inazindua kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya mawasiliano na inawatahadharisha wananchi kwamba kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 ni makosa. Katika kampeni hii, Mamlaka inakusudia kuwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri ili kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwa watanzania.

Katika uzinduzi huu, Mamlaka imewaalika baadhi ya watumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania walio wengi wanafaidika na mawasiliano. Miongoni mwao wako wamiliki wa blog mbalimbali, wasimamizi wa makundi mbalimbali katika mtandao wa FB na mengineyo. Nia ya Mamlaka ni kuomba ushirikiano kwao ili waweze kushiriki katika kampeni hii na kuwahamasisha mashabiki wao kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili kunufaisha Taifa letu kwa matumizi mazuri.

Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wote wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya Mawasiliano inaendelea kuchangia uchumi wa Taifa na kuiweka Tanzania katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.


Imetolewa na:

 MKURUGENZI MKUU
Mamlaka ya mawasiliano TaNzania

31 Julai 2013












MATAWI YA YANGA YAUNGA MKONO UONGOZI KUIKATAA AZAM TV


Bakili Makele (kulia) akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya viongozi wa matawi, Moses Katabaro(katikati) na Lawrence Mwalusako (kushoto) 























Uongozi wa matawi wa klabu ya Yanga (wenyeviti na makatibu) leo umefanya kikao katika makao makuu ya klabu mtaa wa twiga/jangwani kisha kutoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuhusiana na tamko la uongozi (kamati ya utendaji) kutokubali kuonyeshwa kwa michezo yake kwenye luninga.
Awali klabu ya Yanga juzi kupitia kamati ya utendaji ilifanya mkutano na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa klabu kuhusiana na kutoridhishwa na kamati ya muda ya Ligi (TPL) kuingia makubaliano ya kurushwa matangazo ya televsheni kwenye michezo yake.
Akiongea na waandishi wa habari leo katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako alisema baada ya kukaa na viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga jijni Dar es salaam kwa pamoja wamekubali na kuunga mkono hoja zilizowasilisha na viongozi juu ya haki ya matangazo.
Mmoja wa viongozi wa matawi Bakili Makele akiongea kwa niaba ya viongozi wa matawi, alisema TFF inaamua kukandamiza soka la Tanzania kwa kuviamulia maamuzi yake juu ya kuonyeshwa kwa michezo ya timu kwenye luninga.
Makele amesema taratibu za kuipa kampuni ya Azam TV tenda ya kuonyesha michezo ya Ligi Kuu haikua na usawa, kampuni hiyo bado haijaanza hata matangazo, haijulikani ofisi zake zilipo, uwezo wa kurusha matangazo haujulikani kwa watanzania lakini bado wamepewa nafasi hyo.
Kikubwa tunamuomba rais wa TFF Leodgar Tenga kulitazama suala hili kwa umakini, kwani mtazamo wetu viongozi wa kamati ya Ligi wametazama maslahi yao binafsi bila kuzingatia uwezo wa timu na maliasili watu (wapenzi,washabiki).
Huwezi kuipa mgawo sawa timu ya Yanga na timu nyingine ambazo katika mechi zao binafsi wanatapata washabiki 50 kwenye mchezo, wakati Yanga imeongoza kwa mapato katika msimu mzima wa Ligi Kuu ya Vodacom na wastani wa washabiki 8,000 kwa kila mchezo.
Mwisho Makele amesema wanauamini uongozi uliopo na wapo nao bega kwa bega, tunaomba jamii nzima itambue kuwa Yanga inapigania haki zake na hao wote wanaobeza msimamo wetu basi wajibu hoja kwa hoja na sio kuongea tu pasipo kujibu hoja. 

SOURSE:YANGA


KIBONZO: KUWAFUNDISHA WATOTO MAMBO YA DINI NI MUHIMU

www.kitongoni.blogspot.com



NASHEED: MAHER ZAIN - YA NABI SALAM ALAYKA (VOCAL ONLY)




MAWAIDHA: SHEIKH NAASOR BACHU - MAMBO YASIYOBATILISHA SWAUM




VIDEO: SAMSUNG S4 ACTIVE HAINGII MAJI WALA VUMBI





 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU