Facebook Comments Box

Friday, March 29, 2013

DIAMOND NA WEMA WATAMBIANA KATIKA PESA

Wakati WEMA ISACK SEPETU akifungua bonge la ofisi ya kuzalisha filamu, aliyekuwa Mpenzi wake Nasibu Abdul 'DIAMOND PLATNUM' amemjibu kwa kukamilisha mjengo wa maana uliomgharimu takriban Shilingi za Kitanzania Milioni 260 hivyo kwa pamoja kuonesha jeuri ya pesa walizo nazo.

WEMA alifanya uzinduzi wa ofisi yake hiyo bila kumpa taarifa Mama yake mzazi MARIAM SEPETU ili iwe bonge la Surprise kwake pamoja na watu mbalimbali kama vile Diamond Platnumz mwenyewe siku ya Jumatano iliyopita, Jina la Ofisi hiyo ni ENDLESS FAME FILMS iliyopo Mwananyamala- Komakoma Jijini Dar es Salaam.

Wema akiwa katika Ofisi yake hiyo Mpya ya Filamu
Wema akiwa Nyumbani kwake.
Wema akitoka kwake na gari yake aina ya Audi Q7.

Pamoja na Diamond kutoalikwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Ofisi hiyo ya Wema lakini chanzo cha habari kinasema alikuwa katika harakati za kumalizia Mjengo wake ulioko Tegeta ili nae afanye uzinduzi rasmi. Akizungumza na kitongoni blog akiwa kwenye eneo ilipo nyumba hiyo ambayo ilikuwa ikifanyiwa ‘finishing’, Diamond alisema kuwa nyumba hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 260 ni zawadi kwa mama yake SANURA KASSIM ‘SANDRA’.

“Mama yangu ndiyo kila kitu kwangu, mara ya kwanza nilimnunulia gari aina ya Toyota Alteeza nikaona haitoshi, nikaamua kumjengea hii nyumba ambayo itakuwa kama urithi wake hata nikifa leo,” alisema Diamond.

Diamond alimzungusha paparazi wetu na kujionea mjengo huo wenye vyumba vinne vya kulala ambavyo vyote ni ‘self contained’ (chumba chenye choo na bafu), studio kubwa ya kurekodi muziki, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kujenga bwawa la kuogelea ‘swimming pool’, uwanja wa basketball na sehemu maalum ya kufanyia mazoezi (gym) ambapo alisema hadi ifikapo Septemba, mwaka huu kila kitu kitakuwa kimekamilika.
Hii ndiyo Nyumba ya Diamond anayojenga huko Tegeta na gari linalo onekana hapa ndilo gari lake anlotumia ukiachilia mbali Altezza aliyo mnunulia Mama yake.Ukiachana na ukubwa wa nyumba hiyo, uwanja ambao ameuzungushia uzio wa ukuta kuna nyumba nyingine ndogondogo tatu ambazo kwa mujibu wa staa huyo zitakuwa zikipangishwa.
Diamond akiwa Nyumbani kwake Sinza Mori anapoishi sasahivi.







MHANDISI MKUU NA MHANDISI WA WILAYA YA ILALA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUTOKANA NA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA 16


 Bango linaloonesha Ujenzi wa Ghorofa lililoporomoka leo Jijini Dar es Salaam, Jengo ambalo Mhandisi Mkuu na Mhandisi wa Wilaya ya Ilala wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa Uchunguzi zaidi.
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akipatiwa Maelezo na Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Dar es Salaam Suleiman Kova wakati alipofika eneo la tukio ambapo Jengo la ghorofa 16 liliporomoka leo katika makutano ya Mitaa ya INDIRA GANDHI na ASIA.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia kwa pamoja MHANDISI MKUU WA JENGO na MHANDISI WA WILAYA YA ILALA kutokana na kuporomoka kwa Jengo la ghorofa 16 leo asubuhi Jijini Dar es Salaam.

Kwani Mhandisi wa Wilaya ya Ilala ndiye aliyetoa kibali cha kujengwa jengo hilo na Mhandisi Mkuu kuwa yeye ndiye msimamizi mkuu wa Ujenzi katika jengo hilo. Lakini pia MKUU WA MKOA wa Dar es Salaam amesitisha ujenzi wa jengo lingine lililopo pembezoni mwa Jengo lililoporomoka ambalo pia linasimamiwa na Mhandisi huyo huyo anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi.

Kwa Habari zaidi juu ya Tukio hilo endelea kufuatilia kwa karibu kitongoni blog


POLISI ZANZIBAR: MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA PADRI MUSHI AKAMATWA

Picture 
SOURCE:WAVUTI

BREAKING NEWS: JENGO LA GHOROFA 16 LAPOROMOKA KATIKATI YA JIJI LEO HII


Taarifa iliyotufikia hivi punde inasema:
Jengo la ghorofa 16 limeporomoka asubuhi ya leo katikati ya Jiji la Dar es Salaam katika mtaa wa INDIRA GHAND karibu kabisa na Msikiti wa SHIA na Kuua watu watatu(3) na Kujeruhi kadhaa, ila inasemekana idadi ya watu wanao kadiriwa kuwa wamefunikwa na kifusi ni 60 lakini 17 kati yao tayari wameokolewa na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda KOVA amesema Uokoaji unaendelea japo vifaa muhimu vya kuokolea bado havipo lakini wataalamu mbali mbali kutoka Manispaa wapo pale kuhakikisha hali inafanikiwa na kuwaokoa watu zaidi walioko ndani.


 Mtoto Maisamali Kareem (6) ambaye ameokolewa kutoka katika madrasa ya Msikiti wa Shia ulioangukiwa na Jengo hilo
 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda Suleiman Kova na Kulia kwake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Marietha Minangi.

 Kamanda Kova akizungumza na James Mbatia (Mbunge, Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi)


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU