Tuesday, January 29, 2013
MAFURIKO YALETA BALAA MORO JIONI YA LEO
Mvua
kubwa iliyonyesha morogoro jioni ya leo imesababisha mafuriko katika
mtaa wa morogoro.Mvua hiyo iliyoanza kunyesha kuanzia saa tisa alasiri
imenyesha takribani kwa masaaa mawili imesababisha mafuriko katika
barabara ya msamvu kuingia katikati ya mji hali iliyosababisha msongamano
mkubwa wa magari.
Maji yakiwa yamejaa eneo la mtawala baada ya mvua kubwa kunyesha jioni hii mkoani morogoro
Mafuriko
hayo yaliingia katika makazi ya watu na hapa ni mashine za kukoboa
mpunga wakiwa wamesimamisha kazi zao baada ya maji kuingia ndani.
WAZIRI MKUU AENDESHA KIKAO CHA KUTAFUTA SULUHU MTWARA
Waziri
Mkuu Mhe. Mizengo Pinda yupo Mkoani Mtwara akikutana na makundi ya wadau
mbalimbali wa mkoa huo ili kusikia kutoka kwao mawazo, michango na
dukuduku zao kuhusu mradi wa gesi asilia.
Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake...
Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake...
Taarifa
mpya zitawekwa hapa punde zitakazopatikana. Kwa sasa, tafadhali sikiliza
rekodi ya kipindi cha Amka na PRIDE FM radio, kilichozungumzia
muhtasari wa yaliyojiri katika kikao cha jana kati ya Waziri Mkuu na
Wadau.
TAARIFA MPYA ZA ZIARA YA WAZIRI MKUU
Waziri
Mkuu alikuwa akutane na Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana na
kikao kirefu cha madiwani wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara
vijijini pamoja na kikao cha wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya
Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho.
Dondoo muhimu:
Dondoo muhimu:
- Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba la gesi lisiende Dar
- Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka Waziri Mkuu aondoke naye
- Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa kauli moja Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka kutoa kauli za uongo kuhusu Mtwara Vijijini kuunga mkono suala la gesi iende Dar madiwani waMtwara vijijini. Wamesema hawakushirikishwa.
- Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya
- Waziri Mkuu ametumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi Wadau kuwa bomba liende Dar
- Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu
- Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na UwT (Usalama wa Taifa)
- Hawa Ghasia arudishwa Uwanja wa Ndege, JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya hewa
- Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema wao ndio chanzo cha vurugu
Subscribe to:
Posts (Atom)