Facebook Comments Box

Tuesday, June 25, 2013

HUYU NDIO MTANZANIA TAJIRI WA KWANZA KUTAMBULISHWA NA FORBES AFRICA

Picture
Mo mjasirimali kijana mwenye mafanikio ya kipekee katika bara la Afrika.
Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.

Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa Jarida hilo la Forbes African Magazine linasema amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.

Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika.

Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

“Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni 50 za kimarekani hadi dola Billioni 2.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.


TUME YA UCHAGUZI YA AHIRISHA TENA UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA

Tume ya Uchaguzi ya Taifa imetangaza kuahirisha uchaguzi mdogo wa Madiwani uliokuwa ufanyike tarehe 30.06.2013 katika Kata nne -Elerai, Themi, Kaloleni, Kimandolu- za halmashauri ya Manispaa ya Arusha.

Mwenyekiti wa tume hiyo amesema badala yake uchaguzi huo utafanyika tarehe 14 Julai 2013.

Amesema sababu kubwa ya kuahirisha tena uchaguzi huo ni kutokana na kuendelea kutokuwepo kwa viashiria vizuri vya hali ya amani inayoruhusu uchaguzi huo kuendeshwa.

Uchaguzi huo awali ulipangwa ufanyike Jumapili ya terehe 16 Juni 2013, lakini uliahirishwa baada ya kutokea shambulio na mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni za CHADEMA, siku ya Jumamosi ya tarehe 15 Juni 2013, shambulio ambalo lilisababisha vifo vya watu wawili papo hapo na wengine wawili siku chache baadaye.



AFYA YA MANDELA YAZIDI KUWA MBAYA: SASA AMEKATA KAULI


HALI ya taharuki imetanda katika mitaa mbalimali nchini Afrika Kusini kufuatia hali ya Rais wa kwanza mweusi nchini humo, Nelson Madiba Mandela (94) kuwa mbaya na kukata kauli.Taharuki hiyo imetokea baada ya Ikulu ya Afrika Kusini kutangaza kwamba afya ya kiongozi huyo ni mbaya kuliko siku mbili zilizopita,huku taarifa za ndani ya Serikali ya Afrika Kusini zikidai kwamba Madiba hajafungua macho wala kuzungumza chochote kwa wiki moja sasa.Hata hivyo taarifa hiyo ilithibitishwa jana na Rais Jacob Zuma ambaye kwa mara ya kwanza alikiri hadharani kwamba hali ya afya ya Mandela ni mbaya na madaktari wanaendelea na juhudi za kuokoa maisha yake.Zuma ambaye pia ni Rais wa Chama cha African National Congress (ANC), alikiri kufadhaishwa na hali ya kiongozi huyo wa zamani, alipomtembelea katika Hospitali ya Magonjwa ya Moyo ya Medi-Clinic mjini Pretoria na kuzungumza na mkewe, Graca Machel kuhusu hali yake.Hata hivyo Afisa mmoja kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania ameidokeza Habarimpya.com kwamba Serikali ya nchi hiyo ina wakati mgumu huku kila idara ikitakiwa kuwa tayari kwa lolote na kwamba mara watakaposikia taarifa za kifo cha mwasisi wa taifa hilo waanze kufanya maandalizi ya haraka ya kupokea msiba huo mzito.Mbali na hilo Henry Masanja ni mtanzania anayeishi nchini Afrika Kusini akizungumza na Habarimpya.com kwa njia ya simu akiwa Pretoria alisema kwamba, Hali si shwari katika miji mbalimbali ya nchi hii"."Wananchi wote wameshakata tamaa ya kupona kwa kiongozi wao, huku wengine wakiamini kwamba pengine ameshafariki dunia kwa sababu yuko kwenye mashine na hawezi kuzungumza chochote kwa siku kadhaa  wala kufungua macho,hivyo Serikali imeamua kutangaza kuwa afya ya Madiba ni mbaya ili wapate muda wa kufanya maadalizi ya kuitaarifu dunia juu ya kifo cha Madiba alisema Masanja.

SOURSE: HABARI MPYA


PEP GUARDIOLA AKITAMBULISHWA RASMI KUWA KOCHA WA BAYERN MUNICH






CARLO ANCELOTTI NDIO KOCHA MPYA WA REAL MADRID: PSG WAMCHUKUA BEKI WA ZAMAN WA MAN U KUWA KOCHA



Hatimaye Real Madrid wamemtangaza kocha Carlo Ancelotti kuwa kocha wao mpya.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na PSG amechukua nafasi iliyoachwa wazi na na Jose Mourinho, ambaye amerudi Stamford Bridge.
Ancelotti, 54, amesaini mkataba wa miaka mitatu kuongoza benchi la ufundi la Santiago Bernabeu 


Wakati akiondoka PSG, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa na beki wa Manchester United Laurent Blanc ameteuliwa kuchukua nafasi ya Ancelotti ndani ya klabu hiyo inayomilikiwa na waarbu matajiri kutoka Qatar.

Blanc tayari ana uzoefu na kazi ya ukocha baada ya kuzifundisha klabu ya Bordeaux na timu ya taifa ya Ufaransa.
 
SOURSE: SHAFFIH DAUDA


HUYU NDIO MCHEZAJI WA KWANZA ALIE NUNULIWA NA MOURINHO

Jose Mourinho amefungua rasmi akaunti ya Chelsea na kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kijerumani ANDRE SCHURRLE - ambaye leo hii amefaulu vipimo vya afya na kujiunga rasmi na Chelsea akitokea Bayern Leverkusen.

Chelsea wamempa mjerumani huyo mkataba wa miaka mitano, na kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Jose Mourinho tangu arejee kutoka Santiago Bernabeu mapema mwezi uliopita.
Schurrle, 22, alisema: “Nina furaha kusajili hapa. Ni heshima kubwa kwangu kuichezea klabu hii, ninaangalia mbele kuitumikia timu hii.”
Schurrle ana uwezo wa kucheza aidha kama winga au mshambuliaji wa kati akiungana na wachezaji wengine kama  Juan Mata, Eden Hazard, Oscar na Kevin De Bruyne katika kugombea nafasi ya kuwemo katika kikosi cha kwanza cha Mourinho. 
Schurrle amepewa jezi namba 14.
ANGALIA MAVITU YAKE KWENYE VIDEO HII HAPA CHINI
 
 
SOURSE: SHAFFIH DAUDA 


SUGU AKAMATWA NA POLISI LEO





MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa dhamana.

Mwandishi wetu akiwa Mjini Dodoma anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika vikao vya Bunge.

Sugu alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhojiwa aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine.

Hata hivyo taarifa za awali za tukio la kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Chama Cha Manedeleo na Demokrasia (Chadema) zinadai kwambwa inatokana na kosa la kutoa maneno ya uchochezi, matusi na dhihaka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU