Facebook Comments Box

Monday, February 11, 2013

PAPA BENEDICT XVI ATANGAZA KUACHIA MADARAKA

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI ametangaza kuachia madaraka ya kuongoza kanisa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, uamuzi ambao ni wa kwanza tangu karne ya 15 kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP. Katika taarifa yake, Papa amesema amefikia uamuzi huo ambapo sasa ana umri wa miaka 85. Msemaji wa Papa, Federico Lombardi amesema kiongozi huyo wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki duniani, ataachia ofisi rasmi tarehe 28 Februari, mwaka huu saa mbili kamili asubuhi. Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya Vatican wanasema safari hii, kuna uwezekano mikoba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI ikarithiwa na Kardinali kutoka Afrika. Kardinali Peter Turkson wa Ghana ametajwa kama mrithi-mtarajiwa wa nafasi hii nyeti ndani ya Kanisa Katoliki, linalokadiriwa kuwa na waumini zaidi ya bilioni moja dunia nzima. Mwingine ni Kardinali Francis Arinze; mzaliwa wa Nigeria ambaye alichukua nafasi ya Benedict XVIkama Kardinali-Askofu wa Velletri-Segni alipoteuliwa kuwa Papa miaka nane iliyopita.

MAPIGANO MAKUBWA GEITA KATI YA WAISLAM NA WAKRISTO


Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kumetokea mapigano makubwa Geita eneo la Buseresere baina ya Waislam na Wakristo chanzo cha mapigano hayo ni wakristo kuanza kuchinja nyama na kuiuza.
Chanzo chetu kinaarifu mpaka sasa msikiti umesha chomwa moto na polisi bado hawajafika kwa kuhofia uchache wao kwa hiyo wameagiza polisi kutoka Mkoa wa Mwanza waje kuwasaidia kutuliza ghasia hizo.
Silaha zinazotumika ni silaha za jadi watu wanazunguka mtaani wanakukamata wanakuuliza jina ukitaja jina tofauti na imani yao unapigwa kiasi cha kutosha tu
Kwa mujibu wa Taarifa hizo tayari idadi ya watu 10 wamejeruhiwa kwa kukatwa mapanga ambapo mmoja hali yake inaelezwa kuwa mbaya na amekimbizwa ktika hospitali ya wilaya ya geita,tayari polisi wa kikosi maalum cha kutuliza ghasia FFU kikiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Geita wamewasili eneo la tukio.
Wakristo hao walifanya mkutano wa hadhara jana na kusema kuanzia leo hawatakubali kula nyama  iliyochinjwa na waislam. Na kutenga eneo lao maalumu la kuchinji nyama zao

MKASI: SALAMA NA KING MAJUTO




CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME


 KATIBU WA UHAMASISHAJI WA TAMRA TAIFA BWANA HATIBU MGEJA AKIWA NA MWEKA HAZINA WA TAMRA TAIFA BWANA JUMA KOMBO
TANZANIA MEN’S RIGHTS ASSOCIATION
Equal treatments for all
UTANGULIZI
TAMRA ni Asasi ya kiraia iliyoanzishwa na wanaume wa Tanzania kwa lengo la kutoa msaada wa Kisheria pamoja na Elimu ya Haki na Wajibu katika mahusiano ya kindoa kati ya mwanamke na mwanaume.
Kuanzishwa kwa asasi hii kumekuja katika kipindi hiki baada ya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa wapo wanaume  wengi wanaofanyiwa vitendo vya ukatili katika masuala ya ndoa kwa kunyimwa haki zao za kindoa kutupiwa virago pindi mwanamke anapoamua kumchoka mwanamme kufuatana na kukosa kipato, kupungukiwa nguvu za kiume na mambo kama hayo , jambo ambalo limeonekana kuwa ni chanzo cha migogoro katika ndoa inayosababisha ongezeko la watoto wanaoishi bila wazazi wa pande zote mbili yaani  [ Baba na Mama] huku hali hii ikiigharimu jamii na wanandoa kupigana na kusababisha majeraha na mauaji katika jamii.
Si hivyo tu Mwanamme wa Tanzania amekuwa ni mvumilivu kwa vile amekuwa akitendewa mambo yote haya bila kuwa na chombo cha kukemea vitendo hivi jambo lililotoa ushawishi kwa waanzilishi wa chama hiki kupata uchungu na hatimaye kuamua kuanzisha Asasi hii.
Muda mrefu mwanaume wa Tanzania hakupata wapi  pa kwenda kupata msaada wa kisheria, imefika wakati wanaume kuwa na  chama cha kuwatetea dhidi ya unyanyasaji kutoka kwa wake zao katika nyanja mbali mbali ikiwemo mambo ya ndoa,urithi wa mali kwa wagane, pamoja na ulezi wa watoto.
TAMRA kinaenda mbali katika kuelimisha wanaume juu ya haki zao za msingi pamoja na kuwaelimisha juu ya wajibu wao kama baba katika kuitunza familia yake,kuondoa mfumo dume na mfumo jike, kupiga vita unyanyasaji kwa mke na watoto,urithi wa mali kwa wajane na wagane pamoja na kulea watoto kabla na baada ya kufariki kwa wanandoa.
Jina la asasi: Asasi hii itajulikana kuwa ni Chama cha kutetea haki za wanaume Tanzania/Tanzania Men’s Rights Association kwa kifupi TAMRA
(1) Kuanzishwa kwa TAMRA:
Asasi  ya TAMRA ilianzishwa 01/05/2012
(2) Makao Makuu.
Makao makuu ya TAMRA yatakuwa katika Mtaa wa Mpakani ‘A”Kijito Nyama Jijini Dar Es Salaam kituo cha Afrika sana Nyumba Block namba 45.
                    
vile vile kutakuwa na ofisi ndogo ya Makao Makuu Jijini MWANZA
(3)  Anuani ya Chama ni. Chama Cha Kutetea Haki za Wanaume Tanzania.
    S.L.P 60065
   Dar Es Salaam - Tanzania
    Simu: Mwenyekiti TAMRA TAIFA +255 784 203 556
             Katibu Mkuu TAMRA TAIFA +255 787 565 533
    Blog:   yetu ni  www.tamratanzania.blogspot.com
TAFSIRI
“TAMRA” itamaanisha ni TANZANIA MEN’S RIGHTS ASSOCIATION.
       KUTAKUWA NA VIONGOZI WAFUATAO WA TAMRA
·         Kutakuwa na Mwenyekiti wa TAMRA Taifa.
·         Katibu mkuu wa TAMRA Taifa.
·         Mweka Hazina wa TAMRA Taifa.
·         Katibu wa Uhamasishaji wa TAMRA Taifa.
·         Wajumbe wa Bodi ya TAMRA 
KAZI ZA TAMRA.
TAMRA itakuwa na kazi zifuafuatazo:
(1)  Kutetea wanaume dhidi ya unyanyaswaji katika ndoa.
(2) Kutoa elimu juu haki za Wanamme
(3) Kuwaelimisha wanamme kuondokana na mfumo dume/jike.
(4) Kuelimisha wanaume kuhusu haki na usawa kati ya mwanamme na  mwanamke katika kutoa maamuzi kwa mambo mbalimbali ya kifamilia, kisiasa na kiuchumi.
(5) Umiliki wa mali katika familia.
(6) Haki ya kushiriki na kufurahia ndoa.
(7) Kuelimisha jamii juu ya Haki ya kumiliki mali kwa pamoja kabla na baada ya kifo cha mmoja wa wanandoa.
(8) Kuelimisha wanandoa kuhusu Haki na wajibu wa kuheshimiwa na kupendwa kwa kila  mwanandoa kama ilivyo katika maandiko matakatifu bila kuathiri itikadi za dini.
(9) Kuhakikisha kwamba TAMRA inashirikiana na  taasisi za kutetea haki za wanawake ili kuondoa imani potofu dhidi ya mwanamme ili kujenga mahusiano mazuri katika familia badala ya kuchochea uhasama kwa kumkandamiza mwanamme kuwa ndiyo chanzo cha migogoro ndani ya familia.
10.kuhakikisha kuwa kuna usawa na uhuru wa kujieleza pindi mashauri ya ndoa yanapopelekwa katika vituo vya Polisi kwa uchunguzi na hatimaye hatua ya kupelekwa  katika vyombo vya maamuzi.
11.Kuhakikisha kuwa wapo Mawakili wa kutosha panapotokea mashauri katika Mahakama watakaotetea Haki za Wanaume   ili kuhakikisha Haki inatendeka
MALENGO YA TAMRA.
TAMRA itakuwa na malengo kama ifuatavyo:-
(1)  Kupigania Haki za mwanaume katika masuala mbalimbali ikiwamemo kulinda na kudumisha ndoa.
(2) Kulinda Haki ya mwanaume ngazi ya familia ,kitaifa na kimataifa.
(3) Kuelimisha waathirika wa unyanyasaji
(4) Kutoa msaada wa kisheria Bure kwa kutumia mawakili wa TAMRA.
(5) Kutoa elimu ya Afya na malezi ya mtoto wa kiume ili akue katika maadili yanayozingatia haki sawa kwa wote kuondoa dhana ya mfumo dume.
(6) Kutoa elimu juu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa yasiyokuwa na tiba ikiwamo Ukimwi (HIV/AIDS).
(7) Kutoa elimu na mafunzo kwa wanamme ili kuwafundisha ujasiria mali kuondoa  utegemezi .
(8) Kufanya upatanishi na usuluhishi kwa wanandoa kwa kuzingatia mila,Desturi,Dini pamoja na sheria za Nchi.
(9) Kutoa elimu kwa wanaume kukubali mabadiliko ya mwili kufuatana na umri kuwa mkubwa kati ya mwanamme na mwanamke.
10   Kulinda Haki za kila raia bila kujali itikadi za dini, rangi, kabila jinsia na taifa.
      11  Kutoa Elimu ya uraia.
11    Kushirikiana na serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa katika maadhimisho ya  siku ya mwanamme Duniani ikiwemo kuandaa sherehe  hizo kitaifa kufuatana na kalenda ya kimataifa kila mwaka.
12   Kutoa misaada kwa makundi ya wasiojiweza  yatima, wazee,wagonjwa ,wakimbizi majeruhi wa ajari, majanga kama njaa,mafuriko, shule au kujenga majengo ya kutoa huduma za afya na elimu kulinda na kutunza mazingira kuangalia chaguzi ndani na nje ya Tanzania.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU