Facebook Comments Box

Friday, September 12, 2014

BREAKING NEWS: MSIKITI WA MTAMBANI UNAUNGUA TENA

Taarifa zilizo tufikia ni kuwa msikiti wa mtambani umepata mtihani tena baada ya kuungua moto. Chanzo cha moto huo hakijajulikana. Hamna majeruhi alie ripotiwa. Watu walikuwa wakijiandaa kwa ajili ya swala ya Ijumaa ndio likatokea tatizo hilo
waumini wa kiislam wakifanya juhudi kuudhibiti moto huo.
Baada ya muda wa mwezi mmoja wa tukio la kuungua moto kwa majengo ya shule ya Mivumoni iliyoko katika msikiti wa Mtambani,
Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo kwa mara nyingine moto umezuka katika Ghorofa ya pili
ya jengo hilo.


Moto huo unaelezwa na mashuhuda kuwa ulianza muda wa saa sita na nusu za mchana
kabla ya kusaliwa swala ya ijumaa. Jitihada za
kuzima moto huo zilifanyika na kuzaa matunda.
Hata hivyo moto huo ulioanzia katika darasa lilokuwa linatumiwa na wanafunzi kama chumba
chumba cha dharura tangu tukio la awali,
Gari la Zimamoto lilifika wakati moto ushazimwa

gari la Zimamoto
 
Baada ya kuzimwa kwa moto huo taratibu za swala ya ijumaa ziliendelea kama kawaida.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ila kumetokea sintofahamu kwa waumini wa msikiti
 huo ni nini hasa kilicho sababisha kuzuka tena
kwa moto huo hali ya kuwa jengo hilo limekosa
lhuduma ya umeme tangu kuzuke moto wa awali.

Jengo lililoshika moto leo
Kwa mara ya kwanza moto ulizuka siku ya jumatano jioni ya tarehe 13 Agosti 2014.



MAGAZETI YA LEO: IJUMAA TAREHE 12/09/2014

1_75a23.jpg
2_e5bc2.jpg
3_006a7.jpg
4_3561e.jpg
5_1c0d7.jpg
6_5af4c.jpg
10_d0136.jpg
20_5e9fd.jpg
21_ac5c6.jpg
22_d9f81.jpg
23_db78d.jpg
24_63865.jpg
25_92461.jpg
26_f0984.jpg
27_ed6d1.jpg
28_c2f71.jpg
29_355f0.jpg
30_25300.jpg
31_1f9d1.jpg
32_fbc15.jpg
33_74b56.jpg
40_0612e.jpg
60_7d3ab.jpg
61_963aa.jpg
62_b741f.jpg
63_e6293.jpg
1454873_1465270637079850_2172364455719402651_n_dfdcd.jpg
10178021_1465270673746513_846743157055656123_n_15015.jpg
10603790_1465270947079819_953471165469984265_n_024f0.jpg
10701979_1465270930413154_6564764163349578392_n_60bc2.jpg


HATIMAYE MV KIGAMBONI YARUDI KAZINI BAADA YA KUTOKA MATENGENEZONI

Kivuko hiki kilikuwa kwenye matengenezo baada ya kuharibika na kufanya kuwepo na kivuko kimoja tu ambacho ndicho kikubwa cha Mv Magogoni, siku chache zilizopita Waziri wa Ujenzi Mh. John Pombe Magufuli aliwatembelea Navy kukagua matengenezo ya kivuko hicho na kuwataka wamalize haraka marekebisho hayo ili kuwasaidia wananchi maana wanateseka kwa kusubiri Kivuko kimoja kiende halafu kirudi.

Na Jeshi limetimiza ahadi kwa kukamilisha matengenezo hayo na jana Tarehe 11 septemba 2014, Kivuko hicho kimerudi na kuanza kazi yake rasmi kama kinavyoonekana katika picha ya kwanza na ya pili hapo juu.



PATA KUFAHAMU HALI YA MCHEZAJI WA IVORY COAST BAADA YA VIPIMO

Serge Aurier akiwa chini baada ya kuanguka na kuzimia katika mpambano kati ya Cameroun na Ivory Coast

Mlinzi matata wa Ivory Coast amesema kuwa sawa na madaktari baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.Madaktari walitoa uamuzi wao baada ya Serge Aurier kujeruhiwa na kuzimia kwa muda wakati wa michuano ya kufuzu kwa kombe la taifa bingwa Afrika dhidi ya Cameroon Jumatano. 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, alijeruhiwa baada ya kugongana na kinara wa Cameroon, Stephane Mbia mapema wakati wa kipindi cha pili cha mechi kati ya timu zao.

Ivory Coast ilishindwa na Cameroon kwa mabao 4-1. Aliondolewa uwanjani kwa kitanda na alionekana kujeruhiwa vibaya. Lakini Aurier alipata fahamu na kubaki uwanjani kutizama mechi ilipokuwa ikiendelea.

"Alipokea matibabu akiwa katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde, na msaada huo ndio ulimsaidia kupata fahamu kabla ya kurejea sehemu walipokuwa wachezaji wa akiba. ''


MFUNGWA AKUTWA NA SIMU MWILINI




Kwa baadhi ya watu simu ya mkononi ni kifaa tu cha mawasIliano ilihali kwa wengine ni kifa ambacho kinaweza kukuweka katika hali ya kufa kupona.

Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake. Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini mwake kupitia sehemu yake nyeti ya nyuma.

Mfungwa huyo wa gereza la King'ong'o katika jimbo la Nyeri alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo ambazo alikuwa amezificha mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma.
Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.Wamekuwa kwa miaka mingi wakijaribu kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika magereza nchini Kenya kinyume na sheria za magereza.

Maafisa wa magereza wanakiri kwamba wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.
Chanzo:Bbc


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU