Facebook Comments Box

Thursday, January 31, 2013

WANAFUNZI WAPATAO 1580 KUNUFAIKA NA MPANGO WA UFUNDISHWAJI WA LUGHA YA KINGEREZA KWA NJIA YA TEKNOLOJIA



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapund akitiliana saini na Bi Anne Devilliers,Mratibu wa Mradi wa mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa (Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapunda akibadilishana hati na Bi Anne Devilliers,Mratibu wa Mradi wa mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa (Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.


Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Abdallah Ulega akizungumza machache mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba huo wa miaka mitatu.

WANAFUNZI wapatao 1,580 wanaosoma Shule tisa za Sekondari,wilayani Kilwa, mkoani Lindi,watanufaika na mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknolojia ya kisasa TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya
uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo. Mradi huo wa miaka mitatu,utagharimu jumla ya Sh, ya Sh,144,945,218/-zitakazotumika kujenga misingi bora ya Lugha ya kingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia mwaka 2013. Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Addo Mapunda,alipokuwa akitoa taarifa katika hafla fupi ya kutiliana na saini ya utekelezaji wa mpango huo.

Mapunda alisema mpango huo,utakaochukuwa takribani muda wa kipindi cha miaka mitatu,umeanza rasmi mwezi huu kwa wanafunzi wapatao 1,580 wa kidato cha kwanza kutoka Shule tisa za Sekondari zilizopo katika wilaya hiyo. Amezitaja Sekondari zitakazonufaika na mpango huo kuwa ni,Kilwa day iliyopo mji mdogo wa masoko, Mtanga, Songosongo, Mbuyuni, Kinjumbi,Miteja,Mingumbi,Kikanda na Sekondari ya wasichana ya Ilulu. Mkurugenzi Mapunda alisema mafunzo hayo kwa kuanzia yatakuwa ni ya wiki sita,yameanza rasmi hivi karibuni na kwamba walimu wapatao 30 wakiwemo (12) wa kigeni (Volunteers) wakiwemo na walimu wazawa (18). “Hizi Shule tisa kila moja italazimika kutoa walimu wawiliwatakaopatiwa mafunzo kwa ajili ya kuendesha mpango huu katika Shule zote hizo”Alisema Mapunda. Aidha, Mapunda alisema kupitia ufadhili wa mpango huo wa mafunzo ya kingereza,Halmashauri ya wilaya itaendesha semina/warsha kutoa stadi za kufundishia masomo hayo kwa Sekondari hizo tisa zenye walimu wapatao (71).

Mapunda alisema mafunzo hayo ni nyongeza kwa walimu wote waliopo katika Shule hizo tisa za mafunzo ya kingereza ya aina mbili,TEE-TZ itakayoendeshwa kwa ufadhili wa ubalozi wa Marekani,(RELO-Regional
English Language Office kwa Sh,24,158,480/-.Katika ufadhili wa mafunzo hayo ya TEE-TZ na RELO jumla ya Sh,169,103,698/-ndizo zitakazotumika kwa ajili ya utekelezaji wake. Mratibu wa mradi huo,kutoka kampuni hiyo ya Pan African Energy,Anne Devilliers,amesema lengo la mpango huo ni,kutaka kuwawezesha wanafunzi waelewe masomo yao kwa elimu ya Sekondari na kuongeza viwango vya
ufaulu katika mitihani yao ya kidato cha nne.Devilliers akasema imebainika kwamba wapo wanafunzi waliowengi wamekuwa hawafanyi vizuri katika masomo na mitihani yao,kutokana nakutoielewa vyema Lugha ya Kingereza. Mkuu wa wilaya hiyo ya Kilwa, Abdallah Ulega, ameipongeza kampuni ya
Pan African Energy,na akasema kwamba kwa kiasi furani itasaidiakuboresha kiwango cha elimu ndani ya wilaya hiyo,mkoa na Taifa kwa ujumla. Mpango huo,ulianza kwa majaribio katika wilaya ya Mafia mkoani
Pwani,mwaka 2010 na 2011,baada ya kuona mafanikio yake,ndipo uongoziwa wilaya ya Kilwa,ukaamua mpango huo kupelekwa ndani ya wilaya yao.


 















DKT. ASHA ROSE MIGIRO AWAASA WANANCHI WA BUHIGWE KUWA NA MSHIKAMANO



Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyangamba iliopo kwenye Kijiji cha Janda,Wilayani Buhigwe,Kigoma wakati alipoitembelea shule hiyo na kuangalia maendeleo ya Wanafunzi wa shule hiyo,alipokuwa kwenye ziara ya kukutana na wananchi wa Wilaya hiyo jana.



Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Muhinda kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.Dkt. Asha-Rose Migiro amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa na mshikamano ili kuweja kunyanyua maendeleo ya kijiji na wilaya kwa ujumla.



Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kijiji cha Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.





Viongozi wa kijiji wakitambulishwa.





KOCHA KIM POULSEN ATEUA WACHEZAJI 21 WA KUIVAA CAMEROON



KOCHA WA STARZ KIM POULSEN

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.

“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.

Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).


Wednesday, January 30, 2013

KIWANDA CHA CHEMICOTEX KIMEWAKA MOTO




Kiwanda cha ChemiCotex kilichopo huko Africana njia ya Tegeta jijini Dar es Salaam kimeungua moto jioni ya leo tar 30/01/2013.






IGP MWEMA APATA AJALI MBAYA MOROGORO


                                               IGP SAID MWEMA


Jinamizi la ajali  limeendelea  kuwaandama viongozi  wa  juu  serikali na vyama baada ya  juzi waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kunusurika kifo katika ajali  iliyotokea eneo la Bwawani mkoani Morogoro  ,Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP )  Said Mwema leo amenusurika  kifo  baada ya gari lake alilokuwa akisafiria  kupinduka.
Ajali  hiyo  imetokea  majira ya mchana katika  eneo Mkundi Manispaa ya Morogoro wakati kiongozi huyo akitokea  jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Dodoma.
Hata  hivyo katika ajali  hiyo hakuna madhara makubwa kwa  binadamu zaidi ya gari  kuharibika  kiasi na msafara  wa  IGP kuendelea na safari  ya Dodoma kwa  kutumia usafiri mwingine .


Tuesday, January 29, 2013

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA




MAFURIKO YALETA BALAA MORO JIONI YA LEO


 Mvua kubwa iliyonyesha morogoro jioni ya leo imesababisha mafuriko katika mtaa wa morogoro.Mvua hiyo iliyoanza kunyesha kuanzia saa tisa alasiri imenyesha takribani kwa masaaa mawili imesababisha mafuriko katika barabara ya msamvu kuingia katikati ya mji hali iliyosababisha msongamano mkubwa wa magari.
 Maji yakiwa yamejaa eneo la mtawala baada ya mvua kubwa kunyesha jioni hii mkoani morogoro
 Mafuriko hayo yaliingia katika makazi ya watu na hapa ni mashine za kukoboa mpunga wakiwa wamesimamisha kazi zao baada ya maji kuingia ndani.





VILIO VYATAWALA BAADA YA LULU KUACHIWA LEO KWA DHAMANA


Lulu na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu amechiwa huru na Mahakama leo january 29 2013 mchana, pembeni ni mwigizaji Dr. Cheni ambae amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda mrefu sana.

Ama kwa hakika nnje ya mahaka pamegeuka kilio mara muigizaji elizabeth michael kuachiwa kwa dhamana leo tarehe 29 lulu amepewa dhama kutokana na kesi inayomkabili ya kumuuwa bila kukusudia aliyekuwa star wa bongo movie marehemu steven kanumba.

Mara baada ya lulu kumuona mama yake wamejikuta wakiangua kilio hadi watu wakaribu wakawa wanashangaa.kazi ilikuwa kwa muigizaji dk cheni ambaye kiukweli katika watu wakupongezwa katika hili anachukuwa nafasi ya kwanza kwa binadamu ,cheni amekuwa mstari wa mbele kumsimamia lulu hadi amepata dhamana.
Lulu akiingia kwenye gari huku akisaidiwa na Dk cheni kwa nyuma yake
Mama yake lulu aliwahi kukaririwa akisema kwa sasa anamuona cheni ni zaidi ya binadamu wa kawaida kwani bila yeye hajui kama ataweza kumuokowa mwanae mama huyo amejikuta akilia kwa furaha baada ya kumuona tena mwanae huyo.

Dk chen amezungumza na thesuperstarstz na kutuambia anashukuru mungu kwakumpa moyo wa ujasiri wa kumsaidia binti huyo kwani wengi walimsusa lakini tukumbuke mungu ndiye mlipaji wa yote hatupaswi kumuhukumu mtu kwani hata mahakama bado haijamuhukumu lulu sasa sikuona sababu ya baadhi ya wasanii kujitenga na lulu na ndio maana nikajitolea kumsaidia hadi nijue mwisho wake.
Lulu akilia kwa furaha na kushindwa hata kuongea chochote alipokuwa anahojiwa jambo lililofanya cheni amuongelee
Cheni ambaye ni mmoja kati ya wadhamini waliotoa milioni 20 za kitanzania cheni amekuwa masaada mkubwa sana kwa lulu jambO ambalo limefanya lulu kumuona cheni ni zaidi ya baba yake kwa sasa na ndio maana mara nyingi hata kabla ya tukio la lulu na kanumba kutokea  bado lulu alikuwa anamuita cheni baba japo  haikujulikana kwanini na cheni katika familia ya kina lulu anaheshimika sana na ndio maana haikuwa rahisi kwake kutojitolea kwa hilo.


WAZIRI MKUU AENDESHA KIKAO CHA KUTAFUTA SULUHU MTWARA




Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa na viongozi wa Asasi mbalimbali kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara Januari 27, 2013

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda yupo Mkoani Mtwara akikutana na makundi ya wadau mbalimbali wa mkoa huo ili kusikia kutoka kwao mawazo, michango na dukuduku zao kuhusu mradi wa gesi asilia.

Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake...
 Taarifa mpya zitawekwa hapa punde zitakazopatikana. Kwa sasa, tafadhali sikiliza rekodi ya kipindi cha Amka na PRIDE FM radio, kilichozungumzia muhtasari wa yaliyojiri katika kikao cha jana kati ya Waziri Mkuu na Wadau.

TAARIFA MPYA ZA ZIARA YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu alikuwa akutane na Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana na kikao kirefu cha madiwani wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara vijijini pamoja na kikao cha wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho.

Dondoo muhimu:
  • Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba la gesi lisiende Dar
  • Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka Waziri Mkuu aondoke naye
  • Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa kauli moja  Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka  kutoa kauli za uongo kuhusu Mtwara Vijijini kuunga mkono suala la gesi iende Dar madiwani waMtwara vijijini. Wamesema hawakushirikishwa.
  • Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya
  • Waziri Mkuu ametumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi Wadau kuwa bomba liende Dar
  • Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu
  • Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na UwT (Usalama wa Taifa)
  • Hawa Ghasia arudishwa Uwanja wa Ndege, JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya hewa
  • Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema wao ndio chanzo cha vurugu


Monday, January 28, 2013

YANGA NA PRISON WAINGIZA HELA MARA MBILI YA SIMBA NA LYON

Yanga na Tanzania Prisons zimeingiza mapato ya jumla ya sh. 101,016,000 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara iliyofanyika jana (Januari 28 mwaka huu).
Mechi hiyo namba 94 ilichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Watazamaji 17,946 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Watazamaji 16,158 kati ya hao walikata tiketi za sh. 5,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ni 98 waliokata tiketi za sh. 20,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 24,314,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,409,220.34. Asilimia 15 iliyokwenda kwenye uwanja baada ya kuondoa VAT na gharama za tiketi ni sh. 12,363,433.45.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 7,413,060.07, Kamati ya Ligi sh. 7,418,060.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,709,030.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,884,801.14.


LULU HAJAACHIWA ATARUDI MAHAKAMANI KESHO



Lulu hajaachiwa, atarudishwa mahakamani kesho kwakuwa Msajili wa Mahakama Kuu hakuwepo na hii ilikuwa ni kesi ya 'Kuua bila kukusudia'.

Kesho wadhamini watawasilisha nyaraka zao mbele ya msajili ndipo anaweza kuachiwa.
Baadhi ya masharti aliyopewa Lulu ni pamoja kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani, kuripoti mahakamani na wafadhili kuweka bondi ya Shilingi mil 20


SEKRETARIETI YA CCM YATEMBELEA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA

 Pichani kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya,akipokea  Ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,ulioongozwa na  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana uliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot),kuangalia maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategemewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje.UJumbe huo umewasili mapema jana kutoka jijini Dar kwa njia ya Treni ( reli ya kati),ambako wamekuja kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.

 Sehemu ya kuruka na kutua ndege ikiwa katika hutua ya mwisho mwisho,Kwa mujibu wa Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo ameeleza kuwa unatarajiwa kukamilika mnamo juni mwaka huu,ambapo kwa asilimia 80 maeneo mengi yatakuwa yamekwishakamilika.
 Pichani kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa   Machibya,akimtambulisha  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana kwa baadhi ya wanachama wa CCM waliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot) kuwapokea,ambapo Mh Kinana na ujumbe wake waliwasili mapema jana  jioni kuangalia maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje.
 Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na wananchi wakiwemo wanachama wa CCM,waliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma mapema jana jioni walipokwenda kutazama maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho.
 Mafundi ujenzi wakipaka rangi sehemu ya barabara ya kurukia na kutua ndege mapema jana jioni.
 Ujenzi ukiendelea.


Meneja uwanja wa Kigoma Elipid Tesha,wa pili kuli akifafanua jambo kwa ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM),uliofanya ziara fupi ya kuukagua uwanja huo na kujionea ujenzi wake unavyoendelea kwa kasi,kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh Issa Machibya akishuhudia tukio hilo adhimu, na shoto ni  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM,Martin Shigela,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye, pamoja na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro

Sehemu ya eneo ambalo linaendelea kupanuliwa ikiwa ni sehemu ya ongezeko ya marekebisho ya kiwanja hicho cha Kigoma
Pichani kati Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo akifafanua jambo mbele ya ujumbe wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa.


MWANAUME MPAMBANAJI: GODORO KICHWANI, MTOTO MGONGONI NA BEGI BEGANI


 
KAMERA za blogu asubuhi ya Januari 15, 2013 ilimemnasa mwanaume huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akivuka barabara eneo la Lunna katikati ya mji wa Morogoro huku akiwa amebeba mtoto mgongoni na kichwani akiwa na  godoro ambalo alitoka kulinunua kwenye moja ya maduka yaliopo eneo hilo.

Kuna baadhi ya wanaume wanafikira potofu kwamba jukumu la kulea watoto linawahusu wanawake pekee jambo ambalo sio la kweli, jamaa huyu amedhihirisha kwa vitendo jambo hilo kwa kutembea na mtoto wake mgongoni katikakati ya mji wa Morogoro bila kuwa na wasi wasi wowote na maneno au macho ya watu.



Sunday, January 27, 2013

YANGA WAWAONESHA MAAFANDE WA PRISON SOKA SAFI LA KITURUKI

Jerry Tegete akichomoka kushangilia baada ya kuifungia Yanga bao la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya TZ Prisons Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii. Yanga ilishinda 3-1.

Na Mahmoud Zubeiry
YANGA SC imezidi kupaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya jioni hii kuitandika Prisons ya Mbeya mabao 3-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga imetimzia pointi 32 baada ya kucheza mechi 14, hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa wastani wa pointi tano, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 27 na Simba 26.
Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa tayari zimefungana bao 1-1, Yanga wakitangulia kupata bao lao dakika ya 10 kabla ya Prisons kusawazisha dakika ya 17.
Bao la Yanga lilifungwa na Jerry Tegete aliyeunganisha krosi nzuri ya Simon Msuva kutoka wingi ya kulia, wakati la Prisons lilifungwa na Elias Maguri, aliyeunganisha krosi nzuri ya Misango Magai kutoka wingi ya kushoto.
Tegete akiigusa nembo ya Yanga baada ya kufunga la tatu.
Yanga walicheza vizuri dakika 15 za mwanzo na baada ya hapo, timu hizo zilianza kushambuliana kwa zamu, ingawa Watoto wa Jangwani ndio waliopoteza nafasi nzuri zaidi za kufunga.
Kipindi cha pili, Yanga walirudi na kasi nzuri kusaka ushindi na iliwachukua dakika 11 tu kupata bao la pili, lililofungwa na Mbutu Twite baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Prisons.
Wakati Prisons wakiwa kwenye jithada za kusaka bao la kusawazisha, walijikuta wakitandikwa bao la tatu, Tegete tena akiwainua vitini mashabiki wa Yanga, baada ya kupokea pasi nzuri ya Nurdin Bakari dakika ya 65.
Baada ya bao hilo, Yanga walianza kuonyesha vitu vya Uturuki walipoweka kambi ya wiki mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko huu wa pili wa Ligi Kuu, wakicheza soka ya madoido pasi nyingi, uzungu na kila aina ya mbwembwe, ili mradi tu kuwaburudisha mashabiki wake.
Mapema kabla ya mchezo huo, kiungo wa Yanga, Frank Domayo alipatwa na Malaria ya ghafla na kuenguliwa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi yake akaanza Nurdin Bakari, wakati mshambuliaji mpya wa Prisons, Emmanuel Gabriel alienguliwa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi yake akachukua Elias Maguri, kwa sababu ya kutokuwa na leseni ya TFF ya kumruhusu kucheza Ligi Kuu. Suala la leseni ya Gabriel, dhahiri ni uzembe wa viongozi wa Prisons.
Katika mchezo wa leo, 
kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite/Juma Abdul dk 82, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Nurdin Bakari/David Luhende dk 66, Didier Kavumbangu/Hamisi Kiiza dk 64, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.

TZ Prisons; David Abdallah, Aziz Sibo, Henry Mwalugala, Lugano Mwangama, Jumanne Elfadhil, Nurdin Issa, Sino Augustino, Freddy Chudu, Elias Maguri, Misango Magai/John Matei dk58 na Jeremiah Juma. 

Kiungo wa Yanga, Frank Domayo akiwa amelala katika zahanati ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mida hii, baada ya kupatwa na Malaria ya ghafla. Domayo ilikuwa aanze mechi ya leo, lakini kutokana na kuugua huko ghafla, sasa nafasi yake ataanza Nurdin Bakari.

Kiungo wa Yanga, Frank Domayo akiwa amelala katika zahanati ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mida hii, baada ya kupatwa na Malaria ya ghafla. Domayo ilikuwa aanze mechi ya leo, lakini kutokana na kuugua huko ghafla, sasa nafasi yake ataanza Nurdin Bakari.



UJUMBE WA SEKRETARIETI YA CCM WAWASILI SALAMA MKOANI KIGOMA LEO


 Wananchi wa Mkoa wa Kigoma leo wameupokea kwa shangwe Ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) uliowasili mkoani Kigoma ukitokea jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa Treni Reli ya Kati.
Wajumbe hao ambao wanaoongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana ni pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM,Martin Shigela.
Akizungumza baada ya kuwasili Mkoani Kigoma leo, Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana alisema kuwa lengo la wao kutumia usafari huo wa Treni ni kuwadhihirishia wananchi wa Tanzania kuwa Usafiri wa Treni ni Usafiri wa uhakika na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kupitia Wizara ya Uchukuzi, itasimamia kikamilifu usafiri huo na kuendelea kuuboresha zaidi ya ilivyo sasa na kuhakikisha safari zinaongezeka na kuwa za kila siku na si kuwa kwa wiki mara mili kama ilivyo sasa.Nao baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma wameipongeza sana Sekretarieti hiyo kwa uamuzi wao wa kusafiri kwa kutumia Treni kutoka jijini Dar es Salaam hadi Mkoani Kigoma na kujionea hali halisi ya usafiri huo.
Ujumbe huo upo Mkoani Kigoma kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachama pamoja na wananchi wa mji wa Itigi mkoani Singida wakati Treni iliposimama kwa muda mfupi katika mji huo.


Wananchi wa Mkoa wa. kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.


Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa wamekusanyika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akizungumza nao.

Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakielekea kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM wakati ukiwasili Mjini Kigoma leo.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Mji wa Kigoma waliofika kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM uliowasili mjini Kigoma leo kutokea jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Treni ya Reli ya kati.



Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na wananchi wa Mji wa Kigoma waliofika kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM uliowasili mjini Kigoma leo kutokea jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Treni ya Reli ya kati.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma ya utamaduni ya mkoa wa Kigoma iliyokuwa ikipigwa Stesheni leo,huku Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akipiga moja ya ngoma hizo.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) akipena mkono na Dereva wa Treni ya TRL,Bw. Kambi Ali (wa pili kulia) aliyewasafirisha kutoka Jijini Dar es Salaam mpaka Mjini Kigoma salama. Wengine pichani ni Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM), Nape Nnauye.




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU