Facebook Comments Box

Saturday, April 13, 2013

NDEGE YA MAREHEM WAKILI NYAGA YAANGUKA ARUSHA NA KUUA


Ndege iliyokuwa inamilikiwa na Wakili Maarufu Marehem Nyaga Mawalla aliyefariki wiki tatu zilizopita na kuzikwa Nairobi, imeanguka ikiwa katika hatua za mwisho za kutua katika uwanja wa Ndege wa Arusha
Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani pekee anayejulikana kwa jina la Jamal B S, au maarufu kama "Bob Sambeke" aliyekuwa anatokea West Kilimanjaro ambaye naye kapoteza maisha (kafariki)!
Inadaiwa kuwa ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida ya kufunga kiwanja (saa 12.30 jioni) kupita.


JE WAJUA NI MUDA GANI KWA MIAKA,MIEZI,SIKU,SAA NA SEKUNDE TOKA ARSENAL WACHUKUE KOMBE?

Hii ni kwa mujibu wa tovuti maalumu iliyo anzishwa kwa ajili ya kuhesabu muda huo inayojulikana kama www.sincearsenallastwonatrophy.co.uk




FULL TIME: YANGA 3 - 0 JKT OLJORO

FULL TIME: YANGA 3 - 0 JKT OLJORO

DK 45 Saidi Bahanuzi anakosa goli hapa akiwa yeye na kipa. Refa anaongeza dakika 5 za nyongeza

DK 31 Said Bahanuzi anaotea hapa. Amekuwa akiotea mara kwa mara hii inatokana labda na kuwa na usongo wa kufunga

DK 22 BAHANUZI anafunga goli ila refa anasema amekwisha otea

DK 14 anaingia Said Bahanuzi kuchukua nafasi ya Kavumbagu alie umia 

DK 5 OLJORO wanafanya mabadiliko anatoka Golikipa na kuingia mwingine (Shaibu Mussa)

KIPINDI CHA PILI NDIO KINAANZA

HALF TIME: YANGA 3 - 0 JKT OLJORO

DK GOOOOOOOL Hamis Kiiza anaipatia Yanga bao la tatu. Hii ni baada ya pasi zinazojulikana kama 'One two' wakiwa watatu. Yanga 3 Oljoro 0. Refa anaongeza dakika 3 za nyongeza

DK 43 Athumani Idd Chuji anapiga shuti kali na linatoka sentimita chache kutoka golini

DK 40 Yanga 2 - 0 JKT Oljoro. Mpira unaonekana kuelemea upande mmoja Yanga wamekuwa  wakilishambulia sana goli la wapinzani wao

DK 39 Saimon Msuva anaingia na mpira na kupiga shuti kali linalopanguliwa na goli kipa

DK 31 Shadrack Nsajigwa anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul

DK 30 Nsajigwa anapasha inaonekana Juma Abdu hawezi kurudi uwanjani
 
Dk 19 GOOO...! Msuva anaifungia Yanga bao la pili baada ya kuipangua ngome ya Oljoro na kupiga shuti hafifu. YANGA 2-0 OLJORO

Dk 16 Oljoro wanaonekana wamezinduka nao wameanza kutawala kiungo huku wakicheza pasi fupi fupi.


Dk 13 Paul Nonga wa Oljoro anatengewa mpira vizuri na Idd Swaleh lakini shuti lake linatoka nje ya lango la Yanga.


Dk 10 Yanga imetawala mchezo hasa kiungo na imefanya mashambulizi mengi langoni kwa Oljoro.


Dk 5 GOOO....! Nadir Haroub 'Cannavaro' anaipatia Yanga bao la kwanza kwa kichwa akiunga mpira wa kona. YANGA 1-0 OLJORO


3 Simon Msuva wa Yanga anapiga shuti kali langoni kwa Oljoro kipa anaupangua na kuwa kona. Kipa anaumia baada ya kuucheza mpira huo. Mchezo unasimama ili kipa atibiwe.


Dk 1 Juma Abdul wa Yanga anapiga shuti kali langoni kwa JKT Oljoro lakini kipa Lucheke Musa anaudaka mpira. Abdul alipewa pasi na Frank Domayo.


Dk 00 MPIRA UMEANZA!


Young Africans line-up to face JKT Oljoro today

1.Ally Mustafa 'Barthez'
2.Juma Abdul
3.David Luhende
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Athuman Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo 'Chumvi'
9.Didier Kavumbagu
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima


Subs:
1.Yusuph Abdul
2.Shadrack Nsajigwa
3.Oscar Joshua
4.Salum Telela
5.Nurdin Bakari
6.Nizar Khalfani
7.Said Bahanuzi


JKT Oljoro:
1.Lucheke Musa, 
2.Yusuf Machogoti,
3. Majaliwa Sadiki, 
4. Nurdin Mohamed,
5.Shaibu Nayopa, 
6.Salim Mbonde, 
7.Karage Mgunda, 
8.Emmanuel Memba, 
9. Paul Nonga, 
10.Idd Swaleh 
11.Hamis Salehe.


STARSTIMES WAPANDISHA BEI YA VIFURUSHI VYAO


Ikiwa ni miezi minne tu imepita toka tulipoingia rasmi kwenye mfumo dijitali (digital system) kwa vituo vya televisheni.. Startimes wamepandisha gharama ya vifurushi.. 
Kile kilichokuwa kinauzwa Tshs. 9,000 sasa kitauzwa Tshs. 10,000.. 
Kile cha Tshs. 18,000 sasa kitakuwa Tshs. 20,000.. Kile cha Tshs. 36,000 sasa kitakuwa ni Tshs. 40,000.. Itaanza rasmi tarehe 15 April..
TCRA waliahidi mambo  mengi  mazuri kwenye mfumo dijitali..Ahadi  yao  imegeuka  na  kuwa  ndoto.....

Vifurushi  vinapanda  huku  huduma  ikiwa  ni  mbovu  hasa  kwa  hawa  Startimes


HUU NDIO WIZI MWINGINE MKUBWA WA FEDHA ZA WATANZANIA


Huu ndio wizi mwingine mkubwa ulioibuliwa na Mh Zitto Kabwe Kuhusu fedha za Tanzania zinazochotwa na kulipia madeni hewa. Mh Zitto Ameyahabarisha hayo katika ukurasa wake wa Facebook na kusema hiyo ni Kashfa nzito kuwahi kupatikana katika nchi hii. Unaweza kuisoma hapo chini jinsi alivyo iweka.




HIZI NDIO MOVIES MPYA TATU KALI ZA KUANGALIA WEEKEND HII








VITUKO VYA MAJUU


Hawa jamaa wao wameweka foleni ya viatu baada ya kuona muhudumu hayupo
Hili gari sijui litafika bongo lini?


RUSHWA NI RAFIKI WA HAKI

 
Huu mjadala wa Katiba umeanza kusisimua kweli.  Laiti tungekuwa na muda zaidi, nadhani tungejifunza mengi.  Hebu ona barua hii.

Wewe Makengeza,
Wewe kwa kweli unakuwa kipofu.  Katika kulilia mavi ya kale unashindwa kuona mazuri yaliyopo.    Si binadamu tu wanaobadilika kulingana na wakati, hata nchi inapaswa kufanya hivyo, bila unafiki, bila kificho.
Hebu tuchukue mfano wa katiba yetu iliyopitwa na wakati.  Yaani bado inatangaza kwamba tunafuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.  Nani anadanganyika na uongo huo?  Labda vijana ambao wanafikiri Azimio la Arusha linahusu ujenzi wa barabara mjini na kwamba ujamaa maana yake ni kusaidiana kukwapua yanayokwapulika.  
Ujamaa ni hujumaaa!  Bila kusahau kwamba kujitegemea ni kutafuta wafadhili na mafedhuli wengi iwezekanavyo kutoka nje.   Haisaidii!
Kwa hiyo, si vizuri kuendelea kuwa na maneno tata ndani ya katiba.  Lazima kuwa na dira ya kutuongoza na hata kututongoza tukubali kujitoa na kujitosa katika maendeleo ya nchi yetu changa ya macho.
Ndiyo.  Hebu angalia uchaguzi unavyoendelea kwa sasa kupata wajumbe wa mabaraza ya kata.  Ni wajumbe tu wa mabaraza ya kata wenye lengo la kutoa mawazo kuhusu katiba yetu iweje.   Lakini badala ya watu kujinadi kwamba wana mawazo haya au yale kuhusu katiba, wanatwangana ngumi kwa misingi ya makundi ndani ya chama hiki au kile.
Waliofanikiwa kuchaguliwa kwenye ngazi ya mtaa wanadaiwa rushwa ili wapite kwenye ngazi ya kata na kadhalika.   Bila kuhonga, hata nafasi ya kuchangia Katiba Mpya huwezi kupata.
Kwa hiyo, waliofikiria kwamba Katiba ni suala la kuwatafuta watu wenye mawazo chanya ili kuwa na Katiba ambayo itatulinda sisi wa kizazi hiki pamoja na vizazi vijavyo vyote wanajidanganya.   Au tuseme kwamba wanaogombea nafasi hizo za kuingia kwenye mabaraza ya kata wameelewa kitu cha msingi sana kuliko wasomi wote wanaobwatia nadharia.  Mchakato wa katiba ndiyo dira ya Katiba.  
Bila rushwa, nchi yetu haiwezi kuendelea.  Naamini kwamba wananchi wote wameelewa hivyo ndiyo maana wanaendelea kubariki mtindo huu wa kupata wajumbe na mambo mengine yote ndani ya jamii yao.  Msingi huo ni wazi pia.  Nikilinyamazia jambo fulani maana yake nimelikubali.
Kwa hiyo napenda kutangaza kwamba katika misingi ya taifa inayoorodheshwa ndani ya Katiba, itangazwe rasmi kwamba ‘Tanzania ni nchi ya rushwa na kujitafutia’.   Kwa njia hiyo,  tunakuwa mfano bora wa uwazi na ukweli na pia tunaweza kuwashughulikia watu wahafidhina kama wewe mnaotaka kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.  
Hebu tutafakari kidogo.  Juzi, nilipanda daladala kwenda vijijini. Wakati tunaanza safari jamaa mmoja alikuwa anamcheka mwimbaji maarufu eti analalamika kwamba wimbo wake hauchezwi na kituo cha redio kwa kuwa hajatoa hela.
‘Hajui methali isemayo ‘Penya udhia tia rupia’!’

SOURSE: MWANANCHI


YANGA KUJAZWA MAPESA WAKIIVUA UBINGWA SIMBA LEO

Mashabiki wa timu ya Yanga wakiishangilia timu yao siku za hivi karibuni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
YANGA ikishinda mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya JKT Oljoro itaivua rasmi Simba ubingwa lakini itahitaji pointi nyingine saba kufuta ndoto za Azam kuwa bingwa.

Wanachama na matajiri wa Yanga wameingia mstari wa mbele kuhakikisha timu hiyo inashinda mechi zote tano zilizosalia na kufuta jeuri ya Azam ambao kasi yao imeanza kutishia amani ya mtaa wa Jangwani walio kileleni.
Azam inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 46 na Yanga ikishikilia usukani na pointi zake 49 jambo ambalo limezua mshtuko.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba uongozi wa Yanga utatoa Sh.70,000 kwa kila mchezaji kwa kila mechi wanayoshinda. Kwa mechi tano zilizosalia wakishinda timu nzima italamba Sh.10 milioni kwa wachezaji 29.

Lakini matajiri chini ya hamasa ya Abdallah Binkleb na Seif Ahmed Seif Magari wameingiza mkono wao ambapo wameahidi Sh.5 milioni kwa kila mechi Yanga watakayoshinda ingawa kuna wengine wameahidi kuongeza kuanzia mechi ijayo.

Habari za ndani zinasema kuanzia mechi ijayo watakuwa wakipewa dau la Sh.10 milioni na wataanza kununua idadi ya mabao yanayofungwa ili kuwajengea wachezaji morali ya kupachika mabao mengi lengo likiwa ni kurudisha kipigo cha mabao 5-0 watakapokutana na Simba Mei 18.

Simba ndio mabingwa watetezi ambao wakishinda mechi zao tano zilizobaki ikiwemo dhidi ya Azam kesho Jumapili na Yanga Mei 18 itatimiza pointi 50 ambazo Yanga ikishinda leo Jumamosi inazipita hivyo kubakiwa na kazi moja tu ya kuidhibiti Azam.

Yanga ina pointi 49 ikishinda mechi tatu ambazo ni dhidi ya Oljoro, Mgambo na JKT Ruvu pamoja na sare dhidi ya Coastal Union itafikisha pointi 59 ambazo Azam haiwezi kuzifikia kwani ikishinda mechi zake zote itakomea pointi 58.

Kocha wa Yanga, Ernie Brandts ambaye atawakosa nyota wake tegemeo kama Mbuyu Twite mwenye kadi tatu za njano, Jerry Tegete na Stephano Mwasyika ambao hawako fiti kwa asilimia 100 tayari ameshawaambia mabeki, viungo na washambuliaji kuwa ni jukumu lao kufunga mabao katika mechi hiyo na nyingine.

Na katika kuhakikisha anafanikiwa, Brandts aliwahamishia mafichoni nyota wake katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola kutoka Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Yanga inakutana na Oljoro ambayo haipo katika hofu kubwa ya kushuka daraja ikiwa nafasi ya nane na pointi 28 na katika kujiwekea mazingira mazuri ilifika mapema tangu wiki iliyopita na kujificha Ruvu, Pwani.

Brandts alisema: Lengo ni pointi tatu tu. Kutokana na hilo nimewasuka wachezaji wangu wote katika kuhakikisha kila mmoja anafunga na kuzuia.


SOURSE: MWANASPOTI

VIDEO: WABUNGE WALIVYO LUMBANA KUHUSU UGAIDI




KIBONZO: KUPANDA KWA NAULI ZA DALADALA



HII NDIO TAARIFA YA UTAFITI WA KUFELI KWA KIDATO CHA NNE



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU