NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Juma Kaseja amejiunga na timu ya Ashanti United ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara akitokea timu ya Ndanda FC inayocheza daraja la kwanza kama kocha wa makipa wao na anatarajiwa kuanza kuichezea rasmi Januari mwakani, baada ya kuchelewa dirisha la usajili.
Kocha wa makipa wa timu hiyo ya Ilala, Dar es Salaam, Iddi Pazi ‘Father’ amesema jana kwamba Kaseja amejiunga na Ashanti United na amekwishaanza kazi.
Father, alisema kwamba pamoja na Kaseja, pia Ashanti imempata kipa mwingine mzoefu, Amani Simba SC ambaye naye amekwishaanza mazoezi.
“Nipo na Amani Simba na Juma Kaseja hapa Ashanti, naamini wote ni makipa wazuri na watachuana ili kurejea matawi ya juu. Nitawafanyia kazi na watakuwa makipa bora tena,”alisema Pazi, baba wa mshambuliaji wa Simba SC, Zahor Pazi.
Kaseja aliachwa Simba SC mwishoni mwa msimu baada ya kuitumikia timu hiyo tangu mwaka 2003 alipojiunga nayo akitokea Moro United.
Baada ya hapo, alipata ofa ya kwenda St. Eloi Lupopo ya DRC, lakini wakashindwa kuafikiana na kuamua kuangalia ustaarabu mwingine. Wakati wa maandalizi ya msimu mpya, Kaseja alikuwa akifanya mazoezi na Mtibwa Sugar iliyokuwa imeweka kambi Dar es Salaam.
Juhudi za kumpata Kaseja mwenyewe kuthibitisha kujiunga kwake na Ashanti hazikuweza kufanikiwa mapema.
Wednesday, September 18, 2013
KASEJA AJIUNGA NA ASHANTI AKITOKEA NDANDA FC YA DARAJA LA KWANZA
WABUNGE WA NIGERIA WAPIGANA BUNGENI
MWIMBAJI WA ZANZIBAR NJEMA MODERN TAARAB PRINCE AHMED MGENI AFARIKI DUNIA
AHMED MGENI WAKATI WA UHAI WAKE KATIKA PICHA TOFAUTI JUU HAPO
Mgeni alikutwa na umauti huo baada ya kuugua TB ya tumbo kwa muda mrefu anatarajiwa kuzikwa leo visiwani humo.
Enzi za uhai wake msanii huyo aliyepata kuimba katika bendi mbalimbali sambamba na kutoa nyimbo kadhaa zilizoteka alikutwa na umauti huo Alfajiri saa kumi ya kuamkia leo alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja, Zanzibar.
Moja ya kibao kilichompatia umarufu kilijulikana kama Sitetereki "Mlinzi wa kweli ni Mungu aso hiyana na mtu sio wewe mlimwengu hunibabaishi kitu.....
POLISI WAWILI WAKAMATWA WAKISAFIRISHA RISASI 3, 000
Polisi wawili wa Musoma, Mkoa wa Mara na Kibaha, Pwani wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha risasi 3,000 kutoka Musoma kwenda Dar es Salaam.
Wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni aliyekuwa mtunza chumba cha silaha Kikosi cha FFU Musoma na mwenzake mwenye cheo cha Koplo Wilaya ya Kibaha, Pwani. Inadaiwa walikamatwa Juni 2, mwaka huu saa 11:00 alfajiri.
Watuhumiwa wanashikiliwa Kituo cha Polisi Musoma na wamefunguliwa jalada MUS/RB/2465/013 wizi wa risasi 1,056, wanasubiri taratibu zingine za polisi.
Habari zinadai shehena hiyo ilisafirishwa kwa kutumia pikipiki hadi Kituo cha Mabasi, lakini polisi tayari walikuwa wameweka mtego baada ya kupata taarifa kuhusu wizi huo.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwamo wahusika wa basi na nyumba moja ya kulala wageni iliyopo jirani na stendi, baadhi ya askari waliovaa kiraia walionekana maeneo hayo mapema.
Kwa mujibu wa habari za uhakika kutoka ndani ya polisi, Koplo huyo alikutwa na shehena hiyo karibu na kituo cha mabasi ya Kampuni ya Mohammed Trans, akijiandaa kuelekea Dar es Salaam ambako inasemekana wana wateja wao.
Inadaiwa koplo huyo aliomba ruhusa ya ugonjwa kazini kwake na kuitumia kusafiri hadi Musoma kuchukua mzigo huo, inadaiwa biashara yao hiyo ni ya muda mrefu na wana mtandao na watuwanaojihusisha na uhalifu.
Mtandao huo unadaiwa kuwagusa baadhi ya polisi Mkoa wa Tarime na Rorya, ambao huwauzia watu wanaojihusisha na uhalifu wa kutumia silaha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma alipotafutwa kwa simu zake za mkononi licha ya kuitwa, hazikupokewa.
Hata hivyo, aliomba atumiwe ujumbe, licha ya kupelekewa huo ujumbe, hakujibu ingawa taarifa zinadai ameanza likizo ya kustaafu hivi karibuni.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara, Jafari Mohammed alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alikanusha kufahamu suala hilo huku akigeuka kuwa mkali kwa mwandishi.
“Hilo mimi silijui, nani kakwambia wewe… askari kukutwa na risasi mfukoni ni jambo la kawaida huenda ni uzembe tunamshughulikia kwa uzembe,” alisema.
CHANZO: Mwananchi