Facebook Comments Box

Monday, July 1, 2013

VIDEO: WALE WAPENZI WA KIPINDI CHA MKASI LEO KIPO TENA HEWANI

PICHA: BARABARA IKIPINGWA DEKI KWA AJILI YA OBAMA

HAYA NDIO MAPITO ALIYO PITIA BARACK OBAMA

PictureObama na viatu vyake vilivyochakaa soli
Ndugu zangu,

Obama anasema; "Wakati tukiendelea na masomo yetu ya Sheria mimi na Michelle tulifanya kazi katika kampuni ya Uwakili ya Sidley na Austin jijini Chicago.

Binafsi nilikuwa na wasi wasi kuhusu ujana wangu na hasa changamoto kuwa maisha ya sasa ni fedha. Hofu yangu ilikuwa ni lini nitaanza kukamata fedha nyingi ili zisaidie mawazo na fikra zangu kufikia mahala ninapotaka.

Lakini, kutokana na kupanda kwa gharama na mkopo niliyochukua Serikalini kwa ajili ya masomo, niliamua kuendelea kuwatumikia mabwana wawili; chuo na kampuni ya sheria.

Nilijitahidi kadiri nilivyoweza kundunduliza sehemu ya kipato changu . Hatimaye nilifanikiwa kuwa na chumba. Nilinunua suti zangu tatu na pia jozi moja ya viatu.

Hata hivyo, wakati nanunua viatu sikuwa makini, kwani vilionekana vidogo; vilivyonibana na kunifanya nionekane mshamba. Siku niliyopiga ripoti ofisini, kila mmoja aliniangalia.

Ingawa sikujua ni kwa nini, lakini nilihisi walifanya hivyo kutokana na viatu vyangu!"- Barack Obama ( Kutoka kijitabu cha Maisha Ya Barack Obama, alikotoka, aliko na anakokwenda, Maggid Mjengwa, 2008.)

Maggid,
Iringa.
0754 678 252
mjengwablog.com

HUYU NDIO MWANAFUNZI ALIE FUMANIWA GUEST HOUSE NA WAZAZI WAKE

Mwanafunzi mmoja amefumaniwa katika nyumba moja ya wageni (guest house) hapo jana, tarehe 29/6/2013 majira ya saa nane mchana katika eneo la Yombo Vituka jijini Dar es salaam.

Hata hivyo mfumaniwa mwenzake hajakamatwa kwani aliponyoka na kukimbia.

(Picha zote na maelezo yameletwa na Dei Misana)
Picture
Wazazi wa uchungu na hasira wakiwa na binti yao mara baada ya fumanizi.
Picture
Hii ndio sura halisi ya binti aliyefumaniwa.
Picture
Chumba kilichotumika kwa kwa mwanafunzi huyo, mwenzake kufanyia ufuska.
Picture
Wazazi wakimpiga binti yao kwa uchungu na hasira mara baada ya fumanizi.

Source: WAVUTI

HII NDIO RATIBA NZIMA YA OBAMA AKIWA TANZANIA

Picture
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 01 Julai, 2013 mchana kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Obama ambaye atafuatana na Mkewe Mama Michelle atapokelewa na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Baada ya mapokezi, Mhe. Rais Obama atakwenda Ikulu kwa mazungumzo rasmi na Rais Mhe. Kikwete. Aidha, atafanya mkutano na Wafanyabiashara na kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa.

Tarehe 2 Julai 2013, Mhe. Rais Obama atatembelea Mitambo ya kufua Umeme ya Symbion iliyopo Ubungo, Dar es Salaam na kuzindua rasmi Mpango Maalum wa Maendeleo ya Nishati Barani Afrika ulioanzishwa na  
Marekani (Power Africa Initiative).

Mpango huo utaanza na nchi saba ambazo ni: - Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Sudan Kusini.

Mhe. Rais Obama anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 02 Julai 2013.

IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
30 JUNI, 2013

Monday, July 1, 2013
  • On Monday afternoon, President Obama takes part in a formal arrival ceremony in Dar es Salaam, Tanzania.
  • President Obama participates in a bilateral meeting and joint press conference with President Jakaya Kikwete of Tanzania.
  • In the evening, President Obama participates in a CEO roundtable and business leaders forum.
  • President Obama and President Jakaya Kikwete of Tanzania participate in an official dinner.

Tuesday, July 2, 2013

  • On Tuesday morning, President Obama takes place in a Consulate meet and greet.
  • President Obama visits the Ubungo Power Plant.

Atakapowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na ndege yake  Air Force One, Rais w Maekani, Barack Obama atazindua barabara mpya upande wa Mashariki wa lango la kuingia Ikulu ambayo inatarajiwa kuitwa Barack Obama.

Baada ya shughuli hiyo atazungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara wa nchi za Afrika na Marekani kwenye hoteli ya Hyatt Regency,  Dar es Salaam.  Amepanga pia kuzungumza na maofisa wa Ubalozi wa Marekani nchini.

Baadaye atahudhuria dhifa ya taifa usiku ambayo imeandaliwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.

Kesho ataweka shada la maua sehemu ulipokuwa Ubalozi wa Marekani ikiwa ni kumbukumbu ya watu waliouawa katika shambulizi la kigaidi la bomu mwaka 1998, Dar es Salaam. Pia atatembelea mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Symbion iliyoko Ubungo.

Rais Obama atatoa hotuba kuzungumzia mikakati ya Marekani ya kusaidia Afrika kuzalisha nishati ya umeme.

Michelle atakuwa na ratiba yake ambapo atapata staftahi na mwenyeji wake, Salma Kikwete katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), Dar es Salaam.

Pia atatembelea sehemu ulikokuwa ubalozi wa Marekani na kisha atashuhudia onesho la utamaduni la kikundi cha Baba wa Watoto, ambacho kinajumuisha watoto wa mitaani wenye umri wa kuanzia miaka mitano hadi 18 kwenye Makumbusho ya Taifa.

Jumanne, Michelle atahudhuria mkutano na wake wa marais wa nchi za Afrika ambao pia utahudhuriwa na mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush, Laura.

Julai 2, Rais Obama atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Symbion Ubungo saa 4 asubuhi na kisha msafara wake utapita Nelson Mandela, Tazara hadi uwanja wa ndege na kuondoka saa 5.20 asubuhi.
Obama ametangaza mpango wa kuwajengea uwezo viongozi vijana wa Afrika kwa kuwapa mafunzo ya uongozi katika vyuo vikuu vya Marekani hasa katika masuala ya utawala, biashara na uongozi.

Katika hotuba yake katika Chuo Kikuu cha Johannesburg juzi jioni, alisema hatma ya Afrika iko mikononi mwa vijana; hivyo ni lazima wawezeshwe ili kuliongoza vizuri bara hili.

Alisema mafunzo hayo yatatolewa  chini ya mpango wa ufadhili wa Marekani kwa viongozi vijana ambao utawajengea uwezo wa kuendesha huduma za kiserikali ikiwa ni pamoja na biashara na   kuhudumia jamii yao.

Kuanzia mwaka ujao Marekani itatoa mafunzo kwa vijana 500 ambayo yatakuwa ya wiki sita ambapo idadi hiyo itaongezeka hadi vijana 1,000 kila mwaka.

Watakaofadika ni vijana wa kati ya umri wa miaka 25 hadi 35 ambao wamekuwa wakijihusisha na uongozi  ndani ya Serikali, sekta binafsi na asasi za kiraia. Alisema washiriki hao ni lazima waoneshe dhamira yao katika kuitumikia jamii.

Obama alisema Afrika ina mwonekano mzuri kwa siku zijazo na kuwataka vijana wa Afrika kuhakikisha wanatumia uwezo wao katika kutumikia bara lao.

Mpango wa kuendeleza vijana wa Afrika ujulikanao kama YALI ulizinduliwa mwaka 2010 na Rais Obama ikiwa ni sehemu ya kusaidia maendeleo, kuhamasisha ujasiriamali na kujenga uwezo wa Afrika kuwa na viongozi bora wa kizazi kijacho.

ZITTO AMUAMBIA OBAMA TUNATAKA UWAZI WA MIKATABA NA AOMBE RADHI KWA MAUAJI YA LUMUMBA

Hatimaye Barack Obama, Rais wa Marekani anatembelea tena bara la Afrika. Hii itakuwa ni mara ya pili Obama kutembelea Bara hili alikotoka baba yake baada ya ziara yake ya kwanza mwaka 2009. Mwaka huo alitembelea Ghana na Misri ilhali mwaka huu anatembelea Senegali, Afrika Kusini na Tanzania. Ziara hiyo itakayoanza tarehe 26 mwezi Juni, itamfikisha Tanzania tarehe 1 Julai na kuondoka siku ya pili yake.

Uchaguzi wa Obama kuwa Rais wa Marekani ulipokolewa kwa shangwe Afrika nzima. Wakati Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alilia kwa furaha, nchi ya Kenya ilitangaza siku ya mapumziko na Rais wa zamani wa Afrika Kusini ndugu Nelson ‘Madiba’ Mandela alisema ‘ushindi wa Obama unawafanya Waafrika wathubutu kuota ndoto (Jarida la The Economist). Hapa Tanzania kulikuwa kuna shamra shamra za kila namna na magazeti yaliweka vichwa vya habari kana kwamba ni Rais wa Tanzania aliyechaguliwa.

Waafrika walikuwa na matumaini makubwa sana na bwana Obama. Yamefikiwa?
Ni vema ifahamike kuwa Barack Obama ni Rais wa Marekani na siku zote atalinda maslahi ya Marekani tu. Kuwa na matumaini makubwa kwamba labda yeye angeliweza kuiweka Afrika mbele sana ilikuwa ni kujifurahisha tu nafsi. Maslahi ya Marekani ni ya kipaumbele kuliko kitu kingine chochote kwa Rais Obama. Kwa wengi Obama amekuwa kama amewavunja moyo.

Tanzania inapokea kiongozi wa Taifa kubwa duniani wa pili sasa ndani ya kipindi cha miezi 3 tu. Kwanza alikuja Rais wa China na sasa wiki hii anakuja Rais wa Marekani. Maneno ya mtaani na kwenye mabaraza ya majadiliano ni kwamba viongozi hawa wanakuja kugombea maliasili tulizo nazo kama gesi asilia na madini. Nadhani haya ni maneno ya kusema katika kupiga soga maana kunyonywa kwa rasilimali hakuhitaji Rais wa Marekani aje Tanzania. Makampuni yote makubwa yanayochimba dhahabu hapa nchini ni makampuni ya nje na marais wao hawakuja ili waweze kupata mikataba minono ya kuvuna utajiri wetu. Katika kitalu namba 2 cha utafutaji wa mafuta na gesi huko Bahari Kuu kampuni ya kimarekani ya ExxonMobil ina ubia na kampuni ya Norway ya StatOil. Kampuni hiyo haikusubiri Rais wa Marekani aje ili wapate mikataba.

Kuna makampuni mengi sana ya kichina yanajenga barabara zetu hapa nchini yakiwa na mikataba minono sana. Kule Mchuchuma na Liganga kuna kampuni ya kichina inajiandaa na uchimbaji wa chuma na makaa ya mawe. Makampuni yote haya hayakusubiri Rais wao aje.

Hoja inayojengwa hapa ni kwamba ujio wa Marais mbalimbali nchini ni ujio wa kujijenga kidiplomasia na wakati mwingine kama sehemu ya kutuma ujumbe Fulani kwa dunia. Nchi inayotembelewa pia inaweza kuona kuwa diplomasia yake inaheshimiwa na mataifa yanayoitembelea.

Hata hivyo hii haiondoi ukweli kwamba Obama anakuja kwa ajili ya maslahi ya nchi yake kama ilivyo kwa wachina walivyokuja. Tumesikia Rais Obama ataambatana na mamia ya wafanyabishara kutoka Marekani kwa ajili ya kupata fursa za kuwekeza nchini. Pia tutasikia matangazo kuhusu msaada wa pili wa Millenium Challenge ambapo Wamarekani wanaendelea kumwaga pesa nchini kusaidia miundombinu lakini pia kushawishi kuungwa mkono na nchi zetu kwenye maamuzi Fulani Fulani jumuiya za kimataifa.

Tumesikia Obama atakwenda kutembelea mitambo ya kampuni ya Symbion. Hii ni mitambo ambayo miaka 4 iliyopita ilipigiwa kelele kuwa ni mitumba na hivyo TANESCO wasiinunue. Hawakununua na badala yake kampuni hiyo ya kimarekani ikainunua, wakaingia mkataba na TANESCO kuwauzia umeme unaozalishwa na mitambo hiyo hiyo chakavu. Wakati tunasuburi kulipa takribani tshs 105 bilioni kwa Dowans baada ya kutubwaga kwenye kesi, tunasubiri kuona wanasiasa watakaokwenda kumsindikiza Obama kwenye matembezi hayo ya kutembelea mitambo chakavu.

Kampuni kubwa ya kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme ya GE imetangaza kuingia ubia na kampuni ya Symbion kuzalisha umeme nchini. Takribani 400MW zitazalishwa kutoka Mtwara na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa. Pia sehemu kubwa ya umeme utakaozalishwa Mtwara tayari umepata soko kwenye kiwanda cha kuzalisha udongo ulaya (simenti) cha bwana Dangote kule Mtwara. Mtendaji Mkuu wa GE bwana Jeff Immelt ametangaza kuwa kampuni yake itauza mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi mingi zaidi Afrika Mashariki kuliko Marekani katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Ni biashara tu!

Nishati naona ni kipaumbele kikubwa sana kwa ziara ya Rais Obama. Kwa nchi kama yetu yenye watu asilimia 21 tu wenye umeme, ni dhahiri kipaumbele hiki watu wengi watakiiunga mkono. Hata hivyo Obama ni lazima asimame kidete kuhakikisha kuwa kampuni za nchini mwake zinazopata miakataba hapa nchini ziweke wazi mikataba hiyo na kulipa kodi inavyostahili. Makampuni ya mafuta kutoka Marekani hayana historia nzuri duniani na hivyo ni lazima tulisisitize mapema kabisa. Uwazi wa mikataba na uwezo wa kupambana na ukwepaji kodi ni muhimu sana katika vita dhidi ya Ufisadi na ubadhirifu.

Rais Obama atambue kuwa iwapo Tanzania ingekuwa inakusanya nusu ya kodi zinazokwepwa na makampuni makubwa yanayotumia mbinu kali, basi tungehitaji misaada ya Marekani na hapa nchini angekuja kama mbia wa kweli na sawa katika dunia. Hivyo ni vema aungane na Waziri Mkuu wa Uingereza kuhakikisha kuwa makampuni makubwa hayatumii ‘tax havens’ kukwepa kodi katika nchi kama Tanzania. Uwazi wa mapato yao na kilicholipwa kwa Serikali ni vema usisitizwe sana na Obama mwenyewe ili makampuni yao yasikie na yaache kupora utajiri wa Afrika kiujanja ujanja.

Mwisho ni vema kama Rais Obama ataomba radhi kwa ushiriki wa Marekani kwenye mauaji wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo Patrice Lumumba. Hivi Tanzania inahangaika zaidi ya uwezo wake kupeleka majeshi huko mashariki ya Kongo kulinda amani. Waafrika wengi tunaamini kuwa mauaji ya Lumumba ilikuwa ni kama laana kwa Taifa lile na hivyo limekuwa ni taifa la vurugu na vita licha ya utajiri mkubwa ulioko nchini humo. Nyaraka za CIA zinaonyesha dhahiri kuwa Rais wa Marekani wa wakati huo Lyndon Johnson aliagiza kuuwawa kwa mwanamapinduzi Patrice Lumumba. Kuwaomba radhi Waafrika na hasa Wakongo kuhusu mauaji ya Lumumba ni jambo litakaloweza kusaidia sana kurejesha amani Kongo.
Karibu Afrika, Karibu Tanzania ndugu Barack Hussein Obama.

Zitto Z Kabwe

Makala haya yanatarajiwa kutoka kwenye gazeti la MWANANCHI, mfululizo wa makala kuhusu ziara ya Obama.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU