NDOA iliyokuwa tayari kufungwa kati ya Hamis Ngaumba (35),
mkazi wa Bangulo, Ulongoni, Gongo la Mboto, Dar na binti wa miaka 14
anayetajwa kwa jina moja la Zubeda, imesambaratishwa na polisi wa Kituo
cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar kutokana na umri wa bi harusi kuwa
mdogo.
Binti wa miaka 14, Zubeda akiwa tayari kufunga ndoa na Hamis (35). |
Mapema siku ya tukio, msamaria mwema ambaye hakupendezwa na kitendo hicho alitoa taarifa kwa mapaparazi ambao nao waliwataarifu polisi wa Kituo cha Polisi Sitaki-Shari na kupewa maafande kutoka dawati linaloshughulikia unyanyasaji wa kijinsia na kuambatana nao hadi eneo la tukio.
Kabla ya kufika eneo la tukio kwanza ilikuwa ni kwa mjumbe wa eneo hilo Shina Namba 10, Erasto Nyakiege ambaye alikiri kusikia taarifa hizo za mtoto kufungishwa ndoa lakini alizipata muda mfupi kabla polisi na waandishi hao kufika eneo hilo.
Hamis Ngaumba (35) aliyetaka kumuoa binti wa miaka 14. |
Mapaparazi, Polisi na Mjumbe
huyo waliambatana hadi kwenye nyumba ambayo ilikuwa na shamra shamra za
ndoa hiyo na kumkuta shehe akijiandaa kufungisha huku waalikwa wakiwa
wameshakaa mkao wa kula pilau.
Mshtuko mkubwa ulitokea eneo la sherehe baada ya watu kuwaona askari, wengine walikimbia kama wanafukuzwa na simba. Bi harusi yeye alikimbilia chumbani huku bwana harusi akijichanganya katikati ya wageni waalikwa lakini polisi walimweka ‘mtukati’.
Akizungumza baada ya kunaswa, Shehe Bakari alisema ndiyo kwanza alikuwa anajiandaa kwa zoezi la kuwafungisha ndoa wawili hao lakini kama angebaini kuwa mtoto huyo ana miaka isiyokidhi vigezo.
Zubeda alisema cha kushangaza siku moja aliwaona wazazi wa kijana huyo wakipeleka barua ya posa na mahari na kumkabidhi mjomba na bibi yake kwani baba yake mzazi anaishi Shinyanga na mama anaishi Tabora, tangu akiwa mdogo anaishi na bibi yake huyo.

“Mimi natamani sana kusoma lakini sina uwezo kwani niliishia darasa la tatu baada ya wazazi wangu kushindwa kunisomesha ndipo bibi akaja kunichukua ndiyo maana suala la kuolewa limenitokea tu bila mwenyewe kupenda. Ilikuwa kama utani lakini wakapokea mahari,” alisema Zubeda huku akilia kwa uchungu.