Facebook Comments Box

Wednesday, March 13, 2013

PAPA MPYA AMEKWISHAPATIKANA

Huu ni moshi mweupe ulio onekana kwenye dohani la Sistine Chapel ikiwa ni ishara ya kuwa papa mpya amekwisha chaguliwa



ULIWAHI FIKIRIA KUWA WEMA SEPETU AKIKATA NYWELE ATAKUWAJE? ANGALIA PICHA HIZI



HII NI BEHIND THE SCENE YA JIMMY GAIT`S MARUNGU




INASEMEKANA HII NDIO BAISKELI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI




VIDEO HII NDIO INAYODAIWA KUWAONESHA CHADEMA WAKIPANGA MAUWAJI




MCHUNGAJI AKAMATWA MKOANI RUKWA KWA TUHUMA YA UCHOCHEZI WA KIDINI

Mchungaji Christopher Mtikila

Polisi mkoani Rukwa imemkamata na kumuhoji mwenyekiti wa chama cha Democtaric Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila kwa tuhuma za uchochezi wa kidini baina ya wakristo na waislam.
Mtikila ambae yupo mkoani Rukwa kwa takribani wiki mbili amekamatwa baada ya kuitisha kongamano la wachungaji na viongozi wa kidini wa kikristo mjini Sumbawanga
Katika kongamano hilo Mtikila anadaiwa alihamasisha uchochezi uliokuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani
Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda anadai kuwa katika kongamano hilo Mtikila aliwaambia wakristo wamekuwa wakionewa na waislam kwa muda mrefu. Na akiwahamasisha wakristo wawavaimie waislam

SOURSE: HABARI LEO

HIKI NDIO KIKOSI CHA STARS KITAKACHO IVAA MOROCCO

KIM PAULSEN
Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Kim Paulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 amabao wataivaa timu ya Taifa ya Morocco. Wachezaji walioitwa kutoka nje ya nchi ni wawili tu ambao wanachezewa TPO Mazembe. Hii ni mechi ya awali kuwania kwenda kucheza kombe la dunia nchini Brazil 
Makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU