Wednesday, July 24, 2013
GONZALO HIGUAIN NA PEPE REINA WANAFANYA VIPIMO VYA AFYA NAPOLI SASA HIVI
Inaonekana Arsenal imepoteza nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa kiargentina Gonzalo Higuain ambaye imemuwania kwa muda mrefu baada ya mshambuliaji kukaribia kujiunga na klabu ya Napoli ya Italia.
Kwa mujibu wa mtandao wa Sky News ni kwamba hivi sasa nchini Italia mshambuliaji Gonzalo Higuain na kipa wa Liverpool Pepe Reina ambaye nae alihusishwa na Arsenal huko nyuma wapo kwenye vipimo vya afya vya kujiunga na klabu ya Napoli.
Kwa mujibu wa mtandao wa Sky News ni kwamba hivi sasa nchini Italia mshambuliaji Gonzalo Higuain na kipa wa Liverpool Pepe Reina ambaye nae alihusishwa na Arsenal huko nyuma wapo kwenye vipimo vya afya vya kujiunga na klabu ya Napoli.
Real
Madrid na Napoli zimekubalina ada ya uhamisho wa Higuain kuwa kiasi cha
£32million na kukubaliana na mchezaji mwenyewe mkataba wa miaka mitano
kwa mshahara wa paundi 140,000 kwa wiki.
AZAM FC KUFANYA ZIARA KAMA YA MANCHESTER CITY
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wana
lambalamba Azam fc wanatarajiwa kuondoka Agosti 2 mwaka huu kuelekea
nchini Afrika kusini kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na michuano
ya ligi kuu soka Tanzania bara na michuano ya kimataifa mwakani ambapo
watakaa kwa wiki mbili.
Afisa
habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga amesema wameamua kufanya ziara
bondeni kwani wao wameendelea zaidi kisoka kwa maana ya kuwa na ligi
bora, timu bora na mfumo wa kisasa wa kuendesha soka, hivyo watajifunza
mambo mengi kutoka kwao.
Jafar
alisema ziara hiyo itakuwa na manufaa makubwa sana kwani watacheza na
klabu kubwa za huko wakiwemo Supersport United na Orland Pirates.
“Malengo
yetu ni kufanya makubwa katika michuano ya kimataifa, lakini Ubingwa wa
ligi kuu ni muhimu sana kwetu. Na ndio maana tunaenda Afrika kusini
kuweka kambi ya wiki mbili”. Alisema Jafar.
Kuhusu
usajili, Jafar alisema wao hawajasajili mchezaji yeyote mpaka sasa na
hawana mpango wa kufanya hivyo kwani kikosi chao kipo kamili gado.
“Timu
yetu ni nzuri sana, kusajili mara kwa mara kunaharibu timu, sisi tuna
wachezaji wengi wakiwemo vijana wetu na ndio maana hatuhangaiki na
usajili”. Alisema Jafar.
Wakati
huo huo shirikisho la soka Tanzania, TFF, limethibitsha kupokea barua
kutoka klabu ya Azam fc kuwa wanatarajia kuondoka nchini kuelekea Afrika
kusini.
Katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema Azam wamefanya vziuri kuwataarifu wao ili waende kwa kibali sahihi.
Subscribe to:
Posts (Atom)