Facebook Comments Box

Friday, November 27, 2015

RAIS AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (T.R.A)


Rais Dk John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania ( TRA) Rished Bade na kumteua Philiph Mpango kukaimu nafasi hiyo.


Taarifa kutoka ikulu zimesema kuwa uamuzi huo wa Rais Magufuli umefuatia ziara ya waziri mkuu bandarini iliyobaini upotevu wa makontena 349.



Aidha Rais Magufuli amemtaka Rished Bade kutoa ushirikiano kwa Philiph Mpango wakati uchunguzi ukiendelea.



RISHED BADE aliyesimamishwa kupisha uchunguzi.
www.facebook.com/eatv.tv


MSHAURI WA RAISI WA BURUNDI ANUSURIKA KIFO

Mshauri wa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amenusurika shambulio alipokuwa akitoka nyumbani kwake katika eneo la Kajaga, magharibi mwa mji mkuu Bujumbura.
Zenon Ndaruvukanye alinusurika bila majeraha yoyote, lakini mlinzi wake, ambaye alikuwa afisa wa polisi, alifariki kutokana na majeraha ya risasi.
Washambulijai walitoroka wakitumia gari aina ya Toyota  Hilux lakini polisi walipashana habari na gari lao likazuiwa maili kadha kutoka Kajaga. Waliacha gari hilo na kutorokea soko lililo karibu, lakini mwishowe wawili walikamatwa. Mmoja wao alifanikiwa kutoroka.

Gari hilo aina ya Toyota Hilux lilipatikana na silaha mbalimbali zikiwemo bunduki aina ya AK47 na guruneti. 
Polisi baadaye walipelekwa kwenye nyumba moja viungani mwa mji wa Bujumbura ambapo walipata silaha zaidi.
Mji wa Bujumbura umekumbwa na machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 200 tangu Aprili.


SOMA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 27-11-2015 HAPA




MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO KUPITIA CHADEMA ANAEWAKILISHA UKAWA SAID KUBENEA AWATEMBELEA WANANCHI WAKE

Kubenea akizungumza na waandishi wa habari na wananchi katika Soko la Ndizi la Mabibo.

Said Kubenea Mbunge wa jimbo la Ubungo, akiongea na wananchi katika Stendi ya Mabasi ya Ubungo Dar es Salaam kuwashukuru kwa kumchagua na kujua changamoto zao mbalimbali. Mbunge huyo alitembelea Soko la Mabibo, Kituo cha Mabasi cha Mawasiliano.
Hapa akiwaunga mkono wananchi kununua mananasi katika soko la ndizi la mabibo.
Vijana wakiserebuka baada ya kuzungumza na mbunge wao Said Kubenea katika Soko la Mabibo.
Said Kubenea akiwahutubia wananchi katika soko la Mabibo.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU