Facebook Comments Box

Wednesday, August 14, 2013

MAHOJIANO MAALUMU NA SHEIKH PONDA

Sheikh Ponda akiwa hospitali Muhimbili (MOI)
 SWALI: Je, watu waliokupa huduma ya kwanza mara baada ya kujeruhiwa walikuta risasi iliyokujeruhi?
JIBU: Nilipigwa risasi kwa nyuma ikatokea mbele kwa hiyo haikubaki mwilini wala haikuonekana ilipoangukia kwa wakati huo maana kulikuwa na purukushani.

SWALI: Ulipata wapi huduma ya kwanza?

JIBU: Kwa kweli kwa sasa siwezi kukumbuka nilihudumiwa wapi kwa sababu mara baada ya kujeruhiwa sikuwa katika hali yangu ya kawaida, nilichanganyikiwa.

SWALI: Utathibitisha vipi kama ulipigwa risasi?

JIBU: Bahati nzuri ni kwamba tukio hili lilitokea kweupe wapo wengi walioshuhudia, kwa hiyo wanaweza kusaidia kuthibitisha na ushahidi mwingine ni jeraha hili.

SWALI: Nini msimamo wako baada ya tukio?

JIBU: Nitaendelea kuzungumzia haki za Waislamu na siwezi kurudi nyuma. Pamoja na kwamba wananiona mimi ni mtu mchochezi lakini wanaeneza chuki dhidi yangu kwa njia wanazojua wao. Nitaendelea, risasi haitaninyamazisha.

SWALI: Umehusishwa kufanya uchochezi Zanzibar, unalizungumzia vipi hilo?

JIBU: Zanzibar nilichozungumza ni kuhusu kesi dhidi ya viongozi wa Kundi la Uamsho. Watu wamewekwa ndani kwa miezi tisa sasa, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, kesi wanayoshtakiwa ina dhamana, sasa nikauliza kwa hao viongozi, kwa nini hawazingatii sheria? Kesi zina muda mrefu hazitolewi uamuzi, nikawasisitiza wazingatie misingi ya sheria kwa kuwa hivyo wanavyowatendea wananchi wajue kwamba hawastahili kupewa tena ridhaa ya kuongoza nchi, nilifikisha ujumbe wangu.

SWALI: Kuna tukio la kumwagiwa tindikali mabinti wawili wa Uingereza lililotokea Zanzibar, ambalo wewe pia unahusishwa, hili unalizungumziaje?

JIBU: Sijaona huo ushahidi ambao wanahangaika kunihusisha na tukio hilo, nahusishwa vipi? Matukio ya kumwagiwa tindikali yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara huko kabla sijakwenda kuhutubia. Vyombo vya dola vifanye kazi yake vyema ili kubaini ukweli wa jambo hili.

Pia Mwananchi ilizungumza na mke wake, Sheikh Ponda, Hadija Ahmad ambaye alikuwa ameketi pembeni ya kitanda alicholazwa mumewe.

SWALI: Unazungumziaje tukio hili la kujeruhiwa kwa mumeo?

JIBU: Hili ni dhumuni la Serikali, lililenga moja kwa moja kumdhuru ili kunyamazisha harakati zake za kutetea wanyonge. Ni tukio la kupangwa, halijatokea bahati mbaya. Serikali inamfuatilia sana hivyo ililenga kumnyamazisha.

Namshauri Rais (Jakaya Kikwete), kuhakikisha kwamba haki za wanyonge zinawafikia, asije akafikiri hili lililotokea kwa Sheikh Ponda ni suluhisho, ni vyema kufanya mazungumzo ili kuweka mabadiliko.

ALIVYOWAPONYOKA POLISI

Mtu wa karibu wa Sheikh Ponda alisimulia jinsi walivyomsafisha kiongozi huyo kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam na kukwepa vizuizi vya polisi ambao walikuwa wakiendelea kumsaka.

“Msafara ulikuwa na magari mawili. Moja lilitumika kwa uangalizi, lingine lilimbeba Sheikh Ponda. Tulipofika Chalinze tulikuta kizuizi tukakikwepa kwa kupitia Msata kisha Bagamoyo hadi Dar es Salaam na kumfikisha Muhimbili,” alisema.

WAIGOMEA POLISI

Msemaji wa familia ya Sheikh huyo, Isihaka Rashid alisema hawaitambui tume iliyoundwa na polisi kwa kuwa jeshi hilo ndilo linalotuhumiwa.

“Tunachofanya hivi sasa ni kukusanya ushahidi wetu, kwa bahati nzuri tayari tumepata mkanda wa tukio lenyewe ambao utatuwezesha kumbaini aliyemshambulia Sheikh Ponda.

“Hatuwezi kuhitaji majibu ya hiyo tume yao na hata leo kuna maofisa wa polisi kutoka Makao Makuu na Kituo cha Kati, Dar es Salaam walifika wakitaka kumhoji eti kuhusu uchochezi lakini alikataa kuzungumza hadi mwanasheria wake awepo, wakaondoka,” alisema Rashid.

CHANZO:MWANANCHI


UCHAGUZI TFF KUFANYIKA OKTOBA 20: KAMATI KUPITIA MAJINA YA USAJILI IJUMAA



 

UCHAGUZI TFF KUFANYIKA OKTOBA 18
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa tangazo la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika Oktoba 20 mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka huu.
Akitangaza mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.
Fomu kwa wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 16 mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 kamili jioni kwenye ofizi za TFF. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti 20 mwaka huu. Fomu kwa nafasi ya Rais ni sh. 500,000, Makamu wa Rais ni sh. 300,000 wakati wajumbe ni sh. 200,000.
Mbwezeleni amesema kwa wale ambao walilipia fomu katika mchakato uliofutwa na wanakusudia kugombea nafasi zilezile walizolipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.
Kwa upande wa uchaguzi wa TPL Board, fomu zitaanza kutolewa Agosti 16 hadi 20 mwaka huu, na nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambapo ada ni sh. 200,000 wakati wajumbe wa Bodi ada ni sh. 100,000.


KAMATI YA SHERIA SASA KUPITIA USAJILI IJUMAA
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji iliyokuwa ikutane jana (Agosti 13 mwaka huu) na leo (Agosti 14 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza sasa itakutana keshokutwa (Agosti 16 mwaka huu) saa 4 asubuhi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Alex Mgongolwa amepanga tarehe hiyo mpya baada ya kikao cha jana kushindwa kupata akidi. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ina wajumbe saba, na ili kikao kiweze kufanyika ni lazima wapatikane wajumbe kuanzia wanne.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


MSHAMBULIAJI WA MPYA WA SIMBA BETRAM MWOMBEKI AWEKEWA PINGAMIZI NA PAMBA

Mshambuliaji aliyetokea kukonga mioyo ya mashabiki wa Simba kwa kufumania nyavu, Betram Mwombeki amekwaa kisiki katika usajili wake kuichezea timu hiyo baada ya kuwekewa pingamizi na klabu yake aliyoichezea msimu uliopita, Pamba ya Mwanza.
Awali iliripotiwa kuwa Mwombeki amesajiliwa na timu hiyo akitokea nchini Marekani, hata hivyo Pamba wamepinga taarifa hizo na kusema kuwa mchezaji huyo aliichezea timu yao Ligi Daraja la Kwanza na kufunga mabao mawili msimu uliopita.
Mwenyekiti wa Pamba, Kazimoto Miraj Muzo aliiambia Mwananchi kuwa Mwombeki alikuwa Marekani miaka ya nyuma na mwaka jana alijiunga na Pamba wakati wa dirisha dogo la usajili na kucheza mechi kadhaa tofauti na taarifa kuwa ametokea Marekani.
Muzo alisema kuwa hakuweza kucheza mechi nyingi kutokana na kukabiliwa na maumivu ya goti. “Si kweli kuwa ametokea Marekani, tupo hapa na aliichezea timu yetu. Tuliwaambia Simba, wakabisha na sasa tutakutana mbele ya sheria,” alisema Muzo.
Alifafanua kuwa walizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are kuhusiana na usajili wa mchezaji huyo, lakini hakuonyesha kujali taarifa hiyo.
“Tumewasilisha vielelezo vyetu TFF, tunasubiri matokeo ya kikao cha Kamati ya Alex Mgongolwa kutoa uamuzi wake, tumedhamiria kupigania haki yetu mpaka mwisho” alisema.
Alisema kuwa kiasi gani cha fedha watakachoidai Simba iwalipe ni siri, kwani daima wao huwa hawapendi kuweka hadharani masuala ya fedha, hasa za kumuuza mchezaji.
Itang’are alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alithibitisha kuongea na Pamba na kuahidi kulifanyia kazi. “Pamba ni ndugu zetu, miaka ya nyuma walitupa wachezaji wengi kama Hussein Marsha, John Makelele, George Masatu, Juma Amir na wengine, na kwa hili sidhani kama tutashindwana,” alisema Itang’are.
Wakati Simba inakabliwa na kikwazo kuhusiana na Mwombeki, Yanga inaelekea kupeta kwa mchezaji, Mrisho Ngassa kutokana na ukweli kuwa Simba hajawasilisha taarifa nyingine zaidi ya mkataba tu.  
SOURCE: MWANANCHI


PICHA: MARIO BALOTELLI NA LIONEL MESSI WAKUTANA NA PAPA


The Hand of God: Messi and Italy captain Gigi Buffon (left) meet the Pope on Tuesday
Golikipa wa Italia Buffon na Lionel Messi wakiwa na Papa Francis Vatican leo wakati wachezaji wa timu ya taifa ya Italia na Argentina ambao wanajiandaa na mchezo wa kirafiki baina yao walipoenda kumtembelea kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani.
All smiles: Balotelli and the Pope share a joke
Papa akiwa na Kichaa Mario Balotelli wakitaniana wakati wachezaji mbalimbali walipoenda kumtembelea mkuu huyo wa kanisa katoliki duniani
Friendly rivalry: Italy take on Argentina on Wednesday night


VIDEO: LAKUCHUMPA - GODZILLA FT JOTI





VIDEO YA DAKTARI AKIMPIGA NGUMI MGONJWA

Daktari mmoja nchini Urusi, Andrey Votyakov (bingwa katika fani ya usingizi) mapema mwezi uliopita alitimuliwa kazi baada ya video ya chumba cha upasuaji inayorekodi matukio (surveillance camera) kuoneshwa hadharani ambapo daktari huyo alionekana akilumbana na mgonjwa aliyefungwa kitandani na baadaye kumshushia makonde usoni na kifuani, upande wa kushoto.

Mgonjwa huyo aliyekuwa katika kitendo cha magonjwa ya moyo, alikuwa wa umri wa makamo (miaka 45) na alifariki muda mfupi baadaye.

Tukio hilo lilitoea mwezi Februari mwaka huu lakini liligundulika mwezi Julai.

Daktari huyo ambaye hakuwa na rekodi yoyote mbaya kazini, alijitetea kuwa alipandwa na jazba baada ya mgonjwa kumsemea maneno yaliyomuudhi na kujikuta amempiga. Vile vile alisema uchovu uliotokana na kufanya kazi mfululizo kwa saa 24, ulichangia kushindwa kwake kufanya maamuzi yenye busara.


CHANZO: WAVUTI



MWANAFUNZI WA MARANGU SEKONDARI ABAKWA HOTELINI KWA SIKU NNE MFULULIZO

MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Marangu inayomilikiwa na kanisa Katoliki jimbo la Moshi, (jina limehifadhiwa) alitekwa na kukufungiwa kwenye hoteli moja ya kitalii mjini hapa na kufanyiwa vitendo vya ngono kwa muda wa siku nne mfululizo.

Mwanafunzi huyo anadaiwa kutekwa Agosti 6 mwaka huu na kijana mmoja (jina linahifadhiwa) mfanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi (Airtel) mjini Dodoma.

Akizungumza jana na Tanzania Daima Jumatano, kaka wa mwanafunzi huyo, Joseph Temba, alidai mdogo wake alitekwa na mtu huyo na tayari mtuhumiwa ameshakamatwa.

Alisema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Agosti 10, mwaka huu, katika baa moja akiwa na mdogo wake baada ya raia wema kutoa taarifa za kuonekana kwake.

Kwa mujibu wa kaka wa mwanfunzi huyo siku ya tukio alipokea simu kutoka kwa mwangalizi wa wanafunzi (matroni) akimjulisha kutokuwapo bwenini kwa mdogo wake na ndipo walipoanza kufuatilia na kutoa taarifa 
kituo kikuu cha polisi mjini Moshi na kupewa namba Mos/RB/9196/2013.

Alisema siku iliyofuata ya Agosti saba jioni walipokea simu kutoka kwa watu wa karibu wakiwataarifu kuwapo katika hoteli hiyo mdogo wake lakini baada ya kufika walinyimwa kuona kitabu cha wageni ili kuangalia orodha ya majina ya wageni waliofikia hapo ili kujiridhisha kama mtuhumiwa huyo alikuwapo mahali hapo.

Hata hivyo alisema jioni ya Agosti 10 walipokea taarifa za kuonekana kwenye baa hiyo mtuhumiwa akiwa na mdogo wake na kuwajulisha polisi na hatimaye kufanikiwa kumtia mbaroni ambapo hadi sasa bado anahojiwa na jeshi la polisi.

Chanzo cha kutekwa kwa mwanafunzi huyo ni mawasiliano ya simu baina ya mtekaji na mwanafunzi huyo ambapo inadaiwa mtuhumiwa huyo alimrubuni mwafunzi huyo kuacha masomo na kwamba angemtafutia nafasi kwenye shule kubwa za kimataifa.

Inadaiwa kwamba mwanfunzi huyo alikubaliana na propaganda hiyo na kutoka shuleni jioni ya Agosti 6 na kumfuata mtuhumiwa kwenye gari lake na kwenda naye hadi Moshi mjini umbali wa kilomteta 50 kutoka shule ya sekondari Marangu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alisema hana taarifa za kutekwa kwa mwanafunzi huyo kwa kile alichodai alikuwa ametingwa na majukumu ya kikazi mjini Arusha na kuahidi kulifuatilia baadaye.

Charles Ndagulla, 
TANZANIA DAIMA, Moshi.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU