Monday, August 29, 2016
VITUO VIWILI VYA REDIO VYAFUNGIWA KWA MUDA USIO JULIKANA LEO
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amezifungia radio mbili kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi ambavyo vimerushwa hewani vikiashiria uchochezi.
Nape amesema kuwa uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa baada ya kujirdhisha kuwa kipindi cha Matukio kilichorushwa Agosti 25, 2016 muda wa saa 2 usiku hadi saa 3 na Radio 5 pamoja na kipindi cha Morning Magic katika kipengele cha Kupaka Rangi Agosti 17 vilikuwa na maudhui ya uchochezi ambao ungeweza kuleta uvunjifu wa Amani.
Amesema kuwa kufuatia tukio hilo amevifungia viyuo hivyo kwa muda usiojulikana kwani wamekiuka masharti ya kanuni ya 5 (a,b,c na d), kanuni ya 6(2a, b na c) na kanuni ya 218 ya huduma za utangazaji ya mwaka 2005.
PROF. LIPUMBA NA MAGDALENA SAKAYA WAVULIWA UANACHAMA CUF
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Prof. Haruna Lipumba
Chama Cha
Wananchi (CUF) kimewasimamisha uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama
hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa
Bara, Magdalena Sakaya.
Uamuzi
huo umetolewa jana na Baraza Kuu la Chama hicho lililofanya mkutano wake
visiwani Zanzibar kwa lengo la kuwajadili wanachama kadhaa wakiwemo
vigogo hao. Sakaya amevuliwa nyadhifa zote ndani ya chama kabla ya
kusimamishwa.
Taarifa
kutoka ndani ya Mkutano huo zimeeleza kuwa Baraza hilo limewaadhibu
wanachama 15 wakiwemo Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua.
Mbali na
vigogo hao, wengine waliopigwa rungu na Baraza Kuu la CUF ni pamoja na
Katibu wa Baraza la Wazee, Shashi Lugeye, Thomas Malima na Naibu
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano, Abdul Kambaya.
Aidha,
Baraza hilo limemsimamisha uanachama Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah
Nachuma. Hatua hii inaweka matatani ubunge wa Sakaya na Nachuma kwani
wakifikia hatua ya kufukuzwa watakosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.
Lipumba
na Sakaya hawakupata nafasi ya kujitetea kutokana na kutohudhuria
mkutano huo wakati Shashi alipata nafasi ya kujitetea kutokana na uwepo
wake lakini utetezi wake haukuzaa matunda. Katiba ya chama hicho haiwapi
nafasi wabunge hao kukata rufaa kutokana na uamuzi wa Baraza hilo.
Uamuzi
huo umekuja ikiwa ni siku chacha baada ya Mkutano Mkuu Maalum wa Chama
hicho uliolenga kumchagua Mwenyekiti Mpya kuvunjika kutokana na kuwepo
vurugu kubwa baada ya Profesa Lipumba kuingia ndani ya ukumbi huo na
wafuasi wake wakitaka barua yake ya kutaka kurejea kwenye nafasi yake
ijadiliwe na kukubaliwa.
KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA STARS KITAKACHO SAFIRI KWENDA KUIVAA NIGERIA HIKI HAPA
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’,
Charles Boniface Mkwasa, ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi
kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya
mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.
Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa
kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini
utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G
ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo
iliyojitoa katikati ya mashindano.
“Tanzania hatuwezi kuupuuza mchezo huu, tunaupa umakini kabisa kwa sababu tunacheza ugenini ambako matokeo mazuri
yanaweza kutusongesha mbele na kuingia ndani ya timu 99 bora katika
viwango vya FIFA,” amesema Mkwasa.
Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza kutomjumuisha Mshambuliaji wa
Kimataifa, Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo
kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye aliumia katika mchezo wa kuwania
Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
“Timu ilitarajiwa kuingia kambini Agosti 28 siku ya Jumapili, mchezo huo ni wa kukamilisha ratiba ambapo Misri tayari
wameshafuzu fainali za Afrika,” alisema Mkwasa na kuongeza kuwa kuna
mchezaji wa Tanzania, Said Carte Mhando anamfuatilia ili ikiwezekana
baadaye amwite kuchezea timu ya Taifa. Anachezea Klabu ya Brencia Calcio
ya Italia.
Wachezaji walioitwa:
Makipa; Deogratius Munishi (Young Africans) na Aishi Manula (Azam FC)
Mabeki
Kelvin Yondani (Young Africans),Vicent Andrew (Young Africans)
Mwinyi Haji (Young Africans),Mohamed Hussein (Simba SC)
Shomari Kapombe (Azam FC) na David Mwantika (Azam FC)
Viungo
Himid Mao (Azam FC),Shiza Kichuya (Simba SC),Ibrahim Jeba (Mtibwa Sugar),Jonas Mkude (Simba SC),Muzamiru Yassin (Simba SC),Juma Mahadhi (Young Africans) na Farid Mussa (Tenerif ya Hispania)
Washambuliaji
Simon Msuva (Young Africans),Jamal Mnyate (Simba SC),Ibrahim Ajib (Simba SC),John Bocco (Azam FC) na Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji
Subscribe to:
Posts (Atom)