Facebook Comments Box

Sunday, May 5, 2013

TAARIFA YA CCM KWA UMMA KUHUSU CHADEMA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Picture
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Ijumaa iliyopita Mei 3, 2013 Msemaji wa kambi ya Upinzani Bungeni Masuala ya katiba na Sheria Ndg. Tundu Lissu katika hotuba yake pamoja na kuzishutumu taasisi zingine, lakini pia alitoa tuhuma kadhaa dhidi ya CCM.

Tuhuma hizo zilielekezwa kwenye maeneo kadhaa hasa yahusuyo suala la mchakato wa uundwaji wa katiba mpya unaoendelea nchini na ushiriki wa makundi tofauti katika mchakato huo.

Katika kuipa uzito hoja hiyo, Lissu alitoa malalamiko mengi dhidi ya CCM kwa madai kuwa tumeteka mchakato huo kwa kujaza Makada wa CCM katika Mabaraza ya Katiba yaliyoundwa kwenye ngazi ya kata hivi karibuni.

CCM Kama ilivyo taasisi yoyote makini na wenye uzalendo  kwa nchi yao, katika mchakato wa uundwaji wa katiba mpya ina jukumu la kuwahamasisha wanachama na wasio wanachama wake kushiriki mchakato wa katiba nchini kutokana na kutambua umuhimu wake.

Tofauti ya CCM na Chadema katika hili ni,  wakati CCM tunahamasisha watu washiriki kwenye mchakato wa katiba nchini, Chadema wao wanahamasisha watu wavuruge au wasishiriki kabisa mchakato huu.

Mfano mzuri ni jitihada zao za kuziria mchakato huu kwa visingizio vya kitoto kabisa. Juhudi zao za kumtaka Prof. Baregu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ambaye wao Chadema walimpendekeza kwenye tume, ajitoe kwenye tume zinafahamika na wala sio SIRI.

CCM inampongeza kwa dhati Prof. Baregu kwa uzalendo na ukomavu wa kisiasa aliouonyesha kwa kuwakatalia kujitoa kwenye tume na kuweka mbele masilahi ya taifa lake. Kukataa kwa Prof. Baregu kujitoa kwenye tume kwa hoja za kitoto kabisa za Chadema ilipaswa kuwa fundisho kwa vibaraka hawa.

Ilivyo fanya CCM, kuhamasisha wanachama na watanzania kwa ujumla kushiriki mchakato huo, ndivyo taasisi nyingine pia zilivyofanya. Zikiwemo taasisi za dini ambazo zimekuwa zikihamasisha zoezi hili kupitia mikusanyiko ya Ibada, Taasisi zisizo za Kiserikali yaani NGOs kwa kufanya makongamano na makundi mengine kwa kuendesha midahalo, dhambi kwa CCM inatoka wapi?.

Ifahamike kuwa mawasiliano na mjadala juu ya zoezi la mchakato wa uundwaji wa katiba mpya nchini hayakuanza jana ndani ya CCM, bali yalianza siku nyingi kwa  Chama kuunda kamati   iliyopitia na kuja na maoni ya CCM juu ya nini kiwemo kwenye katiba mpya.

Taarifa hiyo  haikufanywa Siri. Iliwasilishwa mbele ya vikao kadhaa vya Chama na kisha kutangazwa kwa umma. Hivyo hoja kwamba mawasiliano ndani ya Chama juu ya mchakato huo wa Katiba nchini umelenga kuhujumu mchakato huo hayana maana yoyote, badala yake hoja hiyo imebeba mtazamo finyu wa wanasiasa wenye tabia za nguruwe za kula watoto wake mwenyewe pindi apatapo njaa.

Chadema ni kama nguruwe ambaye huweza kuzaa watoto wake kisha akishikwa njaa huanza kuwala watoto wake mwenyewe. Mchakato wa katiba nchini ni matunda ya viongozi wa CCM akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM Taifa, kutangaza kuanza kwa mchakato huu. Hatuwezi kuuzaa wenyewe mchakato halafu tukauhujumu wenyewe mchakato huo.

Itakumbukwa umezuka utamaduni mbaya kwa baadhi ya Wabunge wa CHADEMA kutumia Bunge kama jukwaa la kuwashambulia isivyo sawa watu ambao hawana fursa ya kuingia Bungeni kujibu mashambulizi hayo. Utamaduni huu ni wa hovyo unakiuka haki za msingi ambazo zinataka mtu anayetuhumiwa/kushutumiwa apewe fursa ya kusikilizwa. Watanzania lazima tuukatae utamaduni huu.

Hivi karibuni baadhi ya Wabunge wa CHADEMA wamefanya vitendo vya aibu vilivyowakera sana Watanzania. Hili bado limo kwenye akili na midomo ya watu na  sasa Chadema wanatafuta namna ya kuficha aibu yao(nitoke vipi) kwa kurukia hoja ya Mabaraza, kuzusha na kushutumu watu kwa uongo uliokubuhu.

Vituko vyote hivi vya Chadema vimeongezeka baada ya katibu mkuu wa CCM hivi karibuni mjini Morogoro kutoa maelezo ya kina na hoja nzito dhidi ya ukibaraka wa Chadema kwenye suala zima la mchakato wa Katiba.

Nchi nyingi hasa za Afrika zilizokumbwa na machafuko moja ya ajenda kubwa ilikuwa ni swala la katiba mpya. Sasa hapa nchini Chadema wanaona watanzania wanaendelea na mchakato bila machafuko wanakosa majibu kwa mabeberu wanaowafadhili kuchafua nchi yetu, ndio maana kila kukicha wanakuja na visa na vituko kusumbua mchakato wa katiba.

Walianza kwa kukataa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ikiwemo kutomtambua rais. Wakatangaza hadharani nchi haitatawalika kisa wamenyimwa ridhaa na watanzania. Mchakato ulipoanza wa katiba mpya wabunge wao wakazira na kutoka nje ya bunge, baada ya muda wakarudi.

Juzi bungeni wametishia kujitoa kwenye mchakato wa katiba ifikapo tarehe 30/04/2013, leo ni tarehe 05/05/2013!! Wamezoea kutishia nyau, tumechoka na vitisho vya vibaraka hawa. Tunapongeza msimamo wa Tume ya mabadiliko ya Katiba kwa kupuuza hoja ya kufuta mabaraza ya katiba. Chadema wakisusa na wasuse tu.

Tunawasihi watanzania wote wapuuze utoto na ukibaraka huu wa Chadema kwani ugonjwa wao tumesha ufahamu WANAUMWA KIFAFA CHA SIASA. Kila ugonjwa huu ukipanda wanatupa mateke sana. Tuwaombee ipo siku huenda mwenyezi Mungu atawarehemu watapona.

Mwisho

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Ideology and Publicity Secretary



AZAM WAKUBALI KUTOLEWA NA AS FAR RABAT YA MOROCCO


 
 
SOKA ni mchezo wa bahati wakati mwingine. Naam sadakta, usemi huo umedhihirika jana kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah baada ya Azam kulala 2-1 mbele ya wenyeji AS FAR Rabat na kutolewa katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika, licha ya kupata nafasi nzuri ya kusonga mbele dakika ya 81. “Tumekosa penalti dakika ya 81, siwezi kumlaumu refa ikiwa tumekosa penalti zimebaki dakika tisa,” alisema kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall baada ya mchezo.

Azam ilihitaji sare yoyote ya mabao ifuzu na ilikaribia kuipata dakika ya 81 ilipopata penalti ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, lakini fundi wa upigaji wa michomo hiyo, John Raphael Bocco alikwenda kugongesha mwamba mpira huo.

SOURCE:AZAM FC BLOG


LIVE MATCH CENTRE: RUVU SHOOTING 1 - 3 SIMBA SC

Dk 90+3 FULL TIME! RUVU 1-3 SIMBA

Dk 90 Ruvu wamepotea na Simba wanatawala tena kiungo. Dakika tatu zimeongezwa.

Dk 88 GOOOO....! Ismail Mkoko anaipatia Simba bao la tatu kwa kichwa akiunga krosi ya Kiemba. Ruvu 1-3 Simba.

Dk 86 GOOOOO....! Edward Christopher anaifungia Simba bao la pili akimalizia mpira uliotemwa na kipa Haule. Ruvu 1-2 Simba.

Dk 82 Simba wanafanya mabadiliko ametoka Haruna Chanongo ameingia Ismail Mkoko.

Dk 81 Ruvu wanafanya mabadiliko ametoka Said Madega ameingia Hamis Kisuke.

Dk 80 Kipa wa Ruvu, Haule anaumia na kutibiwa kwa muda.

Dk 74 Ngassa anachezewa faulo nje kidogo ya lango la Ruvu.

Dk 70 Simba imefanya mabadiliko ametoka Messi ameingia Edward Christopher.

Dk 64 Kulwa Mfaume anapiga shuti kali linalotoka nje kidogo ya lango la Simba.

Dk 59 YELLOW CARD...! Ngassa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kuutumbukiza mpira wavuni baada ya filimbi ya kuotea kupulizwa.

Dk 55 Ruvu wamefanya mabadiliko wametoka Said Dilunga na Raphael Keyala na wameingia Kulwa Mfaume na Ayoub Kitala. Ruvu 1-1 Simba


Dk 52 GOOOOO.....! Abdulhaman Mussa anaifungia Ruvu bao la kwanza baada ya kuichambua ngome ya Simba. Ruvu 1-1 Simba.

Dk 51 YELLOW CARD....! Ernest Ernest wa Ruvu anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Messi wa Simba.
 
Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!

Dk 45 HALF TIME! Ruvu 0-1 Simba  
Dk 44 YELLOW CARD....! Said Madega wa Ruvu anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Abdallah Seseme. Ruvu 0-1 Simba

Dk 42 Simba inaendelea kutawala kiungo

Dk 40 Simba inapata karibu na lango la Ruvu wanapiga lakini kipa Haule anaudaka mpira. Ruvu 0-1 Simba

Dk 36 Ruvu wamepunguza kasi yao waliyoanza nayo na kutoa nafasi kwa Simba kutawala mchezo.

DK 35: Simba SC 1 - 0 Ruvu Shooting

 Dk 34 Haruna Chanongo anakosa bao baada ya mpira aliopiga kuokolewa na kipa Haule na kuwa kona.

Dk 29 Sunzu anakosa bao la wazi akishindwa kuunga krosi ya Nassor Masoud 'Chollo'.

Dk 21 Felix Sunzu anakosa bao la wazi baada ya kichwa alichopiga kuunga krosi ya Kiemba kugonga mwamba wa juu na kutoka nje ya uwanja.

Dk 18 Ruvu wanapata kona. Said Dilunga anashindwa kuunganisha mpira wa kona na kipa wa Simba, Abel Dhaira anaudaka.

Dk 14 GOOOOO......! Amri Kiemba anaipatia Simba bao la kwanza kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la hatari. Kiemba aliuwahi mpira uliopokonywa na Felix Sunzu kutoka kwa beki wa Ruvu, Nyambiso Athuman. Ruvu 0-1 Simba.

Dk 12 Idadi ya mashabiki waliojitokeza katika uwanja huu wa taifa ni ndogo mno.

Dk 10 Bado mpira unachezwa taratibu mno huku kila timu ikimsoma mwenzake.

DK 5:Simba SC 0 - 0 Ruvu Shooting

Mpira umeanza uwanja wa Taifa - Simba SC vs Ruvu Shooting

Simba line up: Abel Dhaira, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Haruna Chanongo, Abdallah Seseme, Felix Sunzu, Amri Kiemba na Ramadhan Singano 'Messi'.

Line up: Ruvu Shooting; Benjamini Haule, Michael Pius, Baraka Nyakamande, Nyambiso Athuman, Shaban Suzan, Ernest Ernest, Said Madega, Hassan Dilunga, Abdulhaman Mussa, Said Dilunga na Raphael Keyala.


KWA WALE JAMAA WA HAMSINI HII MOVIE YA SNAKE IN THE MONKEY`S SHADOW MNAIKUMBUKA?




PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO LA KANISA KUPIGWA BOMU ARUSHA LEO

Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka
Majeruhi wa tukio hilo wakiwa ndani ya gari wakipelekwa hospitali
Umati wa  wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo.
 Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali
wananchi wakiwa katika eneo la tukio
Polisi waki imarisha doria eneo la tukio   baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali kupatiwa matibabu zaidi ...Mpaka tunaondoka eneo la tukio Viongozi mbali mbali akiwemo mmbunge wa arusha walikuwemo eneo hilo



ANGALIA MOVIES MPYA ZINAZOKUJA








UPDATES ZA KANISA LILILOLIPULIWA LEO ARUSHA

 DSCN2226
DSCN2228Ulinzi ukiimarishwa eneo ulipotokea mlipuko huo na kujeruhi makumi ya waumini

Mkuu wa Mkoa Mulongo naye  amefika  eneo  la  tukio  na  kuwafariji  wahanga  wa  tukio  la  bomu....

RPC  wa  mkoa  wa  Arusha  naye aliambatana  na  mkuu  wa  mkoa  na  muda  huu  alikuwa  anatoa  nasaha  zake  kwa  wananchi....
RPC  amesema  tukio  hili  ni  la kigaidi. Amesema kuwa  aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu. ...
Amesema kuwa Polisi wanawasaka waliohusika  na  unyama  huu  na  ameomba yeyote  mwenye taarifa yoyote aisaide polisi. ..
Waliojeruhiwa ni 50 .Hao wana majeraha ya kawaida  na 3 wako  mahututi
Mpaka sasa  mtu mmoja anashikiliwa  na  polisi kwa mahojiano  zaidi


 INASEMEKANA KUWA BOMU LIMELIPUKA KATIKA KANISA KATOLIKI PAROKIA MPYA YA OLASITI ILIYOKUWA INAZINDULIWA LEO JIJINI ARUSHA MUDA HUU. BOMU HILO LIMELIPUKA WAKATI WAUMINI WA KANISA HILO LA KATOLIKI WAKIENDELEA NA SHEREHE ZA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA  NA MPAKA SASA  HAIJAWEZA KUJULIKANA IDADI KAMILI YA WATU WALIOJERUHIWA LAKINI TAARIFA ZINASEMA KUWA KUNA BAADHI YA WATU WAMEJERUHIWA NA KUWAHISHWA HOSPITALI KWAAJILI YA MATIBABU NA MPAKA MUDA HUU HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA BOMU HILO KULIPUKA.

Mh Zitto Kabwe alizungumzia hilo katika ukuta wake wa facebook



VIDEO: ANGALIA MAGOLI YA F.A.R RABAT NA AZAM YALIVYOFUNGWA




WALE WATU WANGU WA LIVERPOOL HIZI NDIO JEZI MTAKAZO TUMIA MSIMU UJAO 2013/2014

Liverpool Home Shirt 2013-14

Liverpool Away Third Shirt 2013-14



New Liverpool Shirts 2013-14



HIZI NI TWEET ZA KIKUNDI CHA M23 KWA MH BERNARD MEMBE



Picture
Picture


PRECISION AIR YAWAHAKIKISHIA WATEJA WAKE NDEGE ZAKE ZITAENDELEA KUTUA ZANZIBAR

Picture
Picture


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU