Facebook Comments Box

Sunday, June 2, 2013

HUKU MWILI WA NGWEA UKITARAJIWA KUWASILI JUMANNE, MIRAJI KIKWETE ATOA FULANA ZA MSIBA

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Bi Radhia Msuya, akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa Baba Mdogo wa Marehemu Mangwea, Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam leo.

MAMA YAKE 'NGWEA' ADONDOKA GHAFLA NA KULAZWA HOSPITALI


            Bi Denisia Mangwea.mama mzazi wa msanii Albart Mangwea
 
 Mama mzazi wa  marehemu Albart Keneth Mangwea 'NGWEA' Bi Denisia Mangwea[63] leo asubuhi ameanguka ghafla baada ya kupokea taarifa kwamba mwili wa mtoto wake Albeth umeshindwa kuwasili nchini ukitokea Afrika ya kusini.Mtandao huu leo mchana ulipokea taarifa z a tukio hilo  ambapo dada mkubwa wa Albeth Bi Magreth Mangwea alipoulizwa alithibitisha mama yake kuanguka ghafla baada ya kusikia mwili wa mpendwa mtoto wake umeshindwa kuwasili  nchini.
 
" Ni kweli leo asubuhi mama alipoamka na kusikia taarifa kuwa mwili wa mwanae hautofika tena leo Jijini Dar es Salaam kutokana na Taarifa ya Daktari kuchelewa kutolewa  alianguka kwa presha na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro akiendelea na matibabu, na alizinduka baadae  na anaendelea vizuri na kwamba muda wowote anaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.



SHEIKH PONDA ISSA PONDA AUNGURUMA HUKU AKIWASIHI WAISLAMU KUWA NA UMOJA


Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye Kongamano lililofanyika leo jijini Dar es Saalaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa na masheikh. Msimamo wa waisilamu juu ya Maendeleo ya mchakato wa katiba mpya, Dhulma na uonevu dhidi ya waislam pamoja na hatua za kuchukuwa kama madai yao yatapuuzwa.      

Imamu wa Msikiti wa Mtambani Imam Suleiman akimkaribisha Sheikh Ponda kuhutubia waislam kwenye Kongamano hilo.
Takbirrr zikafuatia baada ya kukaribishwa Sheikh Ponda.
Sheikh Konda Juma Bungo nae aliwasilisha mada.
Sheikh Ponda Issa Ponda  (kushoto) akihutubia waislam kwenye kongamano hilo.
Sheikh Ally Basaleh nae hakusita kuwasilisha mada kama anavyoonekana pichani.
Amiri wa Jumuia na Taasisi za Kiislam Tanzania Sheikh Musa Kundecha nae aliwaambia waislam kuwa kwa kawaida mtu akilala ukimwamsha huamka lakini ukimwona amelala una mwamsha na haamki basi ujue hajalala ila anajifanya amelala dawayake ni kumkera mpaka aamke.
Jopo la Masheikh wa Meza kuu
Waumini wa dini ya Kiislam leo wametoa msimamo juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini wakati wa kongamano lililoandaliwa na jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania jijini Dar es Salaam.
Kwenye kongamano hilo ambalo masheikh mbalimbali wakiwemo Sheikh Ponda Issa Ponda, Ally Basaleh, Mussa Kundecha na Kondo Juma Bungo waliwasilisha mada mbalimbali pamoja na kutangaza maazimio ya kongamano hilo.
Moja ya mambo yaliyozungumzwa ni mapendekezo waliyowasilisha kwenye Tume ya katiba mpya ambapo walisema iwapo mapendekezo waliyowasilishwa hayakuzingatiwa na kutupwa yote basi waisilamu watatangaza kusimamisha mchakato huo nchi nzima na kufanya maandamano usiku na mchana.
Hoja hiyo ilikuja baada ya kunukuliwa kauli ya Waziri wa nchi Sera na Uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi, wakati akijibu swali la Mbunge Asumta Mshama aliyetaka kujua kwamba lini serikali itaacha kupanga siku ya kupiga kura kuwa Jumapili wakati wanajua siku hiyo ni siku ya ibada ya wakristo haioni inawadhulumu hakiyao yakufanya ibada?, Lukuvi kwenye jibu lake alisema suala hilo limekuwa likilalamikiwa na watu wengi tu lakini serikali kwenye hilo haina utaratibu maalum wa siku ya kupiga kura ila kwakuwa kuna mchakato wa katiba mpya hilo litazingatiwa.
“Hii ni kinyume kabisa na utaratibu wa tume ya katiba waziri huyu anataka tuamini kwamba  anayafahamu yatakayokuwemo kwenye katiba mpya kabla hata wananchi hawajapelekewa na hata haijaandikwa? Hivyo iweje waislam wanaodai siku ya ijumaa iwe ya mapumziko kwa miaka nenda rudi hawapewi wakristo wanakosa sikumoja tu ndani ya miaka mitano majibu yanapatikana kirahisi?” Alihoji sheikh Ponda.
“Waislam wamekuwa wakiomba ruhusa kwa mabosi wao siku ya ijumaa kwenda kufanya ibada na mara nyingine wananyimwa ruhusa hiyo lakini hakuna vurugu yeyote waliofanya na wanadai haki hiyo kwa miaka yote hii lakini hawapewi lakini wengine wanadai kirahisi na kujibiwa kwa uhakika.” Alifafanua.
Aidha heikh Ponda alifafanua kuwa waislam wavumilie wasubiri rasimu itakapotangazwa kwenye magazeti ya serikali kama mapendekezo waliyowasilishwa yatapuuzwa basi hakuna katiba mpya maandamano usiku na mchana mpaka kieleweke nchi nzima.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU