Saturday, July 13, 2013
KIIZA ATUA LEO JIONI KUSAINI YANGA MIAKA MIWILI
MSHAMBULIAJI
 wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego wa Kampala’ anatua 
Alasiri ya leo Dar es Salaam na ndege ya KQ tayari kusaini Mkataba wa 
kuendelea kuitumikia Yanga SC kwa miaka mingine miwili. 
Hiyo
 inafuatia mpachika mabao huyo kufikia makubaliano na Yanga juu ya dau 
la usajili, baada ya awali kushindana hadi akarejea kwao, Kampala na 
ikaripotiwa alikuwa karibuni kusaini URA ya kwao.
Mfanyabiashara
 mwenye jina mjini, Mussa Katabaro alikwea pipa hadi Uganda wiki mbili 
zilizopita kufanya mazungumzo ya kina na Kiiza ili abaki Yanga na 
hatimaye akakubali kuendelea kuvaa jezi za kijani na njano kwa miaka 
mingine miwili.
Katabaro
 ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC na mmoja wa Wajumbe 
wa Kamati ya Mashindano, chini ya Mwenyekiti Abdallah Bin Kleb ameiambia
 BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba Kiiza anatua na ndege ya shirika la 
Kenya, KQ Alasiri.
Katabaro
 alipokuwa Kampala katika mazungumzo yake na Diego walikubaliana 
kumuongezea Mkataba wa miaka miwili kwa dau la dola za Kimarekani 40,000
 na mshahara wa dola 1,500 kwa mwezi.
Lakini
 Katabaro akaomba Kiiza akubali kuchukua dola 20,000 kwa sasa na dola 
20,000 nyingine atampa katika mwanzo wa mwaka wa pili wa Mkataba wake. 
Kiiza akasema anataka dola 40,000 kamili kwa sababu ana kitu anataka 
kufanya na ndiyo maana alikataa kupokea dola 35,000 na gari, ilia pate 
fedha kamili.
URA  ilikuwa tayari kumsaini Kiiza kwa mshahara wa dola 1,000 na dau la usajili dola 40,000 kama ambazo ameahidiwa Jangwani.
Awali, Kiiza aligoma kusaini Yanga kutokana na kulazimishwa achukue dola 35,000 na dola 5,000 nyingine apewe gari.
![]()  | 
| Anarudi; Hamisi Kiiza anatua leo | 
HIVI NDIVYO CHADEMA WATAKAVYO TOA MSIMAMO WAO KUHUSU KATIBA MPYA LEO
Msimamo wetu kuhusu rasimu ya katiba mpya na mustakabali wa taifa 
utatolewa leo Jumamosi ya Julai 13, 2013 kwenye mkutano wa hadhara 
katika viwanja vya Shule ya Ukombozi-Manzese kuanzia saa 8 mchana.
Hotuba zitatolewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Dk.W.Slaa, T.Lissu, M.Marando nk nathibitisha nami nitakuwapo kuwakaribisha Jimboni Ubungo.
Wananchi wote mnakaribishwa. Njoo wewe, njoo na yule!
Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli!
Muhimu:
Hotuba zitatolewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Dk.W.Slaa, T.Lissu, M.Marando nk nathibitisha nami nitakuwapo kuwakaribisha Jimboni Ubungo.
Wananchi wote mnakaribishwa. Njoo wewe, njoo na yule!
Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli!
Muhimu:
- Shule ipo jirani na Manzese TipTop.
 - Maelekezo wasiliana na M/Kiti wa Kata ya Manzese, Ali Makwilo 0784-691449 au 0715-691449 au 0769-658593
 
---
Taarifa hii imetolewa na:
John Mnyika (Mb)
Jumamosi, Julai 13, 2013
KIJANA WISEMAN LUVANDA ATEMBEA KWA MIGUU KUTOKA MBEYA MPAKA DAR ES SALAAM
![]()  | 
| Wiseman Luvanda (23) akiwasili jijini Dar es Salaam alitokea Mbeya kwa miguu.Akiwa anaiunga mkono Timu ya Taifa | 
![]()  | 
| Watu wakimpokea kwa shangwe kijana aliye onesha uzalendo wa hali ya juu | 
Kijana Wiseman Luvanda(23) akikamilisha safari yake ya kutoka Mbeya hadi Dar kwa miguu! Kauli mbiu yake ni "Tanzania nchi yangu,Taifa Stars Timu yangu, Amka wakati wa Uzalendo ni Sasa". Tumefanya nn kuienzi nchi?
SIMBA YAMSAJILI HAMISI TAMBWE

Klabu
 ya Simba ya Dar es Salaam imefanikiwa kumsajili mfungaji bora wa 
michuano ya Kagame Cup 2013 Hamis Tambwe kutokea Vital O ya Burundi.
Tambwe ambaye pia alikuwa akiwania na mabingwa wa Tanzania bara Yanga, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba.

Tambwe amesaini mkataba huo mbele ya mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba. 
Subscribe to:
Comments (Atom)



