Sunday, September 1, 2013
PICHA: LIVERPOOL WATOA KIPIGO KWA MANCHESTER UNITED; ARSENAL WATOA KIPIGO KWA TOTTENHAM
David Beckham na watoto wake Cruz, Romeo na Brooklyn wakiangalia Arsenal wakitoa kipondo
|
Olivier Giroud akishangilia baada ya kutupia goli la kwanza dakika ya 22 |
Wojciech Szczesny akishangilia goli |
Olivier Giloud akifunga goli mbele ya walinzi wa Tottenham |
Santi Cazorla akimtoka Paulinho |
Kocha wa Tottenham akitoa maelekezo kwa wachezaji wake |
Etienne Capoue akitolewa nje baada ya kuumia kifundo cha mguu. Mechi hiyo iliisha kwa Tottenham kufungwa goli moja na Arsenal |
BAO pekee la Daniel Sturridge limeipa
Liverpool ushindi wa tatu mfululizo katika Ligi Kuu ya England, baada ya
kuwalaza wapinzani wao wa jadi, Manchester United 1-0 jioni hii Uwanja
wa Anfield.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka
24 alikuwa katika sehemu mwafaka na kwa wakati mwafaka wakati
anaunganishia nyavuni mpira wa kona dakika ya nne.
Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Sturridge
katika msimu huu na linaipa ushindi wa tatu mfululizo wa 1-0 timu ya
Brendan Rodgers kuendeleza redeki ya ushindi asilimia 100 katika mbio za
ubingwa.
Philippe Coutinho wa Liverpool alikuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet;
Johnson/Wisdom dk78, Agger, Skrtel, Enrique, Henderson, Lucas, Gerrard,
Aspas/Sterling dk60, Sturridge na Coutinho/Alberto dk84.
Man United: De Gea, Jones/Valencia dk37,
Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Cleverley/Young/Nani dk62, Welbeck,
Giggs/Hernandez dk75 na Van Persie.
Tatu: Liverpool imepata ushindi wa tatu mfululizo katika Ligi Kuu ya England, baada ya kuifunga Manchester United 1-0 Anfield
Ameanza na moto: Daniel Sturridge ameipa Liverpool ushindi kwa bao pekee dakika ya nne
Sehemu mwafaka: Sturridge akiunanisha pasi ya Daniel Agger
Yuko moto: Sturridge ameifungia Liverpool katika mechi zote tatu msimu huu
Shangwe: Sturridge akimkumbatia kocha wake Brendan Rodgers baada ya kufunga
Imependeza: Mashabiki wa Liverpool katika Kop End wakitoa heshima kwa Bill Shankly kabla ya mechi
Kuzaliwa: Wachezaji na mashabiki walitumia dakika moja kwa ajili ya Shankly kabla ya mechi
Mkwara: Steven Gerrard na Robin van Persie wakichimbiana mikwara
Kazi: Martin Skrtel, aliyechukua nafasi ya majeruhi Kolo Toure, akiruka juu kupiga mpira kichwa
Jatibio: Gerrard akipiga shuti la mpira wa adhabu ambalo liliokolewa na kipa David de Gea
Rafu: Danny Welbeck akienda chini baada ya kuchezewa rafu na Lucas na Iago Aspas
Alikuwepo: Kocha wa England, Roy Hodgson alikuwapo jukwaani Anfield kushuhudia mechi hiyo
Jukwaani: Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez anayetumikia adhabu alikuwepo uwanjani leo
Makocha: Kocha wa Liverpool, Rodgers (kulia) na wa Manchester United, David Moyes wakiwa kazin
MAJAMBAZI YAJERUHI NA KUIBA FEDHA MBEZI AFRIKANA
Difenda la Polisi likiondoka eneo la tukio na mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo aliyejeruhiwa.
Geti la kampuni ya Diab Furniture Manufacturing iliyovamiwa na majambazi.
Geti la kampuni ya Diab Furniture Manufacturing iliyovamiwa na majambazi.
Mke wa mlinzi aliyejerujiwa na majambazi akiwa getini na
mwanaye.
Kundi la majambazi waliokuwa na silaha za moto wakiwa na magari mawili
Landcruiser na Noah wamevamia kampuni inayojishughulisha na utengenezaji na
uuzaji wa fenicha ya Diab Furniture Manufacturing Company iliyopo Mbezi
Afrikana jijini Dar es Salaam. Majambazi hayo baada ya kuvamia eneo hilo
yalifanikiwa kupora sefu iliyokuwa na fedha pamoja na kuwajeruhi mmoja wa
viongozi wa kampuni hiyo na mlinzi. (Picha / Habari: Haruni Sanchawa / GPL)
KUMBUKUMBU: BOMU LAUA WANNE BUKOBA
Mmoja wa majeruhi wa bomu la shule ya msingi Tumaini Mwaka 1994, Datius Kalokola hospitalini na baada ya kurudi nyumbani |
Ni kichwa cha habari iliyotoka
kwenye gazeti flani siku ya alhamisi tarehe 1 Septemba 1994, siku moja baada ya kutokea mripuko wa bomu katika shule
ya msingi Tumaini iliyoko Manispaa ya mji wa Bukoba. Ilikuwa Jumatano 31 Agosti 1994 majira ya saa mbili asubuhi tarehe kama ya leo, tulipowapoteza wanafunzi wanne
huku 85 wakiwa wamejeruhiwa kutokana na
ajari hiyo. Nianze kwa kuwakumbuka wenzetu waliotutoka siku hiyo. Mungu
azilaze roho zao mahali pema peponi Ibrahim Mebu, Salehe Abdalah,
Yusuph Bahati na Emmanuel Joseph.
Tukiwa tumejipanga mistari “parade”
tayari kukaguliwa ili tuanze gwaride kuelekea madarasani, mara nikasikia kishindo
kikubwa kilichoambatana na hali ya mtikisiko. Hali iliyomfanya kila mwanafunzi
akimbie pasipo kujua jambo gani limetokea. Baada ya kukimbia umbali wa
takribani mita 15 kutoka eneo la tukio ghafra nikahisi kuishiwa nguvu mguu
wangu wa kushoto, niliposimama na kugeuka nyuma nikaona idadi ya wanafunzi
wasiopungua sita wakiwa wamedondoka chini eneo la tukio.Nilipotizama mguu wangu
ulikuwa ukitokwa na damu nyingi.Nilipata mshtuko na mshangao mkubwa huku nikiwaona wanafunzi wengine pia
wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao. Walimu walitahamaki wasijue
wafanye nini zaidi ya kutuambia wanafunzi tuliokuwa bado tuko ndani ya
mazingira ya shule tulale chini. Wakati huo wengi wetu wakiwa hawaonekani
kabisa katika mazingira hayo ndani ya muda mfupi wengine pasipokujua kama
wamepatwa na majeraha na wengine wakikimbia kuelekea nyumbani kwao huku wakilia
sana na damu zikiwatoka.
Nikiwa kwenye gari l a Msalaba
Mwekundu na majeruhi wengine kuelekea
hospitali, tulikutana na baadhi ya wanafunzi wakirudi shuleni baada ya kufika
nyumbani na kugundua hawako pamoja na ndugu zao ambao walikuwa nao shule moja.
Hali ya utulivu ilipotea ghafla ndani ya mji wa Bukoba na hasa kutokana na
taarifa zilizowafikia wazazi wa
wanafunzi ambao walikuwa wakijiandaa kwenda kazini na wengine wakiwa tayari
wamefika maeneo yao ya kazi. Hakuna mwanafunzi wa shule ya jirani aliyesubiri
kupewa ruhusa ya kwenda nyumbani na mwalimu wake hasa pale wanafunzi wa shule
ya msingi Tumaini walipoonekana wakipita karibu na shule hizo wakibubujikwa machozi huku wakiwa na alama za damu kwenye
mashati na magauni yao ya shule na wengine wakitoa taarifa kwamba ndugu zao au
marafiki zao wamepoteza maisha kwa sababu hawaonekani.
Tukiwa katika chumba maalum
kilichoandaliwa kwa ajiri ya kupokea majeruhi wa ajari hiyo, dakitari
alimwambia nesi mmoja amtizame mwenzetu ambaye aliletwa akiwa hajitambui.Alikuwa
amelazwa chini pembeni yangu. Baada ya nesi huyo kutekeleza agizo hilo kwa
kutumia kipimo ambacho alimuwekea kifuani, nilishuhudia mama huyo nesi akimwaga
chozi bila kujizuia. Kumbe huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kijana mpole Yusuph
Bahati amabaye tuliwai kuishi jirani maeneo ya Kashai. Wakati huo nimeshafahamu
kwamba kilichotokea ni mlipuko wa bomu.
Jioni ya siku hiyo baada ya
kutolewa kwenye chumba cha upasuaji ndani ya Hospitali ya Mkoa Kagera, nilijikuta ndani ya wodi namba 4 ya
hospitali hiyo pamoja na wanafunzi wengine wengi.Wodi mbili za hospitali hiyo
ambazo ni wodi namba 4 na namba 5 zilipokea majeruhi wa ajali hiyo na wagonjwa
waliokuwa humo kabla ya ajari wakahamishiwa vyumba vingine. Nakumbuka tulilazwa
wanafunzi wawiliwawili kitanda kimoja kwa siku hiyo ya kwanza. Kupitia maongezi
ya siku hiyo, nikafahamu kwamba wametutoka wenzetu wanne kutokana na ajari hiyo
akiwemo Ibrahim Mebu ambaye alifariki papo hapo.Huyu pamoja na mwingine
aliyeitwa Salehe Abdarah tulikuwa wote darasa la nne, wakati Yusuph Bahati na
Emanuel Joseph wakiwa darasa la tano.
Kutokana na maelezo yaliyotolewa
na baadhi ya wanafunzi ,bomu hilo liliokotwa jalalani na mwanafunzi mmoja
ambaye hakufahamika kwa jina, akamuuzia
Ibrahimu Mebu shilingi ishirini, wote pasipokujua kama ni kitu cha hatari.
Ibrahimu alikaa nalo kwa takribani siku saba akija nalo darasani na kurudi nalo
nyumbani kabla halijaripuka.Kilichosababisha bomu hilo kuripuka ni baada ya
kulifungua ikiwa ni katika hali ya michezo pasipo kujua ni kitu gani kitatokea.
Shukurani za dhati ziwaendee
wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera na Bugando ya Mwanza kwa jinsi
walivyojitoa usiku na mchana kuhudumia majeruhi na hasa wale waliokuwa na hali
mbaya sana akiwemo Benedict Nshegize. Nawashukuru pia askari wa jeshi la ulinzi
waliofika shuleni hapo kuwaonesha wanafunzi aina na maumbo tofauti ya vitu vya
hatari kama hivyo ili wanafunzi wasivisogelee pindi wavionapo na ikibidi kutoa
taarifa mahali panapotakiwa. Shukurani kwa mkuu wa mkoa aliyekuwepo kwa kipindi
hicho Mzee Philip Mangula kwa ukaribu na msaada aliyoutoa, wazazi, walimu na
wanafunzi wa shule ya msingi Tumaini na shule za jirani.
Kama msimamizi wa gazeti tanzu
hili la Semadat (Semadat Blog) na mwandishi wa kumbukumbu hii ,nikiwa pia miongoni mwa waliokuwa majeruhi wa ajari hiyo,
natoa shukurani za pekee kwa wazazi wangu, baba yangu mzazi Mzee Felix Kalokola
ambaye kwa sasa ni marehemu, mama yangu mzazi Bi.Philotea Kalokola, Baba mkubwa
Mzee Petro Buberwa na mjomba wangu maarufu kama
Dr.Lugenga, wa Hospitali ya Mkoa Kagera. Pia namkumbuka babu yangu
marehemu Philadelph Kamanzi ambaye aliendesha baiskeli jioni ya siku hiyo, akiwa
na huzuni kubwa kutoka Kijijini Kasharu na kufika mjini Bukoba usiku baada ya
kupata taarifa ambazo ni tofauti kidogo kwamba bomu hilo limeangamiza wanafunzi
wote wa shule ya msingi Tumaini.
Sina cha kuwalipa ndugu na marafiki zangu mlionipa huduma kwa kipindi
cha takribani miezi miwili nikiwa hospitalini hatimaye nikapona na kurudi
shule, hata nikaweza tena kuungana na wanafunzi wenzangu kucheza mpira muda wa
mapumziko.
Namshukuru Mungu na namuomba
awasaidie wanafunzi wote Tanzania, Afrika na Ulimwengu mzima, hasa wa shule za
awali na msingi kuepukana na majanga kama haya.
Miaka 7 mpaka 10 baada ya tukio hilo (Kidato cha nne na cha sita) |
YUSSUF HIMID ALIEFUKUZWA CCM ATOA MSIMAMO WAKE
Aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mansour
Yusuf Himid akielezea msimamo wake baada ya kufukuzwa Uanachama CCM ambapo
amesema haendi Mahakamani kupinga uamuzi wa Chama, katika ukumbi wa Salama
hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar)
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilisihi Jimbo la Kiembe Samaki (CCM) Mansour
Yussuf Himid amesema licha ya kufukuzwa Uanachama katika chama hicho hatoenda
Mahakamani kutetea nafasi hiyo kwani kufanya hivyo ni kukaribisha Malumbano
ambayo hayana tija.
Amesema kwenda kupinga uamuzi huo Mahakamani ni kuhalalisha yeye kuwa
Mwakilishi wa Mahakama badala ya Wananchi jambo ambalo hapendelei kutokea
katika maisha yake.
Mansour ameyasema hayo leo katika Kongamano la Kamati ya Maridhiano lililofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Mansour ameyasema hayo leo katika Kongamano la Kamati ya Maridhiano lililofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Amesema amekuwa akiulizwa Maswali mengi na Watu tofauti kuhusu mustakabali wake
kisiasa baada ya kufukuzwa uanachama na kuongeza kuwa hana Pesa za kuchezea
kwenda kupinga uamuzi wa Chama cha Mapinduzi Mahakamani.
“Wenzangu wamenipima na wameniona sifai ni haki yao, siendi Mahakamani, sina pesa za kuchezea wala sitaki kuwa Mwakilishi wa Mahakama” Alisema Mansour
Mansour aliyejiunga CCM mwaka 1987 alienguliwa Uanachama siku za karibuni kutokana na Kamati kuu ya Chama CC kuridhika na madai ya kwenda kinyume na misimamo ya Chama pamoja na kushindwa kuitetea Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mansour ameongeza kuwa kwenda Mahakamani ni kukaribisha malumbano na kusisitiza kuwa Waungwana hawalumbani hivyo ameamua kukaa pembeni.
Amedai kwamba baada ya kufukuzwa uanachama CCM vyama tofauti nchini vimejitokeza kuzungumza naye ili ajiunge navyo na kudokeza kuwa bado hajaamua ni Chama gani ataenda hadi pale muda utakapofika kufanya hivyo
Mansour amesisitiza kuwa hata kama Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC itaitisha uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kiembesamaki yeye hatogombea na kwamba anaweza kufanya hivyo ifikapo mwaka 2015.

Ametumia fursa hiyo pia kuwaomba Radhi wana Jimbo la Kiembe Samaki alilokuwa
akiliongoza toka 2005 na kuwashukuru Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
waliomsaidia katika kupindi chake chote cha Uongozi.
Akigusia suala la Muungano Mansour amesema ataendelea na harakati zake
kusimamia maslahi ya Zanzibar ili kuona mchakato wa Katiba Mpya unakuja
na Katiba yenye Muundo wa Muungano wa Haki na Usawa baina ya Tanganyika na
Zanzibar.
Awali katika Kongamano hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo alimshukuru Rais Kikwete kwa ujasiri wa kuleta mchakato wa Katiba Mpya na kusisitiza kuwa Kamati yake itaendelea kudai Muungano wa usawa na haki.

Mzee Moyo amedai kuwa Kamati yake haihitaji kutambuliwa na Watu wengine na
kwamba inatosha kujulikana na Wananchi ambao wanafahamu wajibu wa Kamati hiyo.
Itakumbukwa kwamba kabla ya Kongamano hilo Chama cha Mapinduzi kilitoa taarifa kwa Vyombo vya habari kuhusu kutoitambua Kamati hiyo inayoongozwa na Mzee Moyo akisaidiwa na Makamo wake Aboubakar Khamis Bakar.

Katika hatua nyingine Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye alikuwa pia Mwanachama wa
Chama cha Mapinduzi Eddy Riyami alitangaza kujiengua na Chama hicho na kusema
kwa sasa yupo huru bila Chama chochote.
Kabla ya Kongamano hilo Kamati hiyo pia iliwasilisha maoni yake kwa Tume ya Katiba mpya ambapo maoni yake yalijikita katika kuifanya Zanzibar kuwa na Mamlaka yake kamili ndani ya Mfumo wa Muungano
Kabla ya Kongamano hilo Kamati hiyo pia iliwasilisha maoni yake kwa Tume ya Katiba mpya ambapo maoni yake yalijikita katika kuifanya Zanzibar kuwa na Mamlaka yake kamili ndani ya Mfumo wa Muungano
JESHI LA POLISI LATOA TAMKO KALI KWA WAPIGA PICHA ZA UTUPU
Jeshi
la Polisi Kanda ya Kinondoni limetoa kauri nzito kuhusu picha za
udhalilishaji zilinazosambazwa na wasanii na baadhi ya watu hapa
nchini..
Akiongea katika mahojiano maarumu mkuu wa kituo cha Polisi Oysterbay “OCD” Mtafungwa alisema kuwa kimsingi kupiga picha za utupu ni kosa kisheria hivyo endapo muhusika akimatwa atashtakiwa kwa mujibu wa sheria.
Mtafungwa aliendelea kufafanua na kusema kuwa "Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya kusimamia sheria iliyowekwa na serikali hivyo huwa kuna namna ya kuwakamata wahusika hasa kama kumetokea malalamiko toka idara flani kuhusiana na matukio yoyote yanayopelekea uvunjifu wa amani au kupotosha maadili” Alisema Kamanda huyo kipenzi cha watu
Aidha Kamanda huyo aliendelea kufafanua “ Pia Jeshi la polisi linamamlaka ya kumkamata mharifu yeyote kwa muda wowote endapo kipindi hicho akikutwa anafanya uharifu ni pamoja na upigaji picha hizo chafu, Lakini kubwa tuhajitaji kumkata mtu na ushahidi ili iwe rahisi kumbana na kumfikisha mbele ya sheria” Alisema
Mtafungwa alimaliza kusema Pindi tupatapo taarifa kuhusuiana na picha hizo chafu “ Tutaendelea kufatilia kupita mitandao ya kijamii ili kuona hizo picha zikoje halafu kuwatolea taarifa hadharani kupita kwa msemaji wa Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni RPC Wambura ambae kisheria ndiye mwenye mamlaka ya kusema”
na kumchukulia hatua kali mpigaji wa picha hizo.
Alisema Mtafungwa

Subscribe to:
Posts (Atom)