Facebook Comments Box

Wednesday, March 6, 2013

MHARIRI MKUU NA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI AVAMIWA USIKU WA MANANE NA KUJERUHIWA VIBAYA KICHWANI


Pichani ni Ndugu Absalom Kibanda akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha matibabu,hospita ya Taifa Muhimbili.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri,na Mhariri Mkuu wa Mtendaji wa New Habari Coperations Ltd, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa usiku  wa kuamikia leo akiwa anashuka nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wasiofahamika na kumpiga kichwani. Amepata majeraha Makubwa kichwani na hasa jichoni,aidha taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo Kibanda alikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu.
Wadau hii ni taarifa ya kushtua sana,lakini tutazidi kutaarifiana kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana,kikubwa tumwombee Mungu amponye haraka
 
SOURCE: JIACHIE BLOG


KIJANA RALPH NAPIERSKI AJIFANYA KADINALI NA KUTAKA KUINGIA KUMCHAGUA PAPA

Kijana Ralph Napierski kushoto akisalimiana na kadinali Sergio Sebastian
Katika kituko kilichoripotiwa sana wakati huu wa kumchagua papa kijana Ralph Napierski ameweza kuepuka ulinzi mkali wavatikani na ikawa imebaki kidogo aingie ndani na yeye kumchagua papa. Kijana huyo alievaa kama Kadinali mavazi yake yalitofautina kidogo na wenzake wakati wote wakiwa na kofia nyekundu yeye alikuwa na nyeusi kiunoni wenzake walijifunga nyekundu yeye alijifunga kitambaa cha rangi ya zambarau. Ilibaki mita chache kijana huyo ambae ni bishop aingie katika ukumbi wa Paul 4 ambao ndio mkutano wa siri kubwa ukifanyika humo na maamuzi ya kumchagua papa yangefanyika humo

RAIS WA VENEZUELA HUGO CHAVEZ AMEFARIKI

Rais wa Venezuela Hugo Chavez amefariki dunia jana na kifo chake kuthibitishwa na makamu wa rais Nicolas Maduro

Wananchi wa mtaa wa caracas wakilia kwa uchungu baada ya taarifa ya msiba wa rais Hugo ambae alikuwa kiboko ya nchi za magharibi kwa msimamo wake usio tetereka



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU