Friday, October 11, 2013
PICHA: AJALI MBAYA KABUKU TANGA
MISHAHARA YA WANASOKA WA TANZANIA
Utafiti wa Mwanaspoti katika klabu zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara umeonyesha kuwa klabu tatu; Azam, Yanga na Simba ndizo zinazolipa wachezaji wake mishahara mikubwa zaidi nchini.
Katika wachezaji 13 wanaolipwa zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwezi, Azam imetoa wachezaji watano sawa na Yanga huku Simba ikitamba na wachezaji watatu.
Kundi la kwanza, wanaolipwa mshahara wa milioni 4/= kwa mwezi ni:
Kipre Tchetche (Azam), Kipre Balou (Azam), Aggrey Morris (Azam), John Bocco (Azam) Brian Umony (Azam) na Haruna Niyonzima (Yanga).
Kundi la pili, wanaolipwa mshahara wa shilingi milioni 3.6/= kwa mwezi yupo Mbuyu Twite wa (Yanga).
Kundi la tatu la wanaolipwa mshahara wa milioni 3.3/= kwa mwezi wapo Abeil Dhaira na Joseph Owino (wote wa Simba)
Kundi la nne linalipwa 2.5/= kwa mwezi lina Mrisho Ngassa wa Yanga.
Kundi la tano la wachezaji ambao wanalipwa milioni mbili kwa mwezi ni:
Didier Kavumbagu (Yanga)
Hamisi Kiiza (Yanga)
Amri Kiemba (Simba)
Uchunguzi wa Mwanaspoti, umethibitisha kuwa mshahara wa chini kwa wachezaji wa Azam ni shilingi milioni moja wakati Simba na Yanga ina kundi la wachezaji wanaolipwa kima cha chini cha shilingi laki tatu kwa mwezi.
Mishahara ya wachezaji haikatwi kodi yoyote.