Mabao
matano yaliyofungwa na mshambuliaji, Mrisho Ngassa na mawili kutoka kwa
John Bocco. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao
ulishuhudia, Tanzania Bara ikiizamisha, Somalia kwa mabao 7-0, kocha
msaidizi wa timu hiyo, Slivester Marsh amesema wamefurahishwa na matokeo
hayo japo wengi walikata tamaa ya kuona timu hiyo ikitinga hatua ya
robo fainali. ” Ilikuwa ni mechi ngumu kwa upande wetu, tulionekana kama
tusingefuzu kwa hatua ya robo fainali. Tunashukuru Mungu na tuna imani
tunaweza kufanya vizuri zaidi” alisema, Marsh.
Ngassa, alitumia dakika 90 mchana wa leo kufunga bao lake la kwanza
katika michuano, na kufunga mengine manne na kuwa kinara wa mabao katika
michuano hiyo. Alifunga mara tano, uku mshambuliaji ‘ patna’ wake,
Bocco, akifunga mabao mengine mawili na kufikisha mabao manne katika
michuano inayoendelea ya Tusker Challenge Cup, uko, Uganda. Wawili hao,
Ngassa na Bocco wamekuwa na wakati mzuri katika michuano hiyo na sasa
wapo juu katika orodha ya wafungaji bora. Ngassa ana matano n ndiye
anayeongoza, uku Bocco, akifuatia na mabao yake manne.
Katika mchezo wa leo, wachezaji, Edward
Christopher, Athuman Idd ” Chuji” na Ramadhani Singano, walipata nafasi
ya kucheza mchezo wao wa kwanza. Watatu hao waliingia kwa wakati tofauti
katika kipindi cha pili, Edo, alimpokea, Bocco, kisha, Chuji akaingia
mahali kwa Frank Domayo na Singano, mahali kwenye nafasi ya Salum
Abubakary. Katika mchezo mwingine, timu ya Taifa ya Burundi, iliifunga,
Sudan Kaskazini, bao 1-0, na kuwa vinara wa kundi kwa kufikisha pointi
tisa, tatu juu ya zile za Stars.