Facebook Comments Box

Tuesday, July 15, 2014

ISRAEL YAANZA TENA KUISHAMBULIA GAZA

 Israel imeanza tena kushambulia Gaza ikidai kuwa Hamas inaishambulia licha ya mkataba wa kusitisha vita kufikiwa. Awali Israel ilikubali kusitisha vita kufuatia pendekezo la Misri kwa
pande zote mbili kusitisha vita Jumanne asubuhi. Hata hivyo, kundi la Hamas, ambalo linadhibiti Gaza, lilikataa makubaliano hayo na kusema ni kama kusalimu amri.

Maafisa wa Palestina wanasema kuwa watu 192 wameuawa katika mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israel siku nane zilizopita ili kukomesha wapiganaji wa Hamas kuusha makombora nchini Israel.

Raia wanne wa Israel wamejeruhiwa vibaya tangu mashambulizi hayo kuanza , lakini hakuna taarfa zozote za vifo.
Wizara ya usalama nchini Israel imesema kuwa roketi 50 zimerushwa ndani ya Israel tangu isitishe vita. Mashambulizi ya hivi punde yamepiga maeneo mawili katika ukanda
wa Gaza. Kundi la Hamas lilisema kuwa hawajapokea pendekezo lolote la kusitisha mashambulizi.

Aliongeza kwamba Hamas inahitaji masharti yake yote kukubaliwa kabla ya kukubali kusitisha vita.
Idara ya usalama nchini Israel imekubali mapendekezo hayo lakini ikasisitiza kuwa itaendelea kushambulia Gaza ikiwa Hamas watasitisha kusidhambulia kwa roketi.


IPTL WATAKA KAFULILA AWALIPE BILIONI 310

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imemfungulia kesi Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ikimtaka aombe radhi na kulipa fidia ya Sh bilioni 310. Katika kesi hiyo ya madai, Kafulila anadaiwa kuidhalilisha kampuni hiyo, kutokana na kauli alizotoa dhidi yake (IPTL).
IPTL na walalamikaji wengine Pan Africa Power Solution (PAP) na Mkurugenzi wa PAP, Harbinger Seth wanamlalamikia Kafulila kuwatuhumu kuchukua fedha kinyume cha sheria katika akaunti ya
Escrow iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Walalamikaji hao kupitia kwa Wakili wao, Augustine Kusalika wamefungua kesi hiyo, wakitaka Kafulila awalipe Sh bilioni 210 kama fidia ya kutoa kauli za udhalilishaji,  kuwasababishia hasara katika biashara na kuharibu mtazamo wa biashara zao. Aidha, wanaiomba Mahakama iamuru Kafulila, awaombe radhi, pia awalipe Sh bilioni 100 kama hasara ya jumla pamoja na usumbufu
walioupata, kutokana na kauli za udhalilishaji. Kwa mujibu wa hati ya madai,  iliyopatikana mwishoni mwa wiki, Juni mwaka huu Kafulila alitangaza kuwa IPTL na Seth, walijipatia fedha kutoka akaunti ya Escrow kinyume cha sheria na kumuita Seth ni 'Singasinga', jambo lililomdhalilisha na kumharibia muonekano wake na biashara yake.

Walalamikaji hao wanadai kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,  bila kuwa na haki, Kafulila alitoa taarifa hizo, kuwa IPTL inajihusisha na biashara zisizo halali na za uongo, jambo
lililosababisha jamii kuamini na kuwaharibia mtazamo wa kibiashara. Aidha, wanadai  Kafulila akiwa mbunge alipoteza kinga ya wabunge inayowalinda wakizungumza bungeni, kwa kuwa alitoa taarifa hizo nje ya shughuli za Bunge.

Walidai Kafulila anaendelea kutoka taarifa hizo,  licha ya kumpa taarifa kwa maneno na maandishi, wakimtaka kuacha kufanya hivyo, kwa kuwa anawaharibia biashara kitaifa na kimataifa.

Kwa mujibu wa hati ya madai, IPTL iliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye shirika hilo, lakini kulitokea mgogoro kati ya IPTL, Kampuni ya VIP Engineering and Marketing na Tanesco, jambo lililosababisha wafike Mahakama Kuu. Kutokana na mgogoro huo, Mahakama iliamuru Sh bilioni 200 zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow, zisitolewe hadi kesi hiyo itakapokwisha na baada ya kesi kuisha, Mahakama iliamuru IPTL ichukue fedha hizo.

Walalamikaji hao wanadai licha ya Kafulila, kujua kuwepo kwa mgogoro huo, aliendelea kutoa tuhuma hizo, huku akijua kuwa IPTL imechukua fedha hizo kwa amri halali ya Mahakama. Wakili huyo alisema wateja wake, wanaiomba Mahakama iamuru Kafulila awalipe Sh bilioni 310 kama fidia, aombe radhi, alipe gharama za uendeshaji wa kesi hiyo na amri nyingine, ambazo
Mahakama itaona zinafaa.


PICHA NA VIDEO YA DUKA LINALO UNGUA MWANANYAMALA MUDA HUU





MUQAWAMA WATUMA NDEGE ISIYO NA RUBANI TEL AVIV

Brigedi ya Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetangaza kuwa, wahandisi wake wamefanikiwa kutengeneza ndege isiyo ya rubani kwa jina la Ababil 1. Ripoti iliyotolewa na brigedia hiyo hii leo, imeeleza kuwa, ndege hiyo imefanikiwa kuruka juu ya jengo la idara ya Wizara ya Vita ya utawala haramu wa Kizayuni mjini Tel Aviv. 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, ndege hiyo isiyo na rubani ni moja kati ya ndege tatu zenye kazi tofauti zilizoundwa na wapiganaji wa muqawama wa Kipalestina. Aidha imezitaja ndege hizo kuwa ni pamoja na ndege ya kijasusi inayofanya kazi za kuchukua habari mbalimbali za adui, ndege ya kutekeleza hujuma na mashambulizi na ya tatu ni ndege inayosheheni mada za miripuko na kujiripua katika eneo maalumu la adui. Imeelezwa kuwa ndege hiyo iliruka mapema leo asubuhi katika shughuli zake za kiupelelezi ambapo iliweza kutuma ripoti muhimu, suala ambalo limeutia kiwewe utawala huo bandia. Kwengineko Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, watu 173 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya utawala haramu wa Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza huku wengine 1, 200 wakijeruhiwa. 

Idadi hiyo imeongezeka kufuatia watu saba kuuawa shahidi hii leo akiwemo mtoto mchanga huku kijana mwingine akiuawa katika shambulizi la anga katika eneo la Rafah.

Wakati huo huo Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas ameutaka Umoja wa Mataifa kuwasaidia Wapalestina. Abbasi ametoa ombi hilo kupitia barua aliyoiwasilisha kwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, Robert Serry akimtaka awasilishe ujumbe huo kwa Katibu Mkuu wa umoja huo. Abbasi amesema kuwa, serikali ya Palestina imekwishachukua maamuzi maalumu ambayo yatatangazwa hivi karibuni kuhusiana na mashambulizi ya utawala haramu wa Israel.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU