Facebook Comments Box

Tuesday, October 22, 2013

IKIJIANDAA KUCHEZA NA RHINO RANGERS KESHO KOCHA WA YANGA AWAOMBEA MSAMAHA WACHEZAJI


Young Africans kesho itashuka dimba la uwanja wa Taifa kucheza na maafande wa jeshi la ulinzi wa wananchi nchini (JWTZ) Rhino Rangers kutoka mkoani Tabora ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa 10.

Mchezo huo ambao utachezwa kuanzia majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika mashariki, ni muhimu kwa timu ya Young Africans kupata pointi 3 ili iweze kujiweka katika mazuri ya kutetea Ubingwa wake.

Akiongea mara baada ya mazoezi ya leo kocha mkuu wa Yanga Ernie Brandts amesema matokeo ya juzi yamemsikitisha yeye, benchi la ufundi, wachezaji, viongozi pamoja na wanachama lakini haikuwa dhamira yao kupoteza pointi 3 muhimu.

Tulikuwa tunaongoza 3-0 mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, lakini kipindi cha pili wachezaji wangu walizembea sana, hawakucheza kwa umakini wala kusikiliza maaelekezo yangu hali iliyopelekea wapinzani wetu kuweza kusawazisha mabao yote 3.

"Tunawaomba sahamani sana wapenzi, washabiki na wanachama wa Young Africans kwa ujumla kwa matokeo ya juzi, tulistahili kushinda lakini kutokua makini kwa wachezaji wetu ndio kulipelekea matokeo hayo kubadilika, kikubwa kwa sasa nimeongea na wachezaji na wameahidi kutorudia makosa katika michezo inayofuata" alisema Brandts. 

Washabiki, wapenzi na wanachama wa Young Africans mnaombwa kesho kujitokeza kwa wingi kuja kuwapa nguvu vijana katika mchezo dhidi ya Rhino Rangers ambapo Yanga ikishinda itafikisha pointi 19 na kwa na tofauti ya pointi 1 tu na wanaongoza Ligi Kuu kwa sasa.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU