Facebook Comments Box

Wednesday, February 6, 2013

MILOVAN CIRKOVIC ATUA DAR KUFUATA MALIPO YAKE SIMBA, ANATAKA ALIPWE FEDHA ZA OKWI


KOCHA wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic ametua nchini jana kufuatilia fedha zake za kuvunjwa mkataba kati yake na klabu hiyo, imefahamika.

Chanzo cha habari makini kutoka ndani ya Simba, kimeambia mtandao huu kwamba, Milovan alitua jana na amepanga katika hoteli moja katikati ya jiji la Dar es Salaam kufuatilia madai yake ambayo ni zaidi ya Sh. 100 milioni.

Fedha anazodai Milovan zinatokana na fidia ya kusitishwa kwa mkataba wake na klabu hiyo ambayo sasa inanolewa na Patrick Liewig raia wa Ufaransa.

Milovan raia wa Serbia alifanikiwa kuipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara klabu ya Simba, lakini msimu huu ameifundisha timu hiyo kwa mzunguko mmoja tu kabla ya kutupiwa virago na klabu hiyo alipoenda kwao kwa likizo.

Inaelezwa kwamba, Milovan amekuja nchini baada ya kupenyezewa habari kwamba, Simba imemuuza mshambuliaji wake Emmanuel Okwi na ipo mbioni kutia kibindoni kiasi cha zaidi ya Sh. 400 milioni.

Taarifa zinasema, Milovan amepanga malipo yake yatokane na mauzo hayo ya Okwi kwani anaamini akikosa fedha kupitia mauzo hayo, hatoweza kupata fedha katika muda mfupi kutoka Simba.

“Kocha amefika jana na yupo katika hoteli ya (anaitaja), yeye amefuatilia fedha zake na anadhani anaweza kulipwa kwani amepewa taarifa kwamba kuna fedha za mauzo ya Okwi,” kimesema chanzo chetu makini kutoka ndani ya Simba.

Mtandao huu ulijaribu kumtafuta Milovan kwa njia ya simu leo kuanzia asubuhi hadi mchana na hatukumpata lakini juhudi zinaendelea ili kuweza kuzungumza naye kufahamu zaidi kuhusu mlolongo wa malipo ya fidia yake.

Shaffidauda.com uliwasiliana na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye alisema hana taarifa za ujio wa Milovan licha kutoweka wazi malipo ya kocha huyo.

“Sifahamu lolote kama Milovan amekuja nchini, hata hayo malipo yake siwezi kuyazungumzia kwa sasa. Nikipata taarifa yoyote tutawasiliana,” amesema Kaburu.





LIVE MATCH: TANZANIA 1 VS CAMEROON 0

FULL TIME : TANZANIA 1 CAMEROON 0

Dk 90 Gooooooooollll Mbwna Samatta anaipatia Tanzania bao la kwanza

 Dk 79 Kaseja anadaka shuti kali la Ashu Clovis wa Cameroon. Walikuwa wamebaki wawili tu.

Dk 73 Cameroon inafanya mabadiliko anatoka Bedimo Henri anaingia Ashu Clovis.

Dk 70 Sure Boy anapiga shuti kali langoni kwa Cameroon lakini beki Ngoula anautoa nje na kuwa kona butu.

Dk 68 Cameroon inafanya mabadiliko anatoka Olinga Fabrice anaingia Edoa Charle.

Dk 66 Sure Boy anapiga shuti kali katika lango la Cameroon lakini kipa Effala Komguep anadaka.

Dk 60 beki wa Cameroon Aminou Bouba anabanwa misuli na kutibiwa uwanjani wakati Taifa Stars ikiwa katika shambulizi kali.

Dk 60 beki wa Cameroon Aminou Bouba anabanwa misuli na kutibiwa uwanjani wakati Taifa Stars ikiwa katika shambulizi kali.

Dk 58 Cameroon inafanya mabadiliko anatoka Tchami Herve anaingia Eloundu.

Dk 56 Taifa Stars inafanya mabadiliko anatoka Mwinyi Kazimoto anaingia Thomas Ulimwengu.

Dk 54 Ngoula wa Cameroon anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Mrisho Ngassa.

Dk 48 Taifa Stars inafanya shambulizi kali langoni kwa Camerooni.

Dk 48 Taifa Stars inafanya shambulizi kali langoni kwa Camerooni.

Dk 45 Kipindi cha pili kimeanza




Dk 45 HALF TIME. Taifa Stars 0-0 Cameroon

Dk 41 Timu zinaendelea kushambuliana kwa zamu na Taifa Stars inafika mara kadhaa langoni kwa Cameroon.

Dk 28 Shomari Kapombe wa Taifa Stars anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezo mbovu.



 Dk 26 Taifa Starz inapata penalti ilikuwa krosi ya nyoni kabla ya beki ngoula kushika mpira. Nyoni anapiga anakosa.

Dk 25: Tanzania 0-0 Cameroon


Dk 20 Kipa wa Taifa Stars, Juma Kaseja anatibiwa baada ya kugongana na mshambuliaji mmoja wa Cameroon.


Dk 19 Frank Domayo anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezo usiofaa kwa mchezaji wa Cameroon.

Dk 15 Timu zinashambuliana kwa zamu na zinatawala kwa pamoja sehemu ya kiungo. TAIFA STARS 0-0 CAMEROON
DK 1: Mpira umeanza Tanzania 0-0 Cameroon


LINE UP: TAIFA STAS, Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Aggrey Morris, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Mwinyi Kazimoto na Amri Kiemba

CAMEROON: Effala komguep,assou ekotto,aminou bouba,ngoula,nyom allan,pierre wome nlend,kingue mpondo,bedimo henry,tchami herve,olinga fabrice,aboubak vicent.


BOBAN, CHOMBO WATIMULIWA MAZOEZINI, KAZIMOTO, NGASSA, BOBAN KIKAANGONI


KLABU ya soka ya Simba, ipo mbioni kuwatimua kikosini wachezaji wake watatu na jana kocha Patrick Liewig aliwatimua mazoezini wachezaji Haruna Moshi ‘Boban’ na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.

Habari zaidi ambazo zimethibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, wachezaji hao watajadiliwa na kamati ya utendaji kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utovu wa nidhamu.

BOBAN, CHOMBO WATIMULIWA MAZOEZINI
Wachezaji Boban na Chombo jana walitimuliwa katika mazoezi ya timu hiyo kwa kile kilichoelezwa kwamba, hawaendani na mazoezi ya Kocha Liewig.

Baada ya kuwavumilia kwa muda mrefu, Liewig aliwaita wachezaji hao na kuwataka kutoka katika kundi la wenzao kisha akawalekeza kwenda kaskazini mwa Uwanja wa TCC.

Wachezaji hao walifanya hivyo hadi wenzao walipomaliza mazoezi na moja kwa moja ilionekana Liewig amefikisha suala lao kwa uongozi ili waweze kuchukuliwa hatua zaidi.

Hata hivyo, mara baada ya kuondoka baadaye, meneja wa Simba, Moses Basena, alimpigia simu Chombo na kumtaka leo audhurie mazoezi ya timu hiyo kama kawaida.

Hiyo ina maana kwamba, Chombo hana kosa kwa Liewig lakini Boban amekalia kuti kavu, kwani hajaitwa na moja kwa moja jina lake limepelekwa kwa uongozi kwa hatua zaidi.

MWINYI KAZIMOTO, NGASSA, BOBAN KIKAANGONI
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ameuambia mtandao huu kwamba wachezaji watatu wa timu hiyo, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto na Boban majina yao yametua kwa uongozi ili waweze kujadiliwa kutokana na kukithiri kwa utovu wa nidhamu kikosini.

Bila kufafanua aina ya utovu wa nidhamu walionao wachezaji hao, Kaburu anasema; “Kocha ametuletea majina ya wachezaji hao na kusema tukae nao kisha tujue kama wanataka kuendelea kuichezea Simba au vinginevyo.”

“Kocha wetu yupo makini katika suala zima la nidhamu na kama mchezaji hana nidhamu, tutatmwondoa kikosini.”

Mtandao unakuahidi kufuatilia zaidi matokeo ya kikao cha uongozi wa Simba juu ya kuwajadili wachezaji hao.





RIDHIWANI KIKWETE AJISAFISHA, AMSAFISHA BABA YAKE NA WAZIRI MKUU KUHUSU KASHFA YA TANZANIA LOAN SOCIETY

.
.
.


ANGALIA PICHA ZA SHEREHE YA KUZALIWA (BIRTHDAY PARTY) YA ISHA MASHAUZI

Isha Mashauzi
on the left









Mzee Ramadhan
Makongo, Isha's father






Isha's brother






The Cake



Isha
distributing the cake



Isha with her
parents












Party by the
swimming pool


MCHORAJI WA KIJIJI CHA NGURUKA WILAYANI UVINZA MKOANI KIGOMA

Mchoraji wa picha mbali mbali,Sudi Amani mkazi wa Kijiji cha Nguruka,Wilayani Uvinza mkoani Kigoma akichora ubao wa kutambulisha Shule ya Sekondari Nguruka,iliopo mkoani humo kama alivyokutwa na kamera yetu.


JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LAKAMATA VIROBA 20 VYA BANGI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waaandishi wa habari (hawapo pichani) madawa ya kulevya aina ya bangi yaliyokuwa kwenye moja ya viroba kati ya 20 vilivyokamatwa na Polisi,mkoa Arusha.

MNAMO TAREHE 31/01/2013 MUDA WA SAA 7:30 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA LOSOITI KIJIJI CHA KIMOKUWA WILAYANI LONGIDO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKISHIRIKIANA NA ASKARI MGAMBO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA AITWAYE MANDEGE S/O PAKASI (54) MFUGAJI NA NI MKAZI WA KITONGOJI CHA LOSOITI AKIWA NA MAGUNIA 20 YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI YANAYOKADIRIWA KUWA NA UZITO WA KILOGRAMU 50 KILA MOJA.
TUKIO HILO LILITOKEA MARA BAAADA YA ASKARI HAO KUPATA TAARIFA TOKA KWA RAIA WEMA, AMBAPO INAELEZWA KWAMBA MTUHUMIWA HUYO PAMOJA NA WENZAKE WAWILI WALIKUWA WANASAFIRISHA MADAWA HAYO KWA KUTUMIA WANYAMA AINA YA PUNDA AMBAO WALIKUWA KUMI AMBAPO KILA MMOJA ALIKUWA AMEBEBESHWA MAGUNIA MAWILI.
MARA BAADA YA WATU HAO KUWAONA ASKARI HAO WATUHUMIWA WAWILI WALIKIMBIA NA WAKAFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA MMOJA.
JESHI LA POLISI MKOANI HAPA BADO LINAENDELEA KUMHOJI MTUHUMIWA HUYO HUKU WATUHUMIWA WAWILI WALIOKIMBIA WANAENDELEA KUTAFUTWA. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,(ACP) LIBERATUS SABAS



KIBONZO CHA LEO: MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA BUNGENI YAWE KWA WATU WA MIAKA 18 NA KUENDELEA



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU