Facebook Comments Box

Thursday, January 31, 2013

WANAFUNZI WAPATAO 1580 KUNUFAIKA NA MPANGO WA UFUNDISHWAJI WA LUGHA YA KINGEREZA KWA NJIA YA TEKNOLOJIA



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapund akitiliana saini na Bi Anne Devilliers,Mratibu wa Mradi wa mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa (Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapunda akibadilishana hati na Bi Anne Devilliers,Mratibu wa Mradi wa mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa (Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.


Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Abdallah Ulega akizungumza machache mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba huo wa miaka mitatu.

WANAFUNZI wapatao 1,580 wanaosoma Shule tisa za Sekondari,wilayani Kilwa, mkoani Lindi,watanufaika na mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknolojia ya kisasa TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya
uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo. Mradi huo wa miaka mitatu,utagharimu jumla ya Sh, ya Sh,144,945,218/-zitakazotumika kujenga misingi bora ya Lugha ya kingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia mwaka 2013. Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Addo Mapunda,alipokuwa akitoa taarifa katika hafla fupi ya kutiliana na saini ya utekelezaji wa mpango huo.

Mapunda alisema mpango huo,utakaochukuwa takribani muda wa kipindi cha miaka mitatu,umeanza rasmi mwezi huu kwa wanafunzi wapatao 1,580 wa kidato cha kwanza kutoka Shule tisa za Sekondari zilizopo katika wilaya hiyo. Amezitaja Sekondari zitakazonufaika na mpango huo kuwa ni,Kilwa day iliyopo mji mdogo wa masoko, Mtanga, Songosongo, Mbuyuni, Kinjumbi,Miteja,Mingumbi,Kikanda na Sekondari ya wasichana ya Ilulu. Mkurugenzi Mapunda alisema mafunzo hayo kwa kuanzia yatakuwa ni ya wiki sita,yameanza rasmi hivi karibuni na kwamba walimu wapatao 30 wakiwemo (12) wa kigeni (Volunteers) wakiwemo na walimu wazawa (18). “Hizi Shule tisa kila moja italazimika kutoa walimu wawiliwatakaopatiwa mafunzo kwa ajili ya kuendesha mpango huu katika Shule zote hizo”Alisema Mapunda. Aidha, Mapunda alisema kupitia ufadhili wa mpango huo wa mafunzo ya kingereza,Halmashauri ya wilaya itaendesha semina/warsha kutoa stadi za kufundishia masomo hayo kwa Sekondari hizo tisa zenye walimu wapatao (71).

Mapunda alisema mafunzo hayo ni nyongeza kwa walimu wote waliopo katika Shule hizo tisa za mafunzo ya kingereza ya aina mbili,TEE-TZ itakayoendeshwa kwa ufadhili wa ubalozi wa Marekani,(RELO-Regional
English Language Office kwa Sh,24,158,480/-.Katika ufadhili wa mafunzo hayo ya TEE-TZ na RELO jumla ya Sh,169,103,698/-ndizo zitakazotumika kwa ajili ya utekelezaji wake. Mratibu wa mradi huo,kutoka kampuni hiyo ya Pan African Energy,Anne Devilliers,amesema lengo la mpango huo ni,kutaka kuwawezesha wanafunzi waelewe masomo yao kwa elimu ya Sekondari na kuongeza viwango vya
ufaulu katika mitihani yao ya kidato cha nne.Devilliers akasema imebainika kwamba wapo wanafunzi waliowengi wamekuwa hawafanyi vizuri katika masomo na mitihani yao,kutokana nakutoielewa vyema Lugha ya Kingereza. Mkuu wa wilaya hiyo ya Kilwa, Abdallah Ulega, ameipongeza kampuni ya
Pan African Energy,na akasema kwamba kwa kiasi furani itasaidiakuboresha kiwango cha elimu ndani ya wilaya hiyo,mkoa na Taifa kwa ujumla. Mpango huo,ulianza kwa majaribio katika wilaya ya Mafia mkoani
Pwani,mwaka 2010 na 2011,baada ya kuona mafanikio yake,ndipo uongoziwa wilaya ya Kilwa,ukaamua mpango huo kupelekwa ndani ya wilaya yao.


 















DKT. ASHA ROSE MIGIRO AWAASA WANANCHI WA BUHIGWE KUWA NA MSHIKAMANO



Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyangamba iliopo kwenye Kijiji cha Janda,Wilayani Buhigwe,Kigoma wakati alipoitembelea shule hiyo na kuangalia maendeleo ya Wanafunzi wa shule hiyo,alipokuwa kwenye ziara ya kukutana na wananchi wa Wilaya hiyo jana.



Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Muhinda kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.Dkt. Asha-Rose Migiro amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa na mshikamano ili kuweja kunyanyua maendeleo ya kijiji na wilaya kwa ujumla.



Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kijiji cha Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.





Viongozi wa kijiji wakitambulishwa.





KOCHA KIM POULSEN ATEUA WACHEZAJI 21 WA KUIVAA CAMEROON



KOCHA WA STARZ KIM POULSEN

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.

“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.

Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU