Facebook Comments Box

Tuesday, January 15, 2013

ANGALIA KIBONZO KINACHOHUSU USAFIRI WA NDEGE

Picture
Picture

SUNZU AUZWA READING KWA BILLION 7 - AENDA KUFANYA VIPIMO VYA AFYA

Sentahafu wa Zambia Stopilla Sunzu amechukua likizo fupi kutoka kwenye kambi ya timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya AFCON 2013 ili apate nafasi ya kwenda nchini England kwenda kufanya vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo. 

Sunzu ambaye anachezea klabu ya TP Mazembe ya DRC ambayo imeandika kwenye mtandao wake kwamba ada ya uhamisho ya $4.8million imeshakubaliwa na kilichobakia ni mchezaji kukamilisha vipimo vya afya. 

Mfungaji huyo wa penati ya ushindi ya Zambia dhidi ya Ivory Coast katika AFCON 2012, anatarajia kurudi Afrika ya kusini January 19, siku mbili kabla ya mabingwa watetezi kuchuana na Ethiopia katika mechi ya ufunguzi.

HATIMAE SIMBA WAMUUZA OKWI

Sakata la mchezaji wa kimataifa wa Uganda anayeichezea klabu bingwa ya Tanzania Bara Simba SC, Emmanuel Okwi kwenda kujiunga na kambi ya Simba iliyopo nchini Oman limefikia mwisho.

Kwa taarifa za ndani kutoka ndani ya klabu ya Simba ni kwamba timu hiyo imefikia maamuzi ya kumuuza mshambuliaji huyo kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya uhamisho hapa nchini ya $300,000.

Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Simba Mh. Aden Rage kwa sasa yupo nchini Tunisia akisimamia taratibu zote za uuzwaji wa Okwi ambaye alisaini mkataba mpya wa kuitumikia Simba hivi karibuni.

"Ni kweli Mwenyekiti yupo Tunisia akishughulikia uuzwaji wa Okwi kwa klabu ya Etoile du Sahel. Ada ya uhamisho ni dola laki tatu na muda mchache ujao dili litakamilika na Okwi atapewa ruhusa ya kuzungumza maslahi binafsi na klabu yake mpya." - kilisema chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba.

Etoile du Sahel ni klabu mojawapo yenye mafanikio makubwa barani Afrika, ikiwa inashikilia rekodi ya kuwa klabu pekee barani afrika kushinda kila kombe linaloandaliwa na CAF.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU