Facebook Comments Box

Monday, September 23, 2013

ASKARI WATATU WAFARIKI BAADA YA GARI LA OPERESHENI KIMBUNGA KUPINDUKA

 
Picture
Miili ya Askari waliofariki ikiwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama-Shinyanga.
Askari Polisi watatu wa Operesheni Kimbunga wamefariki dunia jioni ya tarehe 22/09/2013 siku ya Jumapili mjini Kahama baada ya kupata ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Muleba mkoani Kagera kuelekea makambako mkoani Njombe. 

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Sungamile Kata ya Kagongwa wilayani Kahama wakati dereva wa gari hilo PF3270 PC Yusuph, akijaribu kumkwepa Bibi Kizee mmoja huku gari likiwa kwenye mwendo kasi na hivyo kumshinda na kupinduka.

Majeruhi wanane wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama wakiwemo askari polisi sita na Maafisa Uhamiaji wawili, huku magari yanayosafirisha askari kurudi vituoni kwao yakizuiliwa kuendelea na safari na kulala Kahama.
CHANZO:Wavuti


TANZANIA YATWAA UBINGWA WA AIRTEL RAISING STARS KWA WANAWAKE


Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi captain wa timu ya wasichana Tanzania na kocha wa timu ya wasichana Rogacian Kaijage zawadi za ushindi mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika  

 
Donisia Daniel ndio alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania kwa kufunga bao hilo pekee la ushindi jana.
Tanzania ilikua kundi moja na Sierra-Leone, Malawi, na Uganda. Walishinda mechi moja dhidi ya Sierra-Leone 2-1, wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda na kutoka sare na Malawi 1-1.
Malkia wadogo; Tanzania wakiwa na Kombe lao baada ya ushindi

Katika Robo Fainali, mabinti wa kibongo wakashinda 4-2 kwa mikwaju ya penalti dhidi ya DRC Uwanja wa NIS Sports, kabla ya kuifumua Uganda kwa mabai 8-1 kwenye Nusu Fainali.Mbali na ushindi huo wa wasichana wa Tanzania walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo , Mchezaji bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji bora wa mashindano kwa upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora kwa upande wa wasichana Shelda Boniface.
 Kwa upande wa wavulana Timu ya Niger wametetea tena ubingwa  baada ya kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 7-6  katika mechi ya fainali ya Airtel Rising Stars ilifanyika kwenye uwanja wa Agege nchini Nigeria.
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria, Segun Ognsanya Katikati akimkabithi Nahodha wa timu ya wasichana Tanzania, zawadi za ushindi mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika


Mwakilishi na kiongozi wa Airtel Tanzania bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi na Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika


Mabingwa; Kikosi cha Tanzania wanawake

Niger wamefanya vizuri kuanzia hatua ya makundi  baada ya kushinda michezo yote katika makundi na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu katika mechi sita. Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda.

Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo Michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika nchini Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy Pitch, National Institute for Sports Fiels na Main Bowl.

Mashindano ya kiamataifa ya umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili mwaka huu na yamekua bora kwa vijana wadogo na kwa kuzingatia jinsia.
CHANZO:BIN ZUBEIRI


PAMBANO LA AZAM NA YANGA LAINGIZA MIL 138/=


Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Azam na Yanga lililochezwa jana (Septemba 22 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 138,188,000.

Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 33 la VPL msimu wa 2013/2014 lililomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 walikuwa 24,020.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 33,065,409.1 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 21,079,525.42. 
 
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 16,812,919.89, tiketi sh. 5,022,342, gharama za mechi sh. 10,087,751.93, Kamati ya Ligi sh. 10,087,751.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,043,875.97 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,923,014.64.
Boniface Wambura Mgoyo

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


AZAM FC WAINYAMAZISHA YANGA SC YA JANGWANI KAMA HAWAPO VILE

 Kikosi cha Azam Fc kilichoifunga Yanga SC hapo jana Uwanja wa Taifa
Kikosi cha Yanga SC kilichofungwa hapo jana na Azam Uwanja wa Taifa

Baada ya Tambo za muda mrefu kuwa Yanga wataifunga Azam ambayo wao kwao imekuwa sio kazi na wamediriki kutoa baadhi ya misemo kuwa Azam watabaki kuwa Bidhaa bora na wao Yanga kuwa ni timu bora, sasa hapo jana tarehe 22/09/2013 mambo yaliwageukia hao Timu bora na wakajikuta wakichapwa bao 3 kwa 2 na hao wanaowaita bidhaa bora.

Mambo yalianza kwa Azam kujipatia bao la kuongoza kupitia kwa John Boko 'Adebayo' ambae amekuwa akiwafunga mara nyingi katika dikika ya kwanza tu ya mchezo baada ya kupokea pasi safi kabisa kutoka kwa Mganda Brian Umony ambalo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Yanga wakitafuta nao bao la mapema ili kuwapoteza Azam na juhudi zao zilizaa matunda pale walipopata bao la kusawazisha kupitia kwa Didier Kavumbagu na baadae kuongeza bao la pili kupitia kwa Hamis Kiiza 'Diego' aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Gerison Tegete ambae jana hakuwa makini kwani alikosa mabao mawili tena ya wazi.

Azam walijipatia bao la pili kwa njia ya Tuta baada ya beki mmoja wa Yanga kuunawa mpira ndani ya Eneo la hatari na Mwamuzi kuamuru ipigwe penati ambayo iliwekwa kimiani na Mchezaji mwenye kasi, nguvu na akili nyingi Kipre Herman Chetche akitokea Bench huku Ali Mustafa 'Bartez' wa Yanga akienda kulia na mpira kelekea kushoto kwake.

Baada ya bao hilo Yanga walikuja juu na kuonesha kandanda safi kwa mchezo wao wa kasi na pasi ndefu ndefu ambazo ziliisumbua sana ngome ya Azam lakini juhudi zao hizo zilikwamishwa na Mchezaji Chipukizi Faridi Musa baada ya kupokea pasi safi kutoka wingi ya kulia kwa Kipre Chetche aliyewakimbiza mabeki wa Yanga na kutoa pasi ya Banana Chop kwa mfungaji ambae bila ajizi akamwita Ali Mustafa na Kumfunga kwa guu lake la kushoto na kuipa Timu yake bao la 3 na la ushindi ambalo liliwakatisha tamaa kabisa Yanga kwakuwa muda ulikuwa umekwisha kabisa.

Tazama Picha za Mchezo huo hapa chini kwa hisani ya BIN ZUBEIRY:
 David Charles Luhende akimfanyia madhambi Kipre Chetche
 Kevin Yondani akiokoa kwa kichwa na mpira wa Brian Omony ukamkuta John Bocco akaukwamisha nyavuni na kuipatia Azam bao la kwanza.
 Farid Mussa akimtoka Beki wa Yanga Mbuyu Twite.
 John Bocco akijiandaa kumtoka Twite.
 Joackins Atudo wa Azam akiwania mpira mbele ya Simon Msuva wa Yanga
 Simon Msuva wa Yanga akimtoka Waziri Salum wa Azam
 Athumani Iddi 'Chuji' akimtoka Farid Mussa wa Azam
 Azam FC wakishangilia bao la pili la kusawazisha baada ya penati iliyopigwa na Chetche.








MAN CITY ILIVYO IADHIBU MAN UTD JANA KATIKA LIGI YA UINGEREZA NI AIBU TUPU


 Manchester United imefungwa mabao 4-1 na wapinzani wa Jiji, Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad hapo jana.
 
Kocha David Moyes amekaribishwa vizuri na Manuel Pellegrini kwa mabao ya Sergio Aguero dakika ya 16 na 47,  Yaya Toure dakika ya 45 na Samir Nasri dakika ya 50.
 
Wayne Rooney alitengeneza heshima kwa bao lake la kufutia machozi aliloifungia United dakika ya 78. 
 
Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Jesus Navas /Milner dk71, Toure, Fernandinho, Nasri, Aguero/Javi Garcia dk86 na Negredo/Dzeko DK75.
 
Manchester United: De Gea 5, Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Fellaini, Valencia, Rooney, Young/Cleverley DK51 na Welbeck.
At the double: Sergio Aguero scored twice as City romped to victory

Opening up: Aguero scores the opening goal of the derby in the first half
Perfect start: Aguero celebrates scoring the first goal in the derby
Doubling the advantage: Yaya Toure put City 2-0 up in first half stoppage time
Yaya Toure akifunga bao na kuifanya Man City kuwa 2-0  mpka mwisho wa kipindi cha kwanza.
Derby delight: Yaya Toure celebrates putting City 2-0 up on the stroke of half time
Face in the crowd: Robin van Persie missed the game through injury and watched from the stands
 Robin van Persie aliikosa mechi hiyo baada ya kuwa majeruhi kama unavyo muona jukwaani akitazama mechi hiyo.
Not going to plan: Wayne Rooney, Danny Welbeck and Michael Carrick stand dejected after another goal
Wayne Rooney, Danny Welbeck na Michael Carrickwakiwa wameshika viuno hawaamini baada ya kupigwa moja ya mabao katika mechi hiyo ya jana.
Crowded out: Marouane Fellain vies for the ball with Manchester City's Yaya Toure and Vincent Kompany
Three and easy: Aguero scores his second and City's third in the derby
It's getting better and better: Aguero celebrates with Alvaro Negredo and Samir Nasri Aguero akishangilia na  Alvaro Negredo pamoja na Samir Nasri
Manuel Pellegrini
David Moyes
Manuel Pellegrini na David Moyes wakiwa katika hali tofauti.
Easy does it: Samir Nasri celebrates making it 4-0
Samir Nasri akishangilia baada ya kupiga bao la nne na kuwa 4-0
Punch perfect: Nasri hits the corner flag in celebrationNasri akipiga kibendera cha kona kama ishara ya kushangilia bao
Too little too late: Rooney scores from a free kick to make the score 4-1 in the final ten minutes
Rooney alifunga katika dakika kumi za mwisho na kuipatia Man U angalau bao la kufutia machozi na kufanya mpambano kuisha kwa 4-1.
Teammates on different sides: Joe Hart shakes hands with Rooney at the end
Joe Hart akisalimiana na Rooney mwisho wa mchezo huo.
Trudging off: Rooney, Chris Smalling and David de Gea leave the pitch dejected at the endRooney, Chris Smalling na David de Gea wakitoka uwanjani baada ya mechi kumalizika.
Nightmare: Moyes had a horrible experience in his first Manchester derbyMoyes akiwa katika wakati mgumu  katika mechi yake kubwa ya kwanza kabisa ya Jiji la Manchester ijulikanayo kama "Manchester derby".


ANGALIA JINSI ARSENAL ILIVYO KAA KILELENI JANA KWA KUICHAPA STOKE CITY BAO 3 KWA 1




ANGALIA JINSI MANCHESTER UNITED ILIVYO CHAPWA BAO 4 -1 NA MAN CITY




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU