Tuesday, April 23, 2013
HILI NDILO KUBWA LA KUFURAHISHA KWA MAKIPA WA ARSENAL AMBALO WENGI HAWALIJUI
Hawa ni makipa wa Arsenal ya uingereza kushoto ni Sczesny
na kulia ni Fabianski. Hawa makipa wana vitu vinavyo fanana na kufurahisha.
1. Wamezaliwa tarehe sawa yaani tarehe 18 mwezi wa 4,
2. Wamezaliwa wote nchi
moja ya Poland,
3. Wote wanachezea timu ya taifa moja ya Poland,
4. Wote wanachezea Arsenal
5. Wote wanacheza nafasi moja yaani magolikipa.
HII SIMU INACHAJIWA KWA SODA NA INAKAA MUDA MREFU KULIKO SIMU YA KAWAIDA
SIMU INAYO CHAJIWA NA SODA |
Wanasema hii dunia kilichoshindikana ni kumtengeneza binadamu peke yake, kuna vitu vingine ni ngumu kuamini lakini ni ukweli vimetokea, hiyo ni simu ambayo chaji yake inatokana na soda ya Cocacola au Pepsi ambapo Mbunifu wake ni binti wa Kichina anaitwa Daizi Zheng na betri ya simu hii imegundulika kudumu na chaji mara nne zaidi ya betri ya simu ya kawaida ilivyo. |
HII NDIO TIMU YA PILI YA TAIFA ILIYOTANGWAZWA LEO NA KIM POULSEN
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza timu ya pili
ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao
baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (Aprili 23
mwaka huu) kabla ya kutaja kikosi hicho, Kim amesema timu hiyo ni sehemu
ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.
Amesema timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa
kuchezea timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20
(Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa
Stars, lakini atatumia Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.
“Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa. Wengi wa wachezaji
watakuwa vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya kuwemo ili
kuangalia uwezo wao hata kama uko nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars.
Lakini timu hii vilevile ni changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa
wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao,” amesema.
Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.
-Chanzo TFF
Makipa | |
Aishi Manula | Azam |
Hussein Shariff | Mtibwa Sugar |
Ali Mustapha | Yanga |
Mabeki | |
Kessy Hassan | Mtibwa Sugar |
Kennan Ngoma | Barnsley FC, Uingereza |
Himid Mao | Azam |
Ismail Gambo | Azam |
David Mwantika | Azam |
Miraji Adam | Simba |
Mohamed Hussein | Kagera Sugar |
Waziri Salum | Azam |
Samih Nuhu | Azam |
Emily Mgeta | Simba |
Viungo | |
Haruna Chanongo | Simba |
Edward Christopher | Simba |
Mudathiri Yahya | Azam |
William Lucian | Simba |
Jonas Mkude | Simba |
Hassan Dilunga | Ruvu Shooting |
Jimmy Shoji | JKT Ruvu |
Abdallah Sesem | Simba |
Ramadhan Singano | Simba |
Farid Mussa | Azam |
Vicent Barnabas | Mtibwa Sugar |
Washambuliaji | |
Hussein Javu | Mtibwa Sugar |
Jerome Lambele | Ashanti United |
Zahoro Pazi | JKT Ruvu |
Twaha Hussein | Coastal Union |
Abdallah Karihe | Azam |
Juma Luizio | Mtibwa Sugar |
Subscribe to:
Posts (Atom)