Elizabeth Michael. |
Friday, January 25, 2013
HATIMAYE SERIKALI YAPUNGUZA MAKATO UWANJA WA TAIFA
Angetile Osiah: Katibu wa TFF akisaini hati ya makubaliano hayo.
|
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kamati ya Ligi Kuu, Silas Mwakibinga akisaini hati ya
makubaliano kuhusu matumizi ya Uwanja wa Taifa na mgawanyo wa
mapato.source bin zubeiry
|
BREAKING NEWS: MABOMU YARINDIMA DUMILA SASA HIVI
Katika hali iliyodumu muda mrefu sana ya mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika wilaya ya Kilosa imechukua hatua mpya. Sasa hivi kuna vurugu kubwa kati ya wakulima na wafugaji ambapo hadi gari la mkuu wa wilaya limechomwa moto. Muhabarishaji wetu kutoka eneo hilo anasema kuwa hali ilifikia hivyo baada ya mkuu wa wilaya kuhalalisha mashamba ya wakulima kuwa kijiji cha wafugaji. Mpaka sasa polisi wa kuzuia ghasia wapo eneo hilo wakipiga mabomu.
Hali ya usafiri imekuwa tete kutokana na ghasia hizo. Mahakama iliamua suala hilo lipelekwe kwenye utawala na mkuu wa wilaya siku ya jumatano kaamua Mabogile kiwe kijiji hali hiyo ndio iliyoleta vurugu zote. Mkuu wa wilaya alipopigiwa kutoa maelezo ya sakata hilo alioomba apigiwe simu jioni.
KIGOMA: KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAKATIZA MKATABA NA MKANDARASI
Kikao cha kamati ya ulinzi na usalama chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa
Luteni Kanali mstaafu Issa Machibya kimeridhia kusitishwa kwa Mkataba
wa Mkandarasi M/S Kalyango Contructoins And Building Company Limited
aliyekuwa akijenga daraja Nkwasi Wilayani Uvinza.
Mkandarasi
Kalyango Construction alikabidhiwa eneo la kazi Julai 5, 2012 na
kutakiwa kukamilisha ujezi wa daraja la NKWASI Okitoba 15, 2012,
lakini pamoja na kuongezewa muda hadi Desemba 30, 2012 mkarandasi huyo
alishindwa kukamilisha kazi hiyo.
Hadi
anasimamishwa mkarandasi huyo alikuwa amelipwa zaidi ya milioni 25.7
ambazo ni kati ya shilingi milioni 97.4 alizostahili kulipwa kama
angekamilisha ujenzi.
Baada
ya taarifa ya mkuu wa mkoa safari ikawa ni kuelekea eneo la ujenzi
ambapo meneja wa wakala wa barabara mkoani Kigoma Narisi Choma ndiye
aliyetoa taarifa kwa wafanyakazi wa mkarandasi Kalyango kuwa hawatakiwi
kuendelea na kazi.
Muda
na kwa nyakati tofauti wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, katika
ziara zao, wamekuwa wakiwaonya wakandarasi wanaofanyakazi chini ya
kiwango, kauli ambazo zinaungwa mkono na wakazi wa mwambao wa kusini mwa
ziwa Tanganyika.
HUU NDIO USHAHIDI WA CHADEMA KUWA NAPE SIO MTOTO WA BRIGEDIA NNAUYE
Hoja ya Chadema ni kwamba kama Nape angekuwa mtoto halali wa Marehemu
Brigedia Moses Nnauye basi lazima angetajwa kwenye tangazo hilo la
kumbukumbu ya kifo cha mwanasiasa huyo maarufu. Je jina la Nape
lilisahaulika kimakosa?Je hoja ya Chadema ina ukweli ndani yake?Labda
Nape atajitahidi kutolea ufafanuzi tashwishwi hii.
Subscribe to:
Posts (Atom)