Uongozi wa Yanga umesema umeelekeza nguvu zake katika
kuanza ujenzi wa Uwanja wao wa kisasa kwenye eneo la Kaunda jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema wamekuwa wakiendelea na mchakato huo na mambo yatakapokamilika, kazi ya ujenzi itaanza.
“Usione tuko kimya, mchakato unaendelea nasi tunahitaji muda kwa ajili ya kujadili, kujipanga na baadaye kuanza.
“Kamati inayohusika na masuala hayo inaendelea tunakutana na wahusika na kujadili halafu tunaangalia nini kinaendelea na nini tuendelee nacho.
“Hivyo mnatakiwa kuvuta subira na baadaye mtaona mambo yanaendelea,” alisema Manji.
Tayari uongozi Yanga ulishateua kamati inayoshughulikia suala hilo iliyo chini ya Ridhwani Kikwete.
Lakini kampuni inayohusika na ujenzi wa uwanja huo kutoka China, ilishakabidhi ramani tatu kwa Yanga na wanatakiwa kuchagua moja ambayo itumike na ujenzi.

SOURSE: SALEH JEMBE