Facebook Comments Box

Tuesday, August 19, 2014

PAPA AMRUHUSU PADRI MOSHA KUOA

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani
Moshi. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Raymond Mosha wa Jimbo Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kuachana na daraja hilo.

Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa juzi katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi katika ibada zilizofanyika katika makanisa ya jimbo hilo. Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada zote.

Uamuzi huo ambao ni nadra kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia.

Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa sasa wako vyuo vikuu.

Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi. Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha linaonekana likiwa ni namba 23.

Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.

“Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.” Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo haja ya kuwa na familia lakini kanisa lilikuwa haliruhusu.

“Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu.

CHANZO: TANZANIA CLASSIC


MWANAUME ALIEJIFANYA MWANAMKE NA KUPATA KAZI AKAMATWA UGANDA

Mwanaume mmoja huko nchini Uganda Amekamatwa baada ya Kujifanya ni Mwanamke ili apate kazi ya 'House Girl'.

Zoezi lake hilo lilifanikiwa na kuweza kupata hiyo kazi lakini siku zilivyozidi kwenda Boss wake ambae ni Mama Mwenye Nyumba alishtukia mchezo na kugundua ni Mwanaume, Baada ya kugundulika jamaa alichukua kipigo kutoka kwa Majirani , alipoulizwa kwanini ameamua kufanya hivyo alijitetea akasema Maisha ni magumu na kupata kazi kama mwanaume ni ngumu.


MIAKA 18 BILA KOMRED A M BABU (1924 - 1996): TAFAKURI JUU YA ATHARI ZA 'UTAJIRISHO WA UTAWALA'

Arrival Cabral, Abdulrahman Babu na Eduardo Mondlane

"Kwa dhahiri Ken Saro-Wiwa alipaswa kuuawa, hiyo ni kwa sababu alishirikiri kutenda kile kinachojulikana katika dunia ya tatu kama 'Dhambi ya Kiuchumi' - Kutishia muunganiko wa Kimaslahi kati ya 'Makampuni ya Kimataifa' na Viongozi Walarushwa wa Nchi za Dunia ya Tatu. Wajumbe wa Genge la Watawala wa Kijeshi wa Nigeria walikuwa Manyang'au kwa kuwa walihakikisha sehemu kubwa ya mapato ya Mafuta ya Taifa hilo yanaelekezwa kwenye kukuza Utajiri wao binafsi, na yeyote ambaye alionekana kupinga mpango huu maalum wa 'Utajirisho wa Watawala' alipaswa kushughulikiwa kwa njia yoyote iwayo, halali ama haramu.

Sehemu kubwa ya Mafuta yaliyopelekea mauaji haya ya kila aliyeonekana ni kikwazo cha 'Utajirisho wa Viongozi' yalitokea katika eneo la Ken Saro-Wiwa la Ogoniland. Kampuni ya Mafuta ya 'Shell Oil' ilikuwa inamiliki asilimia 30 ya Shirika la Mafuta la Nigeria, Mafuta ni chanzo kikuu cha 'Rushwa ya Kutisha' inayozunguka maisha ya Nigeria.

Saro-Wiwa hakuwahi kujaribu kukusanya nguvu ya wafuasi katika ngazi ya Kitaifa. Alizituamanisha harakati zake za kudai maslahi ya kiuchumi yatokanayo na Rasilimali kwa watu wake wa Ogoni tu, eneo ambalo lilikuwa na changamoto tofauti na sehemu nyengine za Nigeria. Nigeria bado haijaweza kuzalisha Kiongozi Mahiri mwenye maono na Karisma ya kuwaunganisha pamoja Mamilioni ya Wanaijeria wote ili wauondoe Utawala wa Rushwa na Kinyang'au. Kwahiyo basi Mafungamano ya 'Utajirisho wa Watawala' kati ya Serikali na Makampuni ya Kimataifa yataendelea kufaidi sehemu kubwa ya Rasilimali za Taifa hilo.

Kuthibitisha hilo (La kuendelea kwa mafungamano ya 'Utajirisho wa Watawala'), siku mbili tu baada ya Kunyongwa kwa Ken Saro-Wiwa pamoja na Wanaharakati wenzake nane wa Ogoni (Saturday Dobee, Nordu Eawo, Daniel Gbooko, Paul Levera, Felix Nuate, Baribor Bera, Barinem Kiobel na John Kpuine), Kampuni ya Mafuta ya Shell Oil ilisaini Mkataba wa Dola Bilioni 2.5 (Zaidi ya Trilioni 4 za Tanzania) kwaajili ya Gesi ya Taifa hilo".

Komredi Abdulrahman Mohamed Lain Babu (1924 - 1996), katika Makala yake 'WHY KEN SARO-WIWA HAD TO HANG?' iliyochapwa na Pacific News Service, San Francisco, Marekani - 1996.

Zaidi ya Miaka 18 iliyopita Makomredi wawili muhimu kwa Mapambano ya 'Ukombozi' wa pili wa Bara la Afrika waliiaga dunia, vifo vyao vikiwa na mafunzo makubwa mno kwa kizazi cha sasa cha Tanzania na Afrika kwa Ujumla, hasa kwa mazingira tuliyonayo ya Unyonywaji wa Rasilimali za nchi za Kiafrika unaofanywa kwa ushirikiano kati ya Watawala Mafisadi wanaoziongoza nchi zetu na Makampuni ya Kibepari ya Kimataifa yanayoletwa kwa wimbo wa 'Uwekezaji' usiowanufaisha wananchi wanyonge.

Makomredi hao ni Ndugu Kenule "Ken" Beeson Saro-Wiwa - Mwandishi, Mtayarishaji wa Vipindi vya Televisheni na Mwanaharakati wa Mazingira, na Rais wa Vuguvugu la Uhai wa watu wa Ogoni, MOSOP, aliyeuawa Novemba 10, 1995 kwa kunyongwa na Serikali Katili ya Kijeshi ya Dikteta Sani Abacha baada ya kuendesha Kampeni za kutokutumia nguvu kupinga Uharibifu wa Mazingira uliokuwa ukifanywa na Makampuni makubwa ya Mafuta yaliyokuwa yakichimba mafuta katika eneo la Ogoni, Niger Delta, Nigeria.

Mwengine ni Komredi Abdulrahman Mohammed Lain Babu, Kiongozi Mzalendo mwenye kufuata Itikadi ya Ukomunisti wa mrengo wa Kimarxi na mmoja wa waasisi wa Taifa hili. Babu alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kizalendo cha Kizanzibari cha ZNP, Mwanahabari wa Shirika la Utangazaji la China, Mhariri wa Jarida la Kimapinduzi la ZANEWS, Muasisi na Rais wa Chama cha Mrengo wa Kushoto cha Umma Party kilichorikiana na Chama cha ASP kuunda Serikali ya kwanza ya Mapinduzi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Babu pia alikuwa Waziri wa Mambo ya nje wa SMZ chini ya Rais Karume na Waziri wa Kwanza wa Mipango na Uchumi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Nyerere.

Tarehe 5 mwezi kama huu mwaka 1996 Komredi Babu aliiga dunia jijini London mara baada ya kuumwa kwa muda mfupi, Alizikwa nyumbani kwao Ukutani katika Viunga vya Mji Mkongwe, Unguja Agosti 9, 1996 - Leo ikiwa ni miaka 18 na siku kadhaa tangu Mzalendo huyu atutoke.

Pichani ni Komredi Abdulrahaman Mohammed Babu akiwa pamoja na Komredi Amilcar Cabral (Kushoto), Mhandisi-Kilimo, Mwandishi na Mpigania Uhuru wa Nchi za Guinea-Bissau na Cape Verde na Katibu Mkuu wa Chama cha PAIGC na Komredi Eduardo Mondlane (Kulia), Rais wa Chama cha Ukombozi cha Msumbiji, FRELIMO. Picha husika ilipigwa Oktoba 1965, Jijini Dar es salaam wakati wa Mkutano wa Pili wa Umoja wa Vyama vya Kupigania Uhuru wa nchi za Afrika zinazotawaliwa na Ureno - CONCP, Mkutano ambao Babu alikuwa Mgeni Rasmi.

Picha ni kwa hisani ya Hifadha ya Watanzania Mashuhuri .

Babu ni
Mchumi Mjamaiya
Komredi Mmarxiya
Mwafrika Mmajumiya
Mzalendo Mtanzaniya
Mwanamapinduzi Mzenjibiya
Ulale Pema Mahliya
Vijanao Twakuombeya


KENYA:WAPENZI WA JINSIA MOJA KUPIGWA MAWE HADI KUFA HADHARANI

Nje ya Bunge la Kenya
Muswala wa sheria ya kubuni ya kipekee ambapo sasa bunge la kitaifa linapanga kujadili sheria inayopendekezwa kwamba raia yeyote wa kigeni anayepatikana akishiriki uhusiano wa jinsia moja ahukumiwe kupigwa mawe hadharani hadi kufa na kama ni raia wa Kenya basi ahukumiwe kifungo cha maisha jela.
Mwandishi na mdhamini wa sheria hiyo Edward Onwong’a Nyakeriga anapendekeza kuharamishwa kwa ulawiti na kuhukumiwa jela kwa wanaotenda kosa hilo huku akisisitiza  upo umuhimu wa kuwalinda watoto na vijana ambao wanalengwa na dhulma ambazo kwa muda mrefu zinaepukwa kutokana na mabadiliko, teknolojia na habari isiyo chujwa na watoto mayatima kukosa mwakilishi pamoja na majaribio ya wanaoshiriki uhusiano wa jinsia moja kuwalea watoto ilihali wanaendeleza uhusiano wao.

Mswada huu wa chama cha Republican Liberty Party unaharamisha uhusiano wowote wa jinsia moja na tayari spika wa Bunge la kitaifa Kenya Justin Muturi ameupokea na kuuwasilisha kwa kamati ya sheria bungeni ambayo inatathmini kisha kutoa ripoti kwa bunge


Sio kila mmoja anakubaliana na ndoa za jinsia moja hata katika nchi zilizoendelea ambazo Marais wake wanaunga mkono ndoa hizo

Muswada huo pia unapendekeza kupigwa mawe hadharani hadi kufa kwa mtuhumiwa anayepatikana na kosa la kuwalawiti watoto wadogo au anayefanya kitendo hicho na kumuambukiza mtoto virusi vya ukimwi ambapo tayari wabunge 78 wamekubali kuunga mkono muswada huo kuwa sheria na wengine zaidi wanaendelea kushawishiwa.

Haya yanajiri wakati Bunge la kitaifa la Kenya likibuni kikundi mseto cha wabunge kuhusu maisha ya walio katika uhusiano wa jinsia moja
na wameahidi kutoa mwelekeo wa jinsi ya kushughulikia jambo hilo huku muswada huu ukitarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa wanaotetea haki za binadamu. Mwandishi wa vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina amekua miongoni mwa
waliojitokeza hadharani na kukiri kushiriki mapenzi ya jinsia moja na wakati huohuo Mashirika ya kutetea haki za wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja hivi karibuni yaliwasilisha pendekezo la kutaka Wabunge kuondoa sheria zote zinazowazuia kuishi maisha yao kama watu wengine.

Katiba ya Kenya mwaka 2010 imeharamisha ndoa ya jinsia moja japo haiharamishi moja kwa moja uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja ambapo pia mwezi uliopita utafiti uliofanywa na
kampuni ya Ipsos Synovate umeonyesha kwamba 64% ya Wakenya wanaamini kwamba hisia za kushiriki mapenzi na jinsia sawa ni jambo la kujifunza ilihali 14% kati yao wanaamini watu hao huzaliwa walivyo.


MAGAZETI YA LEO: JUMANNE 19/08/2014

      






MeTL YAPATA MKOPO WA BILIONI 300

Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (MB) akisoma risala yake kwenye hafla ya utiliaji saini wa mkopo wa Bilioni 300 za kitanzania kutoka Benki ya Rand Merchant ya Afrika Kusini (RMB) iliyofanyika kwenye hoteli ya Saxon jijini Johannesburg Afrika Kusini.

Na Mwandishi wetu.
Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imetiliana saini mkataba na benki ya Rand Merchant (RMB) ya Afrika Kusini utakaoiwezesha kupata mkopo wa zaidi ya sh bilioni 300.
Mkataba huo umetiwa saini nchini Afrika Kusini na Ofisa Mtendaji Mkuu MeTL GROUP, Mohammed Dewji.
Akizungumza kabla ya kutiwa saini kwa mkataba huo,Dewji alisema kwamba mkataba huo wa kihistoria unatokana na RMB kuiamini kampuni yake ya MeTL tangu walipoanza mahusiano ya kibiashara mwaka 2007.
“MeTL na RMB tulianza mahusiano yetu mwaka 2007, wakati RMB ilipotukopesha dola za Marekani milioni 7.5million. Wakati huo MeTLilikuwa na bidhaa mbili tu,ngano na sukari! Toka wakati huo, MeTL imekuwa ikikua na kuongeza bidhaa zaidi.” Alisema Dewji na kuongeza kuwa mwaka jana 2013, uwezo wa MeTL wa kukopa sasa umefikia dola milioni 100.
signing

Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane (wa pili kulia) wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 300 za kitanzania. Kushoto ni Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na kulia ni Gregory Havermahl wa RMB wakishuhudia tukio hilo la utiliaji saini wa mkopo baina ya RMB na MeTL Group.
Dewji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini amesema kampuni yake imekuwa na mafanikio makubwa kibiashara mpaka kuaminiwa na benki mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Pamoja na mkopo huo kwa MeTL hivi karibuni kupitia kampuni yake dada ya kuingiza, kuhifadhi na kusambaza mafuta nchini ya Star Oils Ltd, ilipata mkopo wa sh. bilioni 100 kutoka kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
“Mwaka 1999 wakati najiunga katika kampuni hii ya kifamilia biashara yetu ilikuwa ni ya dola za marekani milioni 26 na sasa tumejiongeza mara zaidi ya 60 kwani sasa pato letu litafikia dola za Marekani bilioni 1.5 ifikapo mwishoni mwa mwaka”, alisema Dewji.
Alisema mafanikio yalkiyopatikana ya kulipa mikopo husika yamewezesha yeye kusaini mkataba wa mkopo wa dola za Marekani milioni 200 ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu wafikie uwezo wa kukopa dola milioni 100 za Marekani.
“Ninataka kusema kwamba maendeleo makubwa ya MeTL yasingelifikia hapa bila RMB kutuamini katika hatua za awali” alisema ofisa mtendaji huyo ambaye pia alielezea kazi mbalimbali zinazofanywa na MeTL.
Alisema kampuni yake inafanya shughuli anuai kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo na viwanda, lojistiki, huduma za fedha,majumba ya biashara, petroli,vinu vya kusindika nafaka,vifaa vya plastiki, usambazaji na masuala ya simu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane wakinywa shampeni baada ya kufanya "Toast" kama ishara ya kutakiana kheri na mafanikio kwenye biashara zao.
Akisaini mkopo huo, Dewji aliwashukuru wote waliohudhuria hafla hiyo ya kusaini kati ya kampuni yake MeTL na RMB huku ikijivunia kufanya biashara katika nchi za Ethiopia, Malawi, Msumbiji, Zambia, Dubai, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Sudan Kusini na Kenya.
Alisema kwamba kampuni hiyo inataka kujiimarisha zaidi katika sekta mbalimbali.MeTL kwa sasa ina viwanda zaidi ya 31 nchini Tanzania pekee; huku ikiwa imetawanyika katika nchi 11 zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara.
"Tumejitanua katika nchi mbalimbali barani Afrika, nashukuru kwa ushirikiano mzuri ambao umechangia mafanikio makubwa ya kampuni yetu", alisema Dewji.
Dewji maarufu kwa jina "MO" anasema elimu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Georgetown nchini Marekani ndio iliyomfumbua macho na kuona umuhimu wa kutumia fursa za ushindani wa kibiashara duniani.
“Nia yetu ni kuwa na nguvu kubwa ya kibiashara Afrika Mashariki na Kati tukipania MeTL kuwa na pato la zaidi ya dola za Marekani bilioni 5 kwa mwaka ifikapo mwaka 2018 na kutengeneza ajira za watu 100,000.” Alisema Dewji
Alisema katika hotuba yake hiyo kuwa siri ya mafanikio ya kampuni ya MeTL ya kukua kwa zaidi ya mara 60 katika kipindi cha miaka 15 tangu alipojiunga nayo kuwa ni kutumia vyema fursa zilizopo na pia hamu yangu ya kuwatumikia na kuboresha maisha ya watanzania.
“Falsafa yangu kama mfanyabiashara sio kuridhika na mafanikio niliyonayo bali kuendelea kufanyakazi kwa bidii na kufanikiwa zaidi.” Alisema.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane (kulia). mara baada ya kutiliana saini mkopo wa Bilioni 300 za Kitanzania.


KIBAKA ALIETOROKA POLISI AKAMATWA NA WANANCHI


Mwizi aliyetoroka kituo cha akiwa chini ya ulinzi wa raia wenye hasira kali maeneo ya vingunguti msimbazi
.

Raia wakipanga kumchoma moto kibaka huyo.Kibaka aliyetoroka kituo cha polisi Tabata hatimaye kukukamatwa majira ya saa tano asubuhi maeneo ya msimbazi vingunguti na kurudishwa kituoni



JK AITISHA KAMATI KUU LEO

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ameitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu kitakachofanyika Dodoma leo.

Habari za uhakika zilizopatikana Dar es Salaam jana, zinasema moja ya ajenda kubwa inayoweza kutawala kikao hicho ni mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba ambalo limesusiwa na wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Kwa muda sasa Ukawa wamekuwa wakimtaka Rais Kikwete aliahirishe Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma, kwa kile wanachodai kutotendewa haki. (Martha Magessa)


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU