Facebook Comments Box

Monday, January 28, 2013

YANGA NA PRISON WAINGIZA HELA MARA MBILI YA SIMBA NA LYON

Yanga na Tanzania Prisons zimeingiza mapato ya jumla ya sh. 101,016,000 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara iliyofanyika jana (Januari 28 mwaka huu).
Mechi hiyo namba 94 ilichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Watazamaji 17,946 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Watazamaji 16,158 kati ya hao walikata tiketi za sh. 5,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ni 98 waliokata tiketi za sh. 20,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 24,314,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,409,220.34. Asilimia 15 iliyokwenda kwenye uwanja baada ya kuondoa VAT na gharama za tiketi ni sh. 12,363,433.45.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 7,413,060.07, Kamati ya Ligi sh. 7,418,060.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,709,030.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,884,801.14.


LULU HAJAACHIWA ATARUDI MAHAKAMANI KESHO



Lulu hajaachiwa, atarudishwa mahakamani kesho kwakuwa Msajili wa Mahakama Kuu hakuwepo na hii ilikuwa ni kesi ya 'Kuua bila kukusudia'.

Kesho wadhamini watawasilisha nyaraka zao mbele ya msajili ndipo anaweza kuachiwa.
Baadhi ya masharti aliyopewa Lulu ni pamoja kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani, kuripoti mahakamani na wafadhili kuweka bondi ya Shilingi mil 20


SEKRETARIETI YA CCM YATEMBELEA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA

 Pichani kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya,akipokea  Ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,ulioongozwa na  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana uliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot),kuangalia maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategemewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje.UJumbe huo umewasili mapema jana kutoka jijini Dar kwa njia ya Treni ( reli ya kati),ambako wamekuja kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.

 Sehemu ya kuruka na kutua ndege ikiwa katika hutua ya mwisho mwisho,Kwa mujibu wa Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo ameeleza kuwa unatarajiwa kukamilika mnamo juni mwaka huu,ambapo kwa asilimia 80 maeneo mengi yatakuwa yamekwishakamilika.
 Pichani kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa   Machibya,akimtambulisha  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana kwa baadhi ya wanachama wa CCM waliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot) kuwapokea,ambapo Mh Kinana na ujumbe wake waliwasili mapema jana  jioni kuangalia maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje.
 Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na wananchi wakiwemo wanachama wa CCM,waliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma mapema jana jioni walipokwenda kutazama maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho.
 Mafundi ujenzi wakipaka rangi sehemu ya barabara ya kurukia na kutua ndege mapema jana jioni.
 Ujenzi ukiendelea.


Meneja uwanja wa Kigoma Elipid Tesha,wa pili kuli akifafanua jambo kwa ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM),uliofanya ziara fupi ya kuukagua uwanja huo na kujionea ujenzi wake unavyoendelea kwa kasi,kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh Issa Machibya akishuhudia tukio hilo adhimu, na shoto ni  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM,Martin Shigela,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye, pamoja na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro

Sehemu ya eneo ambalo linaendelea kupanuliwa ikiwa ni sehemu ya ongezeko ya marekebisho ya kiwanja hicho cha Kigoma
Pichani kati Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo akifafanua jambo mbele ya ujumbe wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa.


MWANAUME MPAMBANAJI: GODORO KICHWANI, MTOTO MGONGONI NA BEGI BEGANI


 
KAMERA za blogu asubuhi ya Januari 15, 2013 ilimemnasa mwanaume huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akivuka barabara eneo la Lunna katikati ya mji wa Morogoro huku akiwa amebeba mtoto mgongoni na kichwani akiwa na  godoro ambalo alitoka kulinunua kwenye moja ya maduka yaliopo eneo hilo.

Kuna baadhi ya wanaume wanafikira potofu kwamba jukumu la kulea watoto linawahusu wanawake pekee jambo ambalo sio la kweli, jamaa huyu amedhihirisha kwa vitendo jambo hilo kwa kutembea na mtoto wake mgongoni katikakati ya mji wa Morogoro bila kuwa na wasi wasi wowote na maneno au macho ya watu.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU