Facebook Comments Box

Wednesday, April 9, 2014

RAIS KIKWETE ACHAGULIWA KIONGOZI BORA BARANI AFRIKA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango
Mkubwa Zaidi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 .
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la
kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo la heshima
hiyo itatolewa jioni ya leo, Jumatano, Aprili 9, 2014, katika sherehe
iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C ikiwa
ni pamoja na chakula cha jioni.
Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao
hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa
watu wao na limetolewa kwa Rais Kikwete kwa mwelekeo wake
usiokuwa wa kawaida na wenye mafanikio makubwa kwa masuala ya
utawala bora.

CHANZO: EAST AFRICA RADIO


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU