katika kusheherekea siku ya wapendanoa mwanamuziki kipenzi cha warembo Diamond "rais wa wasafi" aliamua kuweka picha yake na anayesadikiwa kuwa mpenzi wake mpya Penny Mungilwa kwenye mtandao wa Instagram. Kitendo hicho hakikuwapendeza watu wengi ambao watu wengine walimshambulia na kumwambia awe na heshima na wanawake. Picha hiyo ambayo ilifanyiwa mabwebwe ili ionekane kama ya zamani kidogo na isionekane vizuri iliwashitua washabiki wengi. Mmoja wa washabiki wake waliokerwa ni anaejulikama kwa jina la someaglymofo.
Saturday, February 16, 2013
FULL TIME: AZAM 3 - 1 Al NASIR JUBA
FULL TIME AZAM 3 - 1 AL NASIR JUBA
Dk 94 Gooool Kipre Cheche anaiandikia Azam bao la tatu
Dk 90 zimeongozwa dakika 4
Dk 89 wachezaji wa Al nasir wamekuwa wakijidondosha dondosha ili kupoteza muda
Dk 80 Azam 2 - 1 Al Nasir
Dk 81 Goooool Kipre cheche anaipatia Azam goli la pili
Dk 80 Azam 1 - 1 Al Nasir
DK 72 kipre cheche anapiga shuti kali kipa wa Al Nasir anatoa nje
Dk 71 John Boco anapiga kichwa kipa wa Al Nasir anaokoa na kuwa kona
Dk 70 Azam 1 - 1 Al Nasir
Dk 65 Azam 1 - 1 Al Nasir azam wanapata faulo karibia na 18
Dk 59 anatoka Abdi Kassim anaingi John Boco
Dk 52 Azam wanakosa bao. Mpira unagonga mwamba
Dk 48 Abdi Kasim anakosa tena goli la wazi hapa
HT Azam 1 - 1 Al Nasir
Kipindi cha pili kimeanza
Dk 46 Kipa natokea goli linabaki wazi ila Mcha Hamis anapiga mpira nje
Dk 45 Refa anaongeza dakika 3 za ziada
Dk 44 Abdi Kassim "Babi" anakosa goli la wasi kwa kupiga mpira fyongo ndani ya 6
Dk 43 Abraham Malik Sadik wa Al Nasir anaonywa na refa kwa kuoneshwa kadi ya njano
Dk 38 Goooool Al Nasir wanasawazisha hapa. Jacob Osuru anawainua wasudani
DK 37 Azam wanapata kona baada ya piga nikupige kwenye lango la Al Nasir
Dk 30 Azam 1 - 0 Al Nasir
Dk 27 Beki wa Azam anateleza na kuipa nafasi Al Nasir ila Mwadini Ally Mwadini okoa hatari ile
Dk 21 Abdi Kassim Babi anakosa bao la wazi kipa anautoa mpira
Dk 19 Simon Amanya anaonywa kwa kuoneshwa kadi ya njano. Mcha Hamis anaenda kupiga faulo na inatoka nje
Dk 18 kipre cheche anaingia ndani ya 18 na kutoa pasi ambayo inatolewa nje na beki. Azam wamekuwa wakilisakama lango la wasudani sana
Dk 16 Azam inafanya mabadiliko, ametoka Brian Umony ameingia Khamis Mcha.
Dk 14 Gooo...! Abdi Kasim anaipatia Azam bao la kwanza kwa kichwa akiunga krosi ya Kipre Tcheche. Azam 1-0 Al Nasir.
Dk 13 Azam 0 - 0 Al Nassir Juba
Kikosi cha Azam FC kitakachoshuka Uwanja wa Taifa leo jioni kuikabili Al Nasri Juba ya Sudan Kusini kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kinaundwa na
Mwadini Ally (GK), Himid Mao, Malika Ndeule, David Mwantika, Jockins Atudo, Michael Bolou, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Humphrey Mieno, Brian Umony, Abdi Kassim ‘Babi’ na Tchetche Kipre.
Sub: Aishi Salum, Luckson Kakolaki, Khamis Mcha ‘Vialli’, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aziz, Abdulhalim Humud, Seif Abdalah ‘Karihe’, Gaudence Mwaikimba, Seleman Uhuru na Omari Mtaki
Benchi la ufundi: Kocha Stewart Hall, msaidizi Ibrahim Shikanda, kocha wa makipa Idd Abubakar, Daktari Mwanandi Mwankemwa na Paul Gomez
All the Best Guys!
God Bless Azam FC, God Bless Tanzania!

TENGA AMCHINJIA BAHARINI MALINZI, AMWAMBIA; "KAKA NENDA FIFA TU, HAPA UMEKWAMA"
Rais wa TFF, Tenga akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo Uwanja wa Taifa |
Na Mahmoud Zubeiry
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba wagombea walioenguliwa na Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wana namna mbili tu za kufanya ili kutafuta haki yao, moja kuomba pingamizi dhidi yao kusikilizwa tena au kwenda Mahakama ya Usuluhishi ya Soka (CAS), iliyo chini ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF, Tenga amesema kwamba TFF ilijiwekea utaratibu ambao lazima uheshimiwe.
Alisema mchakato wa uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Februari 24, mwaka huu ulianza vizuri na umeendelea vizuri hadi kufika hapa ulipo, ingawa amekiri kuna matatizo.
Tenga alisema kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa TFF, Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ndiyo chombo cha mwisho na mtu anapokwama hapo hana pa kwenda zaidi ya CAS.
Kauli hiyo ya Tenga imefuatia Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake Iddi Mtiginjola kumuengua mgombea wa nafasi ya Urais, Jamal Malinzi kwa madai mawili, kukosa uzoefu na kupinga waraka wa mabadiliko ya uchaguzi.
Taarifa ya Mtiginjola Jumatatu, ilisema kwamba mgombea pekee aliyepitishwa katika nafasi ya Urais, inayoachwa wazi na Tenga anayeng’atuka ni Athumani Jumanne Nyamlani.
Malinzi aliwekewa pingamizi awali, lakini akashinda mbele ya Kamati ya Uchaguzi na baadaye akakatiwa Rufaa, ambayo imemuengua.
Nyamlani pia aliwekewa pingamizi, akashinda na akakatiwa Rufaa lakini pia ameshinda, baada ya pingamizi alilowekewa kutupiliwa mbali.
Wengine walioenguliwa ni Michael Wambura aliyekuwa akiwania nafasi ya Makamu wa Rais na Ahmed Yahya aliyekuwa akiwania nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Ligi.
Hata hivyo, Tenga amesema kwamba tayari Malinzi na Mohamed Yahya wameomba kusikilizwa upya kwa pingamizi dhidi yao.
Kufuatia matatizo haya, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Jumanne wiki hii iliamua kusimamisha kampeni za uchaguzi wa shirikisho hilo zilizopangwa kuanza Jumatano, kuelekea uchaguzi huo Februari 24, mwaka huu.
Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Lyatto ilisema kwamba, Kamati yake imechukua hatua hiyo kutokana na Mamlaka iliyonayo Kikatiba.
“1. Kamati ya Uchaguzi, kwa mamlaka iliyonayo, kupitia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 3(1), 6(1) (g) na (l), 10(5), 11(6) inayosomeka pamoja na Ibara ya 14(1) na (2) na pia Ibara ya 26(5) na (6), imesitisha zoezi la kampeni za uchaguzi wa TFF na TPL Board lililokuwa lianze kesho tarehe 13/02/2013 hadi hapo itakapowatangazia, ili kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF,”imesema taarifa hiyo.
Aidha, Taarifa ya Lyatto imesema; “2. Tarehe za Uchaguzi Mkuu wa TFF na TPL Board zinabaki kama zilivyopangwa. 3. Taarifa hii inazingatia pia Ibara ya 2(4) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF inayoagiza uongozi uliopo madarakani kuendelea na kutekeleza majukumu ya Shirikisho hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika,”.
LILE SAKATA LA KUTOKUWA NA MITAALA MAALUM MKURUGENZI WA TAASISI YA ELIMU TANZANIA AJIUZURU
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Dk Paul Mushi
Kufuatia
sakata kuwa Serikali haina mitaala rasmi ya kufundishia shuleni,
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Dk Paul Mushi,
amejiuzulu wadhifa huo.
Nafasi yake imechukuliwa na Mkurugenzi wa Idara ya kubuni na kuendeleza Vifaa vya Elimu, Dk Leonard Akwilapo.
Akihojiwa kwa njia ya simu jana jijini Dar es Salaam, Dk. Mushi alithibitisha kujiuzulu na kusema alichukua hatua hiyo kwa hiari yake bila kushinikizwa na mtu, “Hakuna aliyenishinikiza nimeamua mwenyewe kuandika barua ya kujiuzulu,” alisema Dk. Mushi
Kaimu Mkurugenzi Dk. Akwilapo alipohojiwa juu ya mtangulizi wake aliyeachia ngazi , Alhamisi wiki hii, alisema aliondoka kwa maamuzi yake mwenyewe bila shinikizo kama alivyoeleza, “Sio siri ni kweli amejiuzulu na aliniambia ni maamuzi yake aliyoyafanya ya kujivua madaraka ya Mkurugenzi Mkuu bila ya kugombana na mtu na juzi ndio alipewa barua yake na mimi kupatiwa barua ya kuwa kaimu,” alisema Dk Akwilapo
Katika mkutano wa Bunge la mwezi huu, Mbunge wa kuteuliwa na Rais James Mbatia (NCCR-Mageuzi), aliwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu hapa nchini.
Katika hoja hiyo, aliibua sakata la kutokuwapo kwa mitaala inayoongoza ufundishaji wa masomo shuleni hali inayosababisha kudorora kwa elimu. Kadhalika aliibua tuhuma za uchapishwaji wa vitabu ambavyo maudhui yake hayana viwango pia waliopewa kazi ya kuchapisha ndiyo hao waliokuwa wahariri na waandishi. Pia alihoji sababu za uchapishaji wa vitabu hivyo kufanyika nje ya Tanzania hali ambayo inasababisha kuwapo kwa matumizi mabaya ya fedha.
Katika kujibu hoja hizo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alilithibitishia Bunge kuwa serikali ina mitaala na nakala zake ziliwasilishwa bungeni na hoja hiyo ikazimwa. Baada ya kuwasilishwa kwa mitaala hiyo, bunge iliunda kamati ya kujiridhisha kama ni kweli mitaala hiyo ni sahihi ambapo ilikuja na majibu ya kujiridhisha kuwa ni ya kweli.
Hata hivyo, kwa upande wa James Mbatia alisema bado kuna utata katika mitaala hiyo licha ya kamati hiyo kujiridhisha kuwa mitaala ipo sahihi.
PICHA ZA KIKAO CHA BARAZA LA VIJANA LA CCM KINACHOFANYIKA LEO NA KESHO DODOMA
Meza kuu wakati wa kuanza kikao |
Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wiliam Malecela maarufu kama LEMutuz akiwa anasisitiza jambo kwenye mkutano huo. |
Sekretarieti ya UVCCM ikiwa meza ya mbele pamoja na wajumbe wengine wa Baraza Kuu la UVCCM |
Wajumbe wa Baraza mbele pamoja na Chipukizi na kikundi cha uhamasishaji wa UVCCM Mkoa wa Dodoma wakiwa safu ya nyuma. |
Kikao kikifunguliwa |
Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa. |
HUYU NDIO MMAASAI WA KWANZA ANAENDESHA NDEGE AINA YA AIRBUS YA FAST JET
William Zelothe Stepehen akiwa ndani ya ndege aina ya Airbus A319.
William Zelothe Stepehen akiwa na marubani wa ndege ya Fastjet.
William
Zelothe Stepehen ni Mtanzania wa Kwanza Mmaasai aliyepewa ithibati ya
kuiongoza ndege aina ya Airbus A319 punde tu baada ya kupokea mafunzo ya
urubani yaliyodhaminiwa na shirika la ndege la fastjet. Alipata mafunzo
hayo nchini Uingereza kwa muda wa takriban miezi miwili na amerudi
nchini Tanzania hivi karibuni. William alikulia Olosipe jijini Arusha
ambapo ni nyumbani kwa wazazi wake.
William
anafananisha anavyojihisi anapoiongoza ndege ya Airbus A319, na wakati
akiwa katika nyumba nzuri ya kifahari na ya kisasa; anaielezea ndege ya
Airbus A319 kama ndege iliyo imara na ambayo imewekewa mifumo mingi ya
usalama. Kwa maneno yake mwenyewe, anasema “Ndege ya Airbus inakulinda
kweli kweli, kama unaifahamu vyema”
William
amewahi kusomea usimamizi wa wanyama pori; alipata mafunzo ya urubani
kwa mara ya kwanza kule Florida Aviation Academy nchini Marekani mwaka
2006 ambapo alipata leseni yake ya usafirishaji kwa ndege. Ingawa ana
umri mdogo, ana uzoefu wa masaa 3,053 ya kuongoza ndege.
Kumwajiri
rubani huyu mtanzania mwenye miaka 28, ni mojawapo ya jitihada za
fastjet za kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inaajiri watendaji wazawa
waliobobea katika fani hiyo hapa nchini. Mikakati yao ya kuajiri pia ni
mojawapo ya wajibu wao mpana wa kuwekeza nchini Tanzania. Kwa kila
rubani aliyepokea mafunzo, fastjet imetumia gharama inayokadiriwa
shilingi 49,546,400 hela za kitanzania ambayo ni sawa na 31,027 dola za
kimarekani.
fastjet
ni shirika jipya la ndege la nauli nafuu Afrika ambalo lilipata umiliki
wa FLY540 na kwa mantiki hiyo likazindua kampuni ya kwanza ya usafiri
wa ndege ambalo linazingatia bajeti. Fastjet, ambayo inaungwa mkono na
mwanzilishi wa Lonrho na easyGroup Bwana Stelios Haji Ioannou,
imetambulisha nauli za kiwango cha chini hadi kiasi cha Tsh32,000 bila
kujumlisha kodi ili kuwawezesha mamilioni ya watu ambao walikuwa
wameshindwa kusafiri kwa ndege, kuweza kusafiria ndege kwa mara ya
kwanza na kuendelea kutumia ndege mara kwa mara. Tangu kuzinduliwa kwake
mwezi Novemba 2012, shirika hili la fastjet limewasafirisha zaidi ya
watu 70,000 na asilimia 99.7 ya safari za ndege zikisafiri katika muda
uliopangwa.
HII NDIO HUKUMU YA KESI YA SISTER ALIEFUMANIWA NA MME WA MTU
MAHAKAMA
ya Mwanzo mjini hapa, imemtia hatiani aliyekuwa mtawa wa Shirika la
Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani,
kwa kufumaniwa na mume wa mtu na kuamriwa kumlipa fidia ya Sh 700,000
mlalamikaji.
Katika kesi ya msingi ya madai, mlalamikaji Asteria Mgabo alimtaka Sista Yasinta amlipe Sh milioni 3 baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa, Martin Msangawale (39) ambaye pia ni mkazi wa mjini hapa.
Sista huyo ambaye ni daktari katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa, kwa sasa anaishi nje ya nyumba ya utawa eneo la Kantalamba.
Katika hati ya awali ya madai, inadaiwa mshitakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa na mumewe Msangawale wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Chipa iliyopo eneo la Katandala mjini hapa, Desemba 24 mwaka jana majira ya saa 7 usiku ikiwa ni siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas.
Akisoma hukumu hiyo juzi, hakimu wa mahakama hiyo, Jaffar Mkinga alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mlalamikaji ulikuwa mzito wenye kuondoa shaka zote kuwa mdaiwa alitenda kosa hilo tofauti na utetezi uliotolewa na mdai kuwa ulikuwa dhaifu.
Awali katika utetezi wake mdaiwa aliiambia mahakama hiyo kuwa kwanza alikuwa hajui kuwa Martin alikuwa mume wa mtu na kukiri mbele ya mahakama hiyo kuwa alimweleza kuwa hana mke hivyo alimwomba amuoe.
Lakini Hakimu Mkinga alipinga utetezi huo kwa sababu usiku huo wa mkesha wa Krismas mwaka jana, saa saba na robo usiku, mlalamikaji akiongozana na mwenyekiti wa mtaa wakiwa na mashahidi wengine watatu, walimkuta mdaiwa na Martin wakitoka katika moja ya vyumba katika nyumba ya kulala wageni ya Chipa, akasainishwa.
“Kama hukufahamu kuwa Martin alikuwa hana mke ilikuwaje ukakubali kusaini karatasi hiyo ya fumanizi iliyoandaliwa na mwenyekiti huyo?” alihoji hakimu, akamhukumu kulipa sh 700,000.

HAWA NDIO WABUNGE WALIOKUBALI KWENDA JKT NA SABABU ZAO
JUMLA
ya wabunge 47 kutoka vyama CCM, Chadema na NCCR-Mageuzi, wamekubali
kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa ajili ya mafunzo na
uzalendo kwa taifa.
Habari za kuaminika zilizopatikana mjini Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na Makao Makuu ya JKT, zinasema wabunge hao wametawanywa katika vikosi mbalimbali na wanatakiwa kuripoti kwenye vikosi vyao kunzia Machi mosi, mwaka huu.
Msemaji wa JKT, Meja Emmanuel Mruga, alipoulizwa kuhusu wabunge hao kujiunga na jeshi hilo, alisema mpaka sasa wana orodha ya wabunge 47 kutoka vyama mbalimbali.
Alisema wabunge hao, wametawanywa katika kambi mbalimbali kwa ajili ya mafunzo ambayo yatarajia kuanza mwezi ujao.
Alisema wabunge hao, waliomba wenyewe kwa ajili ya kupata mafunzo ambayo wanaamini yatawajengea uzalendo zaidi kwa taifa lao.
Baadhi ya wabunge ambao KITONGONI imepata majina yao na vyama wanavyotoka kwenye mabano ni David Kafulila (NCCR-Mageuzi), Zitto Kabwe (CHADEMA), Halima Mdee (CHADEMA), Freeman Mbowe (CHADEMA), Abdulkarim Shaha (CCM), Esther Bulaya (CCM), Twaida Galusi (CCM), Neema Hemed (CCM), Ezekiel Wenje (CHADEMA), Joshua Nassari (CHADEMA), Raya Ibrahim (CHADEMA), Godbless Lema (CHADEMA) na Nyambari Nyangwine (CCM).
Akizungumzia mafunzo hayo, Zitto Kabwe alisema kuanzia sasa anajiandaa kuanza maisha mapya ya jeshi na atapumzika siasa kwa muda wa miezi sita.
“Najiandaa kupumzika siasa, kwa ajili ya kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), nadhani ni hatua nzuri ambayo tunataka kuwaonyesha Watanzania wazalendo na vijana wenzetu,” alisema Zitto.
Naye Mdee, alisema zaidi ya robo tatu ya wabunge wote vijana wa chama hicho, waliomba kujiunga JKT na tayari wamepangwa katika vikosi mbalimbali.
“Si mimi na Zitto, nakwambia karibu robo tatu ya wabunge vijana wa CHADEMA, tumeamua kujiunga kwenye mafunzo ya JKT,” alisema Mdee.
Alisema yeye amepangwa kikosi cha 842 KJ kilichopo Mlale, mkoani Ruvuma.
Alisema wengine ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambaye amepangiwa kikosi cha JKT Ruvu, Mkoa wa Pwani.
Habari zinasema Mbowe aliomba kujiunga JTK na amepangiwa kambi moja mkoani Tabora.
Akizungumzia sababu za kujiunga na jeshi hilo, Mdee alisema wanataka kujifunza mambo tofauti yatakayowasaidia kutekeleza wajibu wao wa kisiasa na kijamii sawasawa.
“Unajua sisi ni viongozi wa watu, tunadhani mafunzo ya kijeshi yatatusaidia kutekeleza kazi za kila siku, kujifunza ukakamavu, na zaidi kwa vipi tunaweza kujilinda kwa mantiki ya usalama binafsi.
“Kingine ni kujifunza kazi za kila siku za maisha, kiuchumi, kijamii, kilimo na vitu kama hivyo ukizingatia sisi ni viongozi tunaopaswa kuongoza watu, hususani wapiga kura kwa mifano.
Kuhusu kujifunza zaidi uzalendo kama ambavyo imekuwa ikisemwa na viongozi serikalini, Mdee alisema uzalendo ni tabia ya mtu binafsi na kamwe jeshi haliwezi kumfundisha mtu uzalendo.
“Ninakubaliana na suala la nidhamu, jeshi linaweza kumfundisha mtu nidhamu, lakini siyo uzalendo.
“Walioharibu nchi na kuitumbukiza katika ufukara na ufisadi karibu wote wamepitia jeshini, hatuna cha kujifunza kwao kutokana na kwenda kwao jeshini,” alisema na kuongeza:
“Ngoja twende huko tukajifunze mambo ya ziada, naamini tutapata kitu cha ziada kwa ajili yetu na jamii tunayoiongoza”.

SINGANO (MESSI) NA KAPOMBE KWENDA SUNDERLAND YA ENGLAND
WACHEZAJI chipukizi wa timu ya soka ya Simba Ramadhan Singano ‘Messi’ na Shomari Kapombe wanatarajiwa kwenda kufanya majaribio katika kituo maalum cha vijana cha klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Sunderland.
Aidha, vuiongozi wa Simba, wanatarajiwa kwenda huko hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine watashuhudia mechi ya ligi kuu ya England baina ya wenyeji Sunderland dhidi ya Fulham itakayopigwa Machi 2 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema, hatua hiyo inafuatia ushirikiano baina yao na Sunderland uliotokana na matunda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Alisema katika makubaliano yao ya ushirikiano na udhamini, Sunderland ambayo imepania zaidi kuwekeza katika soka la vijana ambapo itakuwa ikichukua wachezaji katika makundi tofauti ya umri wa klabu ya Simba na kwenda kujifunza katika taasisi yao ya vijana.
Rage aliongeza kuwa, Kapombe na Singano watakwenda huko mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom ambapo pamoja na kupatiwa mafunzo maalum katika kituo cha kulea vijana cha timu hiyo, kama watafanya vema katika mazoezi yao huenda wakasajiliwa kuichezea timu ya vijana ya Sunderland.
Aidha, Rage aliongeza kuwa mazungumzo kuhusiana na udhamini wao na Sunderland yapo katika hali na ndiyo maana uongozi umealikwa kwenda huko si kwa ajili tu ya kushuhudia mechi bali kubadiklishana uzoefu na viongozi wa timu hiyo.
Akizungumzia maandalizi ya mechi yao yao ya ligi ya mabingwa Afrika kesho dhidi ya CR Libolo ya Angola, Rage alisema kikosi cha timu hiyo kipo katika hali nzuri na wachezaji wana ari kubwa ya kuhakisha wanashinda, hivyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia.
Kuhusiana na kusuasua kwa Simba kwenye ligi kuu bara, Rage alisema hiyo inatokana na timu zote zinazoshiriki ligi hiyo kujipanga vema,huku akibeza watu wanaoendekeza ushabiki zaidi badala ya kuangalia ushindani uliopo uwanjani.
Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharoos amewataka watu kujitokeza kwa wingi kuishangilia Simba katika mchezo wake wa kesho huku akiwasihi zaidi wanawake wenzake kwenda kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam utakapopigwa mchezo huo.
JE, WAJUA MPENZI WA PREZZO ALIEKUFA ALIKUWA MKE WA MTU? ANGALIA PICHA HIZI ZA HARUSI
Baada ya kuweka picha hizo za ushahidi kuwa marehemu alikuwa mke wake jamaa akaamua kutoa biti zito kwa Prezzo akae mbali katika kipindi hiki kigumu katika familia yake
UMOJA WA MATAIFA WASEMA MAZUNGUMZO NDIO NJIA SAHIHI YA KUMALIZA MIGOGORO YA KIDINI
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson |
Wakati viongozi wakuu mbalimbali nchini Tanzania wakisisitiza haja na umuhimu wa viongozi wa
madhebu ya dini kuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara. Umoja wa Mataifa
nao kwa upande wake unaeleza kwamba ni
kwa njia ya mazungumzo
migogoro ya dini inaweza kuepukika.
Kauli hiyo ya Umoja wa Mataifa, umetolewa na Jan Eliasson,Nabu Katibu Mkuu wa chombo hicho ya kimataifa , wakati wa
tukio maalum la Muungano kwaajili ya utamaduni wa Amani kwa njia
ya maelewano ya madhehebu ya dini. Tukio ambalo limefanyika
mwishoni mwa wiki hapa umoja wa mataifa likiwahusisha wawakilishi kutoka dini mbalimbali, vyama visivyo vya kiserikali
na mabalozi.
“Migogoro mingi inayoendelea hivi sasa duniani, ni migogoro ya kidini. Mazungumzo baina ya
imani mbalimbali yanaweza kusaidia kusuluhisha migogoro hii. Tunaweza kupambana na chuki kwa njia ya
mazungumzo ili kujenga maelewano na
kujenga daraja la maisha bora kwa jamii zetu”.Akasema Naibu Katibu Mkuu
Na kuongeza kuwa, dini zote
zimekuwa mstari wa mbele katika juhudi
si tu za kuhimiza amani na upendo, bali hata katika miradi ya kuwasaidia watu maskini kwa kutoa huduma kama vile za afya, na kuwasaidia vijana.
Hata hivyo akaonya kwamba, siasa kali za kidini zimekuwa chimbuko la uharibifu wa kudumu
na mateso katika jamii.
Na kwa sababu hiyo akasisitiza
kutoachiwa kwa vikundi vya dini vyenye misimamo mikali kuharibu na kuvuruga amani na maendeleo na kazi nzuri inayofanywa na
madhehebu ya dini .
“Hatuwezi kuruhusu kundi dogo la watu
wenye misimamo mikali kuharibu kazi
nzuri zinazofanywa na jumuia za kidini
kwa waumini wao duniani kote” akahimiza Bw. Eliasson
Akaelezea wasi wasi wake kuhusu vijana kutumiwa na vikundi vyenye misimamo mikali
kueneza kampeni za chuki na vurugu kwa ahadi za kupata dhawabu au wokovu
ili wao watimize malengo yao.
“Kwa kawaida vijana wana nguvu. Tunapashwa
kutafuta njia nzuri na sahihi za
kuwafanya wazitumie nvugu zao kuboresha
maisha yao” akasisitiza Naibu Katibu Mkuu.
Naye
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuk Jeremic kwa upande wake alisema Umoja wa Mataifa unaweza kufaidika sana kama viongozi wote wa dini watajihusisha na
kufanya kazi kwa moja ili kuleta amani. Huku akiutaka Umoja huo kuogeza kasi ya kushirikiana na
madhehebu ya dini.
“ Hebu basi na turejee na kukumbatia wito unaotolewa na imani
zetu, wito wa kuwasaidia watu wengine wenye matatizo, wito wa kuheshimiana
wenyewe kwa wenyewe,ikiwa ni pamoja na
uhuru wa kuabudu wakati wowote na mahali popote bila ya kujali tofauti
zetu za imani”.
Rais huyo wa Baraza Kuu akasema kila
mtu anawajibu wa kuwasiliana na mwenzake na kusahau yaliyopitia na kuonya
kwamba kama vyanzo vilivyopita vya
migogoro ya kidini vitaendelea kukumbushiwa mara kwa mara, kuna hatari kubwa ya
kuitumbukiza dunia katika machafuko ya
kutisha.

ZIARA YA MAMA SALMA LINDI MJINI NA WANACHAMA WA CHADEMA NA CUF WALIOJIUNGA NA CCM
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mama Salma Kikwete mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nanyanje, wilaya ya Chikonje, wilaya ya Lindi mjini. |
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Chikonje, wakimsikiliza Mama Salma Kikwete alipozungumza nao katika kikao cha ndani, kwenye Ofisi ya CCM ya Kata hiyo. |
Wanachama wapya wa CCM waliokabidhiwa kadi zao wakiwemo kutoka vyama vya CUF na Chadema, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao na Mama Salma Kikwete. |
Wasanii wa kundi la ngoma ya zindiko ya Chikonje wakionyesha umahiri wao katika mkutano huo. Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kijiji cha Nanyanje kata ya Chikonje mkoani Lindi. |
Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya zindiko ya
wakazi wa Chikonje, iliyotumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara
uliofanyika leo.
|
Wananchi wakiselebuka kwa nyimbo za CCM wakati wa mkutano huo. |
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kijiji cha Nanyanje kata ya Chikonje mkoani Lindi. |
Subscribe to:
Posts (Atom)