Facebook Comments Box

Monday, April 1, 2013

ANGALIA JUMA NATURE ALIVYOTAWAZWA RASMI KUWA MFALME WA TEMEKE BAADA YA KUWABURUZA TEMEKE FAMILY


Sir Kassim Juma Nature, kinara wa kundi la TMK Wanaume Halisi akiwanyooshea Mike mashabiki wake usiku wa kuamkia leo katika mchuano wa NANI MFALME ambapo mashabiki walimkubali kuwa Mfalme wao dhidi ya mahasimu wao, TMK Wanaume Family.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mashabiki wa TMK Halisi, wakati wote vidole juu...TATU BILA, hata walipopagawishwa na nyimbo kali za TMK Family.
Mhe. Temba akicheza na mashabiki katika mpambano huo wa kukata na shoka
JB wa TMK Halisi akicheza na mashabiki wake pia
Sir Nature (kulia) na Doro..kazini
Mhe. Temba na Chege,,,kazini
..Inspector Haroun akiwa jukwaani akiwakilisha Gangwe Mob kivyake
..Inspector anapoamua kuvua viatu na kupiga shoo peku...
..Chezea Dar Live wewe!
Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akionesha manjonjo yake mbele ya mpiga gitaa wake!
...dogo Lila kutoka kundi la Nature, akiwa ni member mpya wa kundi, akichana mistari vibaya mno....
...dogo Aslay wa TMK Family akiwaimbisha mashabiki
...Profesa jay nae alikuwepo kuwakilisha vilivyo game ya Hip Hop
DJ Jd alikuwepo kwenye mashine kucheza nyimbo za Prof jay na pia kuwaonesha Ma DJ chipukizi jinsi ngoma inavyochezwa!
........shooo wa Wanaume Family ikipamba moto
DJ JD alikuwa kama jaji pia, hapa akimtangaza Nature ndiye Mfalame kama mashabiki walivyoitikia.
Nature akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mfalme.


WAKAZI WA BUKOBA WAMLAKI DIAMOND PLATNUMZ KWA KISHINDO













Jana msanii Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz alitua mjini Bukoba, Kagera kuendelea na ziara yake ya kutumbuiza mikoa ya kaskazini magharibi. Kama inavyoonekana kwenye picha, umati mkubwa wa watu ulijitokeza kumlaki Diamond, kitu ambacho kilimpelekea msanii huyo kuchomoza juu ya gari kuwasalimia.

Kwa mujibu wa Diamond’s official website, kitendo cha Diamond kujichomoza juu ya gari kilisababisha msongamano mkubwa zaidi, na kusababisha barabara kufungwa, na baadhi ya kazi kusimama kwa muda.
“Juzi….Tarehe 30 march niliwasili salama salimini mjini bukoba Mkoani Kagera….Pili niwashukuru Mashabiki zangu wote Mkoani Humu kwa kunipokea kwa hali na mali ,Hii inaonyesha jinsi gani watanzania wanathamini na wana mapenzi na wasanii wao…..!!” aandika Diamond.

Aliongeza “Nililazimika kutoka Juu ya Gari kuwasalimu kabla sijaelekea hotelini…. Nilivotokeza hali ilizidi kuwa mbaya zaidi….Polisi walilazimika kufunga barabara kadhaa mjini bukoba na hata kazi zingine kusimama kwa muda kutokana na watu kuzingira Gari nilokuwepo kila kona nilipokuwa napita”. 
SOURCE:Diamond

KAULI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA BAADA YA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA 16 DAR ES SALAAM

 Picha hii kwa hisani ya maktaba:

 Tarehe 29 Machi 2013, mnamo saa mbili na nusu asubuhi jengo linalojengwa kwenye kiwanja namba 2032/73 Mtaa wa Indira Gandhi lilianguka kutokana na sababu ambazo bado hazijathibitishwa kitaalam na mamlaka husika. Shirika la Nyumba la Taifa linasikitika sana kutokana na kuanguka kwa jengo hilo pamoja na maafa yaliyotokana na tukio hilo la kusikitisha. Pia Shirika linatoa pole kwa wale wote waliofikwa na msiba uliotokana na ajali hii.

Mradi huu wa ubia kati ya NHC na M/s Ladha Construction Limited ya Jijini Dar Es Salaam ulianza kutekelezwa tarehe 4 Februari 2008 ambapo Shirika la Nyumba litakuwa na hisa asilimia 25 na mbia ana asilimia 75 mara baada ya mradi kukamilika. Kwa mujibu wa sera ya ubia iliyoanza kutumika mwaka 1993 na kuhuishwa mwaka 1995 na 2005, Shirika la Nyumba la Taifa lilikuwa likitoa ardhi ambayo ilikuwa ikihesabika kama asilimia 25 ya mtaji wake kwenye jengo husika na mbia alikuwa akipata asilimia 75.

Kwa mujibu wa mkataba huo mbia mwendelezaji M/s Ladha Contruction Limited kama walivyo wabia wengine, anapaswa kabla ya kuanza ujenzi kupata vibali kutoka kwenye mamlaka husika na kuwa na wataalam wa ujenzi na washauri waliokubalika na kuthibitishwa na mamlaka husika. Aidha, mbia huyu akishapata wataalam hao ndiye anayehusika kuingia nao mikataba ya kazi ya kujenga na kusimamia ubora wa jengo husika kwa mujibu wa sheria. Katika mradi huu mbia mwendelezaji aliajiri wataalamu wote waliosajiliwa na Mamlaka husika ambazo ni CRB, ERB, AQRB na Mansipaa husika na mamlaka nyinginezo. Kwa kuwa ujenzi ulikuwa bado haujakamilika, Shirika lilikuwa bado halijapata asilimia 25 ya umiliki wake.

Pia tunapenda kuufahamisha Umma kuwa, Shirika la Nyumba la Taifa, lilisimamisha utoaji wa miradi mipya ya ubia mwaka 2010 ili kuweza kutathimini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa miradi ya ubia na hivyo kuwezesha kutengeneza sera mpya. Kama sehemu ya zoezi hilo, shirika pia lilifuta jumla ya mikataba 64 ambayo ilikuwa imesainiwa lakini haijaanza ujenzi.

Katika sera mpya ambayo utekelezaji wake utaanza hivi karibuni Shirika litahusika moja kwa moja katika kuteuwa mjenzi mtaalam (contractor), msimamizi mtaalam wa mradi husika (consultant) na kusimamia kikamilifu shughuli zote za ujenzi.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa zaidi zitatolewa baada ya vyombo husika kuwasiliana na mjenzi wa mradi huu. Aidha, taarifa zinaweza kupatikana moja kwa moja kutoka M/s Ladha Construction Limited ambaye ndiye mbia mwendelezaji aliyekuwa anasimamia ujenzi huu.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII S.L.P. 2977 Simu: 2851590 DAR ES SALAAM
Telegrams : "NYUMBA" TANZANIA
Fax 2851442



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU